Jaji Samatta: Rais hana kinga kwa mambo aliyoyafanya akiwa Rais bali yale aliyoyafanya kama Rais

Salary Slip

JF-Expert Member
Apr 3, 2012
46,887
143,983
RAIS MSTAAFU ANAWEZA KUFUNGULIWA MASHTAKA NA OFISI YA DPP

Haya yameelezwa na Jaji Mkuu Mstaafu, Barnabas Samatta katika Mjadala wa Uwajibikaji uliandaliwa na Taasisi ya Uwajibikaji iitwayo Wajibu katika Chuo cha Sheria Tanzania(Law School of Tanzania) Jijini Dar es Salaam

Jaji Samatta amefafanua kuwa Rais mstaafu ana kinga lakini ina mipaka. Kinga haihusu mambo aliyofanya akiwa Rais bali yale aliyofanya kama Rais

Ametoa mfano kuwa endapo Rais akifanya vitendo vya kifisadi atakuwa amefanya akiwa Rais kwani kama Rais huwezi kuwa fisadi au kushiriki ufisadi.

Ameyaeleza haya akiwa anasisitiza uhuru wa Ofisi ya Mkurugenzi wa Mashtaka(DPP) kuwa haipaswi kuingiliwa kwa vyovyote vile

Amesema DPP hawajibiki kwa Rais, Waziri Mkuu, Bunge wala Mahakama na si sawa Serikali kuingilia utendaji wake kwani inaweza pelekea kulinda maslahi ya viongozi waovu

Aliongezea kuwa anazungumza hayo kwa kuwa ana uzoefu wa kuwa Mkurugenzi wa Mashtaka kuanzia 1972 hadi 1976
#JFLeo

Chanzo: Ukurasa wa Instagram wa JamiiForums
 
Yuko sahihi Kwenye kuzungumza lakin hayatekelezeki Kwenye Uwanja wa kisheria

Uzi unaotenganisha hayo mambo Mawili ni mwembamba sana

Huo Ufisadi ili aweze kufanya unakuwa Kwenye Wajibu wake wa Urais

Mf. Rais anaweza kusema Tufanye Mradi Fulani let say Ujenzi wa Mradi wa Ununuzi wa Jengo Yeye akaishia hapo
Lakin akatoa Maelekezo Kama Rais nini Cha kufanya

Rejea Sakata la Ununuzi wa Jengo la Ubalozi wa Tanzania Nchini Italy wakati wa Ubalozi wa Prof Mahalu

Mzee Benjamin Mkapa alifika Mahakamani akasema Ni Yeye ndio aliamuru ifanyike 'Single source' Kwenye mchakato wa Ununuzi akaulizwa Na Wakili wa Serikal wapi aliandika akajibu Maelekezo ya Rais sio lazima yawe kimaandishi anamaliza ushahdi huku anacheka kwa dharau Mahakamani

Tukumbuke Ufisadi huwa unafanyika kwa umakini Sana Hata asie Rais kumtia hatiani sio jambo dogo

Rais fisadi tusidhan anapiga Simu kwa Governor Na kuelekeza awekewe Fedha Kwenye Account Fulani, ingekuwa hivyo ingekuwa Rahisi Sana kumtia hatiani
 
A
Na wale vikaragosi vyake na vijibwa koko anavyopenda kuvitumia akiwemo msiba & co.
Mpaka hapa ni wazi anaweza kuwekwa ndani wakati mawakili wanabishana mahakamani juu ya vifungu vya katiba iwapo atapatikana na tuhuma za ufisadi kwani ni wazi kutotokea mvutano ila wakati huo anaweza kuwa teyati yuko ndani nae anasota na akishindwa, ndio atakaa ndani jumla maana kuna makosa tuaambiwa hayana dhamana.
 
Hapana huyu kichaa hana mamlaka ya kutumia hata senti moja toka hazina kama nchini hakuna emergency ya kumlazimisha kuchota bila idhini ya Bunge. Hilo ni kosa ambalo linaweza kabisa kumpandisha kizimbani.

Yuko sahihi Kwenye kuzungumza lakin hayatekelezeki Kwenye Uwanja wa kisheria

Uzi unaotenganisha hayo mambo Mawili ni mwembamba sana

Huo Ufisadi ili aweze kufanya unakuwa Kwenye Wajibu wake wa Urais

Mf. Rais anaweza kusema Tufanye Mradi Fulani let say Ujenzi wa Mradi wa Ununuzi wa Jengo Yeye akaishia hapo
Lakin akatoa Maelekezo Kama Rais nini Cha kufanya

Rejea Sakata la Ununuzi wa Jengo la Ubalozi wa Tanzania Nchini Italy wakati wa Ubalozi wa Prof Mahalu

Tukumbuke Ufisadi huwa unafanyika kwa umakini Sana Hata asie Rais kumtia hatiani sio jambo dogo

Rais fisadi tusidhan anapiga Simu kwa Governor Na kuelekeza awekewe Fedha Kwenye Account Fulani, ingekuwa hivyo ingekuwa Rahisi Sana kumtia hatiani
 
Hapana huyu kichaa hana mamlaka ya kutumia hata senti moja toka hazina kama nchini hakuna emergency ya kumlazimisha kuchota bila idhini ya Bunge. Hilo ni kosa ambalo linaweza kabisa kumpandisha kizimbani.

Umeandika vyema Sana

'...Kama HaKuna emergency ...'

Nani wa kuamua hiyo Kuwa Ni emergency or not

Sheria huwa inatoa mianya Mingi Sana
 
Hakuna mianya yoyote inapokuja kwenye Taifa kuwepo kwenye emergency. Ni lazima Umma utangaziwe kwa kinaga ubaga kuhusu hiyo hali husika na siyo tu kuamua kiholela holela na nchi yetu haijawahi kuwa kwenye emergency kwa miaka mingi.

Umeandika vyema Sana

'...Kama HaKuna emergency ...'

Nani wa kuamua hiyo Kuwa Ni emergency or not

Sheria huwa inatoa mianya Mingi Sana
 
Hivi hichi kizazi cha kina Samatta tutakipata tena Tanzania ?

Pia Rt CJ Samatta kapendekeza mahakama ya mafisadi ibadilishwe jina kwani kwa jina hilo unakuwa tayari ushahukumu mtu ni fisadi ilhali bado ni mtuhumiwa tu .

Sent using Jamii Forums mobile app

Kizazi hiki hakina watu wa level ile

Kwanza Majaji wengi wa zamani walikuwa Na Vitabu vya kisheria walivyotunga Na nilikuwa nondo Kweli Kweli Na unavikuta mpaka Kwenye Maktaba Kubwa Duniani

Mf Hayati Judge Nixon Chipeta
 
Hakuna mianya yoyote inapokuja kwenye Taifa kuwepo kwenye emergency. Ni lazima Umma utangaziwe kwa kinaga ubaga kuhusu hiyo hali husika na siyo tu kuamua kiholela holela na nchi yetu haijawahi kuwa kwenye emergency kwa miaka mingi.

Sawa
 
  • Thanks
Reactions: BAK
Hivi hichi kizazi cha kina Samatta tutakipata tena Tanzania ?

Pia Rt CJ Samatta kapendekeza mahakama ya mafisadi ibadilishwe jina kwani kwa jina hilo unakuwa tayari ushahukumu mtu ni fisadi ilhali bado ni mtuhumiwa tu .

Sent using Jamii Forums mobile app
Ndo tatizo la awamu hii, wana mawazo ya kuhukumu kabla ya kuisubiri mahakama iamue, visasi visasi tu

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Mzee wangu Samatha mimi nakupenda sana na umeongea ukweli mtupu. Lakini nadhani huu ujumbe wako utakufanya ujenge uadui na watawala wa nchi hii.

Speech yako ya ulipokuwa unamaliza Ujaji Mkuu ninayo mpaka leo. Mwaka juzi ukarudia kusema tena pale Ikulu kwamba nchi haiwezi kuwa na maendeleo bila utawala wa sheria.

Kauli zako hazijawahi kupendwa na watawala. Tena kipindi hiki ndiyo nadhani watakutafuta kabisa.
 
19 Reactions
Reply
Back
Top Bottom