Jaji Samatta: Rais hana kinga kwa mambo aliyoyafanya akiwa Rais bali yale aliyoyafanya kama Rais

Salary Slip

JF-Expert Member
Apr 3, 2012
38,113
2,000
RAIS MSTAAFU ANAWEZA KUFUNGULIWA MASHTAKA NA OFISI YA DPP

Haya yameelezwa na Jaji Mkuu Mstaafu, Barnabas Samatta katika Mjadala wa Uwajibikaji uliandaliwa na Taasisi ya Uwajibikaji iitwayo Wajibu katika Chuo cha Sheria Tanzania(Law School of Tanzania) Jijini Dar es Salaam

Jaji Samatta amefafanua kuwa Rais mstaafu ana kinga lakini ina mipaka. Kinga haihusu mambo aliyofanya akiwa Rais bali yale aliyofanya kama Rais

Ametoa mfano kuwa endapo Rais akifanya vitendo vya kifisadi atakuwa amefanya akiwa Rais kwani kama Rais huwezi kuwa fisadi au kushiriki ufisadi.

Ameyaeleza haya akiwa anasisitiza uhuru wa Ofisi ya Mkurugenzi wa Mashtaka(DPP) kuwa haipaswi kuingiliwa kwa vyovyote vile

Amesema DPP hawajibiki kwa Rais, Waziri Mkuu, Bunge wala Mahakama na si sawa Serikali kuingilia utendaji wake kwani inaweza pelekea kulinda maslahi ya viongozi waovu

Aliongezea kuwa anazungumza hayo kwa kuwa ana uzoefu wa kuwa Mkurugenzi wa Mashtaka kuanzia 1972 hadi 1976
#JFLeo

Chanzo: Ukurasa wa Instagram wa JamiiForums
 
nzagambadume

JF-Expert Member
Apr 9, 2018
2,080
2,000
ACHUKULIWE HATUA HUYU SAMATA,ANAICHAFUA NCHI,AKAMATWE HARAKA IKIBIDI ATEKWE,UVCCM HATUKUBALIANI NA MANENO YAKE YANOYADHALILISHA TAASISI TUKUFU YA U RAIS
 
areafiftyone

JF-Expert Member
Jan 4, 2017
7,334
2,000
RAIS MSTAAFU ANAWEZA KUFUNGULIWA MASHTAKA NA OFISI YA DPP

Haya yameelezwa na Jaji Mkuu Mstaafu, Barnabas Samatta katika Mjadala wa Uwajibikaji uliandaliwa na Taasisi ya Uwajibikaji iitwayo Wajibu katika Chuo cha Sheria Tanzania(Law School of Tanzania) Jijini Dar es Salaam

Jaji Samatta amefafanua kuwa Rais mstaafu ana kinga lakini ina mipaka. Kinga haihusu mambo aliyofanya akiwa Rais bali yale aliyofanya kama Rais

Ametoa mfano kuwa endapo Rais akifanya vitendo vya kifisadi atakuwa amefanya akiwa Rais kwani kama Rais huwezi kuwa fisadi au kushiriki ufisadi.

Ameyaeleza haya akiwa anasisitiza uhuru wa Ofisi ya Mkurugenzi wa Mashtaka(DPP) kuwa haipaswi kuingiliwa kwa vyovyote vile

Amesema DPP hawajibiki kwa Rais, Waziri Mkuu, Bunge wala Mahakama na si sawa Serikali kuingilia utendaji wake kwani inaweza pelekea kulinda maslahi ya viongozi waovu

Aliongezea kuwa anazungumza hayo kwa kuwa ana uzoefu wa kuwa Mkurugenzi wa Mashtaka kuanzia 1972 hadi 1976
#JFLeo

Chanzo: Ukurasa wa Instagram wa JamiiForums
DPP na Wabunge ndio wanaotuangusha.
Wapo marais wastaafu waliofanyia Watanzania vituko,lakini wanakula "butter" mtaani,hii haikubaliki.
 
Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Top Bottom