Jaji Samatta: Rais hana kinga kwa mambo aliyoyafanya akiwa Rais bali yale aliyoyafanya kama Rais

Salary Slip

JF-Expert Member
Apr 3, 2012
38,249
2,000
RAIS MSTAAFU ANAWEZA KUFUNGULIWA MASHTAKA NA OFISI YA DPP

Haya yameelezwa na Jaji Mkuu Mstaafu, Barnabas Samatta katika Mjadala wa Uwajibikaji uliandaliwa na Taasisi ya Uwajibikaji iitwayo Wajibu katika Chuo cha Sheria Tanzania(Law School of Tanzania) Jijini Dar es Salaam

Jaji Samatta amefafanua kuwa Rais mstaafu ana kinga lakini ina mipaka. Kinga haihusu mambo aliyofanya akiwa Rais bali yale aliyofanya kama Rais

Ametoa mfano kuwa endapo Rais akifanya vitendo vya kifisadi atakuwa amefanya akiwa Rais kwani kama Rais huwezi kuwa fisadi au kushiriki ufisadi.

Ameyaeleza haya akiwa anasisitiza uhuru wa Ofisi ya Mkurugenzi wa Mashtaka(DPP) kuwa haipaswi kuingiliwa kwa vyovyote vile

Amesema DPP hawajibiki kwa Rais, Waziri Mkuu, Bunge wala Mahakama na si sawa Serikali kuingilia utendaji wake kwani inaweza pelekea kulinda maslahi ya viongozi waovu

Aliongezea kuwa anazungumza hayo kwa kuwa ana uzoefu wa kuwa Mkurugenzi wa Mashtaka kuanzia 1972 hadi 1976
#JFLeo

Chanzo: Ukurasa wa Instagram wa JamiiForums
 
Yamakagashi

JF-Expert Member
Sep 19, 2016
8,682
2,000
Mzee wangu Samatha mimi nakupenda sana na umeongea ukweli mtupu. Lakini nadhani huu ujumbe wako utakufanya ujenge uadui na watawala wa nchi hii.
Mzee huyu haogopi ni kaiva kweli kweli ingekuwa kwenye field zetu kule angekuwa 5 Star General

Hababaishwi unakumbuka kikao cha Ikulu Magufuli alipoita wazee ?

Samatta kama kawaida alisimamia ukweli na bila kuogopa chochote

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Papushikashi

JF-Expert Member
Feb 28, 2016
8,061
2,000
Yuko sahihi Kwenye kuzungumza lakin hayatekelezeki Kwenye Uwanja wa kisheria

Uzi unaotenganisha hayo mambo Mawili ni mwembamba sana

Huo Ufisadi ili aweze kufanya unakuwa Kwenye Wajibu wake wa Urais

Mf. Rais anaweza kusema Tufanye Mradi Fulani let say Ujenzi wa Mradi wa Ununuzi wa Jengo Yeye akaishia hapo
Lakin akatoa Maelekezo Kama Rais nini Cha kufanya

Rejea Sakata la Ununuzi wa Jengo la Ubalozi wa Tanzania Nchini Italy wakati wa Ubalozi wa Prof Mahalu

Mzee Benjamin Mkapa alifika Mahakamani akasema Ni Yeye ndio aliamuru ifanyike 'Single source' Kwenye mchakato wa Ununuzi akaulizwa Na Wakili wa Serikal wapi aliandika akajibu Maelekezo ya Rais sio lazima yawe kimaandishi anamaliza ushahdi huku anacheka kwa dharau Mahakamani

Tukumbuke Ufisadi huwa unafanyika kwa umakini Sana Hata asie Rais kumtia hatiani sio jambo dogo

Rais fisadi tusidhan anapiga Simu kwa Governor Na kuelekeza awekewe Fedha Kwenye Account Fulani, ingekuwa hivyo ingekuwa Rahisi Sana kumtia hatiani
Mfano tuchukulie kabla hajawa raisi alifanya ufisadi kama kuuza mali ya serikali kama Majengo na ikadhibitika kweli ulikuwa ufisadi...vp anaweza kushitakiwa?

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Regnatus Cletus

JF-Expert Member
May 26, 2018
1,116

Mahakama itaamua, sio wewe.
 
GSL

JF-Expert Member
Oct 19, 2010
284
500
Mf Hayati Judge Nixon Chipeta[/QUOTE]
Aliitwa Buxton David Chipeta. Sio Nixon.
Nimeishi naye kama jirani akiwa Mahakama Kuu Tabora (akiwa na akina Marando, Mushi na Rubama).
Hawa, pamoja na akina Katiti, Rugakingira, etc walikuwa very seroius na kazi yao....no wonder walikuwa wa kuhesabu.
 
Gulwa

JF-Expert Member
Jun 16, 2008
5,043
2,000
RAIS MSTAAFU ANAWEZA KUFUNGULIWA MASHTAKA NA OFISI YA DPP
-
Haya yameelezwa na Jaji Mkuu Mstaafu, Barnabas Samatta katika Mjadala wa Uwajibikaji uliandaliwa na Taasisi ya Uwajibikaji iitwayo Wajibu katika Chuo cha Sheria Tanzania(Law School of Tanzania) Jijini Dar es Salaam
-
Jaji Samatta amefafanua kuwa Rais mstaafu ana kinga lakini ina mipaka. Kinga haihusu mambo aliyofanya akiwa Rais bali yale aliyofanya kama Rais
-
Ametoa mfano kuwa endapo Rais akifanya vitendo vya kifisadi atakuwa amefanya akiwa Rais kwani kama Rais huwezi kuwa fisadi au kushiriki ufisadi.
-
Ameyaeleza haya akiwa anasisitiza uhuru wa Ofisi ya Mkurugenzi wa Mashtaka(DPP) kuwa haipaswi kuingiliwa kwa vyovyote vile
-
Amesema DPP hawajibiki kwa Rais, Waziri Mkuu, Bunge wala Mahakama na si sawa Serikali kuingilia utendaji wake kwani inaweza pelekea kulinda maslahi ya viongozi waovu
-
Aliongezea kuwa anazungumza hayo kwa kuwa ana uzoefu wa kuwa Mkurugenzi wa Mashtaka kuanzia 1972 hadi 1976
#JFLeo

Chanzo: Ukurasa wa Instagram wa JamiiForums
Kumbe ndio maana jiwe kajaza wasukuma ili asishitakiwe kwa uovu wake
 
BAK

JF-Expert Member
Feb 11, 2007
99,322
2,000
We’re on the same page Mkuu. I wish we had more people like him in our beautiful country to tell the TRUTH and nothing but THE WHOLE TRUTH.

Nakwambia ukweli kabisa, Mzee Samatha ni moja ya majaji wa kipekee sana Tanzania. Lakini sidhani kama huu ujumbe wake utapokelewa vizuri na watawala.

Jaji Warioba alipoonyesha nia ya kuwasaidia watanzania wa vizazi vijavyo alipogwa kibao na Paul Makonda. Sasa unategema Samatha atapona.
 
Kataskopos

JF-Expert Member
Jul 26, 2012
15,952
2,000
Mzee huyu haogopi ni kaiva kweli kweli ingekuwa kwenye field zetu kule angekuwa 5 Star General

Hababaishwi unakumbuka kikao cha Ikulu Magufuli alipoita wazee ?

Samatta kama kawaida alisimamia ukweli na bila kuogopa chochote

Sent using Jamii Forums mobile app
Hata Jaji Warioba naye ameiva sana lakini alipigwa kibao na Paulo Makonda, Mkuu wa Mkoa wa Dar es salaam. Ule ulikuwa ni utawala wa JK, unadhani kwenye utawala huu atapona kweli ???

No body is safe hapa Tanzania kwasasa...
 
Papushikashi

JF-Expert Member
Feb 28, 2016
8,061
2,000
Kizazi hiki hakina watu wa level ile

Kwanza Majaji wengi wa zamani walikuwa Na Vitabu vya kisheria walivyotunga Na nilikuwa nondo Kweli Kweli Na unavikuta mpaka Kwenye Maktaba Kubwa Duniani

Mf Hayati Judge Nixon Chipeta
Natamani tungekuwa na mijadala ya hoja kama hivi bila kupigana risasi, kutekana na kutishiana

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Pohamba

JF-Expert Member
Jun 2, 2015
22,572
2,000
Mfano tuchukulie kabla hajawa raisi alifanya ufisadi kama kuuza mali ya serikali kama Majengo na ikadhibitika kweli ulikuwa ufisadi...vp anaweza kushitakiwa?

Sent using Jamii Forums mobile app
Hapo anashtakiwa bila ya Shida yeyote

Changamoto ipo Kwenye kuamua kosa lipi kafanya akiwa Rais Na lipi kafanya Kama Rais!

Sio Kazi nyepesi ila ninachojua Mara nyingi wanaoumia Ni Wasaidizi wa Rais ambao wao hawana Kinga Na Mara nyingi Maelekezo huwa wanapewa kwa Mdomo hivyo Ni Rahisi Mtawala akakuruka

Mf imekuja kandarasi ya Ujenzi wa Barabara anakuitia ofisin anakukutanisha Na Mkandarasi anakwambia 'angalia namna ya kumsaidia huyu'
Hapo kamaliza sasa Wewe unaenda kufanya juu chini mpaka unampa yule Kandarasi likija kubutuka Kuwa Mchakato umekiukwa unakaangwa Wewe sio yule aliekupa Maelekezo ya Mdomo
 
mrangi

JF-Expert Member
Feb 19, 2014
47,919
2,000
Yuko sahihi Kwenye kuzungumza lakin hayatekelezeki Kwenye Uwanja wa kisheria

Uzi unaotenganisha hayo mambo Mawili ni mwembamba sana

Huo Ufisadi ili aweze kufanya unakuwa Kwenye Wajibu wake wa Urais

Mf. Rais anaweza kusema Tufanye Mradi Fulani let say Ujenzi wa Mradi wa Ununuzi wa Jengo Yeye akaishia hapo
Lakin akatoa Maelekezo Kama Rais nini Cha kufanya

Rejea Sakata la Ununuzi wa Jengo la Ubalozi wa Tanzania Nchini Italy wakati wa Ubalozi wa Prof Mahalu

Mzee Benjamin Mkapa alifika Mahakamani akasema Ni Yeye ndio aliamuru ifanyike 'Single source' Kwenye mchakato wa Ununuzi akaulizwa Na Wakili wa Serikal wapi aliandika akajibu Maelekezo ya Rais sio lazima yawe kimaandishi anamaliza ushahdi huku anacheka kwa dharau Mahakamani

Tukumbuke Ufisadi huwa unafanyika kwa umakini Sana Hata asie Rais kumtia hatiani sio jambo dogo

Rais fisadi tusidhan anapiga Simu kwa Governor Na kuelekeza awekewe Fedha Kwenye Account Fulani, ingekuwa hivyo ingekuwa Rahisi Sana kumtia hatiani
Ndomana mnambiwa inahitajika katiba mpya

Ova

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Top Bottom