Jaji Samata akiri katiba iliyopo ina mapungufu makubwa | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Jaji Samata akiri katiba iliyopo ina mapungufu makubwa

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by Biz2geza, Nov 17, 2011.

 1. Biz2geza

  Biz2geza Senior Member

  #1
  Nov 17, 2011
  Joined: Oct 12, 2011
  Messages: 117
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  leo jaji mstaafu barnabas samatta amefunguka na kudai kuwa katiba ya sasa inamapungufu makubwa na inawapa baadhi ya watu madaraka makubwa ambayo yanawafanya kuwa madikteta. Mambo aliyogusia ni pamoja na
  1. Raisi kuwa na madaraka makubwa katika katiba
  2. Tume ya uchaguzi kuwa idara ndani ya serikali kitu ambacho kinaifanya kutokuwa huru
  3. Spika wa bunge kutoka kwenye chama cha siasa kitu ambacho kinamfanya kuonyesha upendeleo wa dhairi.
  Mwisho hakasema mchakato wa kwenda kwenye katiba mpya lazima uwe wa uhuru na amani na kila mwananchi ashirikishwe.
  Mytake.
  Haya maoni ambayo yanatolewa na watu maarufu kama magamba hawatayasikia basi lakuvunda halina ubani.
  Source.itv news
   
 2. Losambo

  Losambo JF-Expert Member

  #2
  Nov 17, 2011
  Joined: Nov 8, 2011
  Messages: 2,623
  Likes Received: 8
  Trophy Points: 0
  Jaji mstaafu Samata akiri katiba iliyopo kuwa na mapungufu makubwa.

  Moja ya mapungufu hayo ametaja ni tume ya uchaguzi kwa nini iwe idara ndani ya serikali? Ametaka iwe huru kutoka serikalini.

  Katika mjadala Dr. W.Slaa akikoleza kwa kusema ni lazima katiba ifafanue wazi kuhusu umiliki wa ardhi na mambo mengine mengi ambayo bado ni tata.

  Hata hivyo wadau mbali mbali waliochangia katika mjadala huo wameponda tabia ya wabunge wa CCM kuacha kujadili hoja za msingi na kujadili watu hasa Tundu Lissu ambaye anaonekana mwiba katika zoezi zima la muswada wa katiba.

  Source ITV habari 20:00.

  Nawasilisha.
   
 3. Gagurito

  Gagurito JF-Expert Member

  #3
  Nov 17, 2011
  Joined: Feb 11, 2011
  Messages: 5,610
  Likes Received: 25
  Trophy Points: 135
  Yeah! Twajua inamapungufu bt angependekeza njia mpadala ya kuyatatua or angekemea bei kitendo kinachoendelea bungeni dodoma!
   
 4. Chimunguru

  Chimunguru JF-Expert Member

  #4
  Nov 17, 2011
  Joined: May 3, 2009
  Messages: 9,843
  Likes Received: 270
  Trophy Points: 180
  aisee nimefurahi saaana hata maoni ya wachangiaji yanaonesha jinsi watu walivyo na hasira na muswada mbovu!
   
 5. M

  Malunde-Malundi JF-Expert Member

  #5
  Nov 17, 2011
  Joined: Jan 10, 2008
  Messages: 1,287
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Nimekuta anamalizikia mchungaji mooja kwa hasira ebu tupe update zaidi maana haya magamba yanahitaji strong pre emptive. Barnabas kwa kweli mie namuona kama profesor na guru anayetumia sana vema taaluma
   
 6. j

  jigoku JF-Expert Member

  #6
  Nov 17, 2011
  Joined: Sep 9, 2011
  Messages: 2,347
  Likes Received: 80
  Trophy Points: 145
  Mkuu nimeingalia taarifa hiyo na kuisikia vizuri na nimesikia washiriki wengine ambao wako kada za wananchi wa kawaida lakini hakuna aliefurahishwa na yale yanayofanywa na wabunge wa CCM kule Dodoma,najiuliza kule waliko je wameingalia taarifa hiyo?au wametune TV inayotangaza habari za kujipendekeza kwao bila kutangaza taarifa zinazowapa changamoto.Lakini Jaji Samata amemaliza kila kitu.Ila nilishituka kwa hotuba ya makamu wa rais Dr Bilal,una mlengo wa kupinga kile kinachosemwa na kambi ya upinzani pamoja na jukwaa la katiba,ila aibu imewashika wale wote wanaowaona Chadema wanaopinga vikali mswada huo na baadhi yao tunapinga vikali hata tulioko nje ya bunge
   
 7. Losambo

  Losambo JF-Expert Member

  #7
  Nov 17, 2011
  Joined: Nov 8, 2011
  Messages: 2,623
  Likes Received: 8
  Trophy Points: 0
  Mkuu hata mimi nimeona hiyo habari na kurusha thread nadhani MoDs wataiunganisha na hii kwa kuwa yako ndiyo iliyowahi lakini kiukweli nimefurahishwa sana na maoni ya yule jaji mstaafu.
  Nilikuwa namuona makamu wa rais Dr. Bilal akifuka moshi katika ufunguzi huku dhahiri akiona aibu!!!
   
 8. Biz2geza

  Biz2geza Senior Member

  #8
  Nov 17, 2011
  Joined: Oct 12, 2011
  Messages: 117
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  gagurito.jaji samatta ametoa mapendekezo yake kuanzia kwenye mchakato mpaka katiba yenyewe,zoezi liwe na ushirikishwaji wananchi,madaraka ya raisi yapunguzwe,spika asitoke kwenye chama cha siasa na tume ya uchaguzi iwe huru.
   
 9. mpapai

  mpapai New Member

  #9
  Nov 17, 2011
  Joined: Apr 10, 2011
  Messages: 2
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Huyu jaji mnafiki, mbona wakati akiwa kazini hakulisema hili wakati alikuwa na madaraka
   
 10. Losambo

  Losambo JF-Expert Member

  #10
  Nov 17, 2011
  Joined: Nov 8, 2011
  Messages: 2,623
  Likes Received: 8
  Trophy Points: 0
  Siyo kwamba hajaelewa ila alitaka ipondwe CDM ili afurahi.
   
 11. j

  jigoku JF-Expert Member

  #11
  Nov 17, 2011
  Joined: Sep 9, 2011
  Messages: 2,347
  Likes Received: 80
  Trophy Points: 145
  Kwa ujasiri aliokuwa nao wakati wa kutoa mada najua atakuwa amependekeza nini kifanyike na hata hivyo kumbuka waandisha huwa wana uhuru wa kuchagua angle ya kuripotia,aidha kama amekiri kuwa ni mbovu na inampa raisi kuwa dikteta basi jibu tunalo alilotoa Lisu ndo tulifanyie kazi.ila kwa kuwa CCM ni magamba na ni viziwi najua hawatayafanyia kazi mawazo hayo.Na kama hawajasoma alama za nyakati basi mie nitaamini 100%CCM ni laana pamoja na wote wanaoishabikia,kwani katika mjadala huo ambao makamu wa raisi alikuwepo kuna mchangiaji ameeleza jinsi wabunge wa CCM walivyokuwa wanahara huko bungeni ,mchangiaji huyo hakusita kuonyesha hasira zake mbele ya Bilal pale aliposema alitaka kuipiga teke TV baada ya kuangalia kile kilichosemwa na mbunge wa ccm kule dodoma
   
 12. palalisote

  palalisote JF-Expert Member

  #12
  Nov 17, 2011
  Joined: Aug 4, 2010
  Messages: 8,352
  Likes Received: 37
  Trophy Points: 0
  waache tu ccm wasipokubali kuiondoa hapo bungeni, basi wananchi tutaandaaa katiba yetu
   
 13. Nyangomboli

  Nyangomboli JF-Expert Member

  #13
  Nov 17, 2011
  Joined: Nov 24, 2010
  Messages: 2,307
  Likes Received: 649
  Trophy Points: 280
  kwani weye hujui kama jaji huapishwa na kuahidi kuilinda na kuienzi katiba? angeanzia wapi?
   
 14. de'levis

  de'levis JF-Expert Member

  #14
  Nov 17, 2011
  Joined: Nov 14, 2011
  Messages: 1,188
  Likes Received: 380
  Trophy Points: 180
  wazee wameongea ukweli mtupu ila magamba mabshi kweli
   
 15. Losambo

  Losambo JF-Expert Member

  #15
  Nov 17, 2011
  Joined: Nov 8, 2011
  Messages: 2,623
  Likes Received: 8
  Trophy Points: 0
  Naona zile zilikuwa ni salamu tosha kwa madr wote, yaani Dr. JK na Dr. Balal.
   
 16. de'levis

  de'levis JF-Expert Member

  #16
  Nov 17, 2011
  Joined: Nov 14, 2011
  Messages: 1,188
  Likes Received: 380
  Trophy Points: 180
  wasipoiondoa itakula kwao ngoja hiyo kesho maana wamekuwa wanaahirisha kufunga huo mjadala
   
 17. BBJ

  BBJ JF-Expert Member

  #17
  Nov 17, 2011
  Joined: Sep 2, 2011
  Messages: 1,183
  Likes Received: 9
  Trophy Points: 135
  Kwakweli hata Mimi Judge Samatta kanifurahisha sana kwa points alizozitoa,ila kuna jamaa ni MKULIMA,amesema anashangaa WABUNGE wa CCM badala ya kujikita ktk hoja wao Tundu Lissu mara Kibanda kana kwamba hao watu ndio muswada uliokua unajadiliwa.Poor CCM,
   
 18. Losambo

  Losambo JF-Expert Member

  #18
  Nov 17, 2011
  Joined: Nov 8, 2011
  Messages: 2,623
  Likes Received: 8
  Trophy Points: 0
  Ndiyo maana Zitto Kabwe kawapa angalizo la kutopuuza madai ya CDM kwani endapo watapuuza wataanza mchakato wa kuunda ya kwao.
   
 19. Filipo

  Filipo JF-Expert Member

  #19
  Nov 17, 2011
  Joined: Jan 6, 2011
  Messages: 9,329
  Likes Received: 210
  Trophy Points: 160
  Nimemwona nikajiuliza kama magamba nao wamesikiliza. Maana tukisema sisi tunaambiwa ni cdm! Kwani cdm si watu.
  Wote tunakumbuka udikteta wa ma dc na ma rc. Tuliona walimu wakichapwa viboko. Tunaona rc Arusha akilazimisha bendera za cdm zishushwe kwenye matawi ya chama huko Arumeru! Tumemsikia Mbunge akilalamika dc kuingia kwenye boma na kuchukua mbuzi na ng'ombe kama wake. Huu udikteta unalindwa na katiba. Halafu tunaletewa mswada unaomwongezea rais udikteta! Tukikataa kuujadili, bunge linageuka "lango la jiji"

  Acha watutukane wanavyotaka, watudharau, watudhalilishe, lakini hoja ya msingi inabaki palepale, Hatuutaki huo mswada!
   
 20. de'levis

  de'levis JF-Expert Member

  #20
  Nov 17, 2011
  Joined: Nov 14, 2011
  Messages: 1,188
  Likes Received: 380
  Trophy Points: 180
  wautumie usiku huu vizuri na wawaze vizuri ili wauondoe huo mswaada..vinginevyo sii tutawaonyesha kuwa katiba ni ya wananchi wote
   
Loading...