Mystery
JF-Expert Member
- Mar 8, 2012
- 15,477
- 30,137
Tumeshuhudia moja ya uamuzi wa kihistoria katika mahakama zetu, baada ya Jaji Sam Rumanyika wa Mahakama Kuu kutoa uamuzi kuwa akina Mbowe waliendekea kusota rumande kwa sababu binafsi na wala si kwa sababu za kisheria, kwa wao kufutiwa dhamana waliyokuwa wamepewa kisheria na mahakama ya Kisutu na hivyo kusababisha akina Mbowe kuendelea kusota rumande kwa kipindi cha zaidi ya miezi mitatu
Pili hata uamuzi wake Jaji Rumanyika wa kutengua uamuzi wa mahakama yake ya chini ya kisutu kuwa akina Mbowe hawahitajiki tena kuwa wanaripoti kila wiki mahakamani hapo na badala yake akaamuru kuwa wanapaswa wawe wanaripoti Mara moja tu kwa mwezi pia ni wa kihistoria
Nadhani ingekuwa vyema kwa Mahakama kuu baada ya kuona kuwa akina Mbowe wameendelea kusota rumande kwa sababu binafsi na wala siyo kwa sababu za kisheria kwa aliyekuwa Hakimu Mkazi Mkuu, Wilbard Mashauri aliyetoa hukumu ya kuwafutia dhamana akina Mbowe naye angepewa adhabu na mahakama hiyo ili liwe fundisho kwa wale wote wanaozitumia mahakama hizo kwa sababu zao binafsi.
Kwa kweli ni jambo linalohuzunisha sana tena sana kwa mtu kama Freeman Mbowe na mbunge mwenzake wa Chadema, Esther Matiko ambao mahakama kuu imethibitisha pasipo shaka yoyote kuwa wamekomolewa kwa kukaa rumande kwa kipindi chote hicho
Vile vile Jeshi letu la Polisi nalo lingewajibika kwa vitendo vyake vya kiuonezi vya kuwakamata holela viongozi wa upinzani, hususani kutoka chama kikuu cha upinzani cha Chadema na kuwaburuza mahakamani kwa kile wanachokiita kuwa ni sababu za kijinai kuwa wanatumia lugha za uchochezi, wakati katika hali halisi ni za kisiasa kwa kuwa nchi yetu ipo kwenye mfumo wa kidemokrasia na ni wa vyama vingi ambapo wapinzani wao wakuu wa Chama cha CCM walipaswa kuzijibu kwenye majukwaa ya kisiasa,i kama inavyoainishwa katika Katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania wa Tanzania, 1977, ibara ya 3(1) ili liwe fundisho kwa mamlaka zote zinazopenda kuisigina Katiba ya nchi yetu waziwazi kwa manufaa yao binafsi
Kama ungetolewa uamuzi huo ungekuwa fundisho kubwa ili vyombo hivyo visirudie tena makosa wanayoyafanya kwa lengo la kukomoana