Jaji Salome Kaganda ateuliwa Kamishna wa Maadili ya Viongozi wa Umma

Halisi

JF-Expert Member
Jan 16, 2007
2,812
1,250
DIRECTORATE OF PRESIDENTIAL COMMUNICATIONS
UNITED REPUBLIC OF TANZANIA

Telephone: 255-22-2114512, 2116898
E-mail: press@ikulu.go.tz
Fax: 255-22-2113425PRESIDENT’S OFFICE,
THE STATE HOUSE,
P.O. BOX 9120,
DAR ES SALAAM.
Tanzania.
TAARIFA KWA VYOMBO VYA HABARI


Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mheshimiwa Jakaya Mrisho Kikwete amemteua Jaji Mstaafu Salome Suzette Kaganda kuwa Kamishna wa Maadili ya Viongozi wa Umma.

Taarifa iliyotolewa Ikulu, Dar es Salaam, leo, Jumatano, Desemba 8, 2010, na Katibu Mkuu Kiongozi, Mheshimiwa Phillemon Luhanjo, inasema kuwa uteuzi huo ulianza Jumamosi, Desemba 4, 2010.

Jaji Mstaafu Salome Kaganda anachukua nafasi iliyoachwa wazi na Jaji Mstaafu Stephen Ihema ambaye amemaliza muda wake.

Kabla ya kustaafu, Mheshimiwa Salome Suzette Kaganda alikuwa Jaji Mfawidhi wa Mahakama Kuu, Kanda ya Kusini, Songea.

Imetolewa na:

Kurugenzi ya Mawasiliano ya Rais,
Ikulu,
DAR ES SALAAM.

08 Desemba, 2010
 

Mr. Zero

JF-Expert Member
Jun 5, 2007
12,679
2,000
DIRECTORATE OF PRESIDENTIAL COMMUNICATIONS
UNITED REPUBLIC OF TANZANIA

Telephone: 255-22-2114512, 2116898
E-mail: press@ikulu.go.tz
Fax: 255-22-2113425PRESIDENT'S OFFICE,
THE STATE HOUSE,
P.O. BOX 9120,
DAR ES SALAAM.
Tanzania.
TAARIFA KWA VYOMBO VYA HABARI


Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mheshimiwa Jakaya Mrisho Kikwete amemteua Jaji Mstaafu Salome Suzette Kaganda kuwa Kamishna wa Maadili ya Viongozi wa Umma.

Taarifa iliyotolewa Ikulu, Dar es Salaam, leo, Jumatano, Desemba 8, 2010, na Katibu Mkuu Kiongozi, Mheshimiwa Phillemon Luhanjo, inasema kuwa uteuzi huo ulianza Jumamosi, Desemba 4, 2010.

Jaji Mstaafu Salome Kaganda anachukua nafasi iliyoachwa wazi na Jaji Mstaafu Stephen Ihema ambaye amemaliza muda wake.

Kabla ya kustaafu, Mheshimiwa Salome Suzette Kaganda alikuwa Jaji Mfawidhi wa Mahakama Kuu, Kanda ya Kusini, Songea.

Imetolewa na:

Kurugenzi ya Mawasiliano ya Rais,
Ikulu,
DAR ES SALAAM.

08 Desemba, 2010

Hivi hili tatizo la kuchanganya lugha litakwisha lini??
 

czar

JF-Expert Member
Oct 11, 2010
340
0
Uzuzu tu, wanajua kiswahili vizuri kibaya inatoka ofisini tena ofisi kubwa kabisa AIBUUU!
 

BLUE BALAA

JF-Expert Member
Nov 30, 2010
1,155
2,000
Headed paper za kiswahili zimekwisha ikabidi waichakachue ile ya kingereza
 

Ngambo Ngali

JF-Expert Member
Apr 17, 2009
3,518
2,000
Hivi hili tatizo la kuchanganya lugha litakwisha lini??

Mimi naona tatizo sio kuchanganya lugha, hapa tatizo ni kuendelea na chuma chakavu syndrome(ccs), recycling phenomenon(rp) call it by any name. Kama mtu amestaafu ajira serikalini inabidi akae nyumbani na wajukuu wake sio kuanza tena kuzunguka kwenye ofisi za serikali kuendelea kufanya kazi za serikali.

Hii inatokana na madaraka makubwa ambayo rais anayo chini ya Katiba, uteuzi huu hauwi vetted, hauwezi kuulizwa popote. Nafasi haikutangazwa, kama ingetangazwa kuna watanzania wengi tu wangeweza kujaza hiyo nafasi. Wastaafu wanahitajika pale ambapo hakuna watu wenye qualification wa unri husika.

Ndio maana wananchi wanataka katiba mpya kuondokana na ccs na rp
 

Rutashubanyuma

JF-Expert Member
Sep 24, 2010
203,226
2,000
Ateuliwa kuongoza Tume ya Maadili ya Viongozi wa Umma

Wednesday, 08 December 2010 19:15 newsroom
Na Mwandishi Wetu
RAIS Jakaya Kikwete amemteua Jaji mstaafu Salome Kaganda kuwa Kamishna wa Maadili ya Viongozi wa Umma
Taarifa iliyotolewa na Ikulu, mjini Dar es Salaam, jana na Katibu Mkuu Kiongozi, Phillemon Luhanjo, ilisema uteuzi huo ulianza Desemba 4, mwaka huu. Jaji Salome anachukua nafasi iliyoachwa wazi na Jaji mstaafu Stephen Ihema ambaye amemaliza muda wake.
Kabla ya kustaafu, Jaji Salome alikuwa Jaji Mfawidhi wa Mahakama Kuu, Kanda ya Kusini, Songea.
 

Iza

JF-Expert Member
Jan 8, 2009
1,981
2,000
Sasa kwa aina hii ya viongozi wanaowekwa wakati ni wastaafu..unategemea wazo jipya lijitapita hapo..
Hata sijui ni maadili gani yanasimamiwa manake tunaona yanavunjwa kila leo..
 

BONGOLALA

JF-Expert Member
Sep 14, 2009
16,528
2,000
vijana tuna nafasi kweli ktk utawala huu?wazee wanastaafu wanarudishwa serikalini kiaina kwani kuna upungufu wa wanasheria kiasi hicho?mtu anastaafu mara anachaguliwa kuwa balozi nchi fulani.jee consultations nani atafanya?
 

DENYO

JF-Expert Member
Sep 14, 2010
698
195
sijui kama atawaweza mafisadi na masultani au atafunika kombe zimwi wapite
 

Mwawado

JF-Expert Member
Nov 2, 2006
998
195
Moja ya kazi kubwa ya Kamisheni hii ni kupitia na kuangalia mali za Viongozi kama walivyojaza katika Fomu zao za Maadili.Kiongozi aliyemaliza muda wake hapo Jaji Mstaafu Stephen Ihema alishindwa kabisa kusimamia hilo,ilifika mpaka wafanyakazi wa Kamisheni hiyo kulalamika Ofisi ya Waziri Mkuu na baadaye Ikulu,lakini Jaji huyo aliachiwa nafasi hiyo kwa miaka 10 (Aliteuliwa oktoba/2005) mpaka leo tunaposikia uteuzi mwingine wa Jaji Salome Kaganda.Ni wazi Mama huyu atajaribu kuangalia utajiri mkubwa wa Viongozi wa serikali unatoka wapi?Isije ikawa kitengo hichi kinachowekwa wanasheria waliobobea kinalinda na kusimami mali dhalimu za Viongozi.
 

Mtego wa Noti

JF-Expert Member
Nov 27, 2010
2,480
2,000
hamna kitu hapa zaidi ya kulipana fadhila..watu tunakamuliwa na jua mtaani halafu watu wanastaaf na kurudishwa kazini... upuuzi mtupu...
 

Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Top Bottom