Jaji Ramadhani et al wameiua mahakama kwa mikono yao | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Jaji Ramadhani et al wameiua mahakama kwa mikono yao

Discussion in 'Jukwaa la Sheria (The Law Forum)' started by Mnyamahodzo, Jun 21, 2010.

 1. Mnyamahodzo

  Mnyamahodzo JF-Expert Member

  #1
  Jun 21, 2010
  Joined: May 23, 2008
  Messages: 1,854
  Likes Received: 220
  Trophy Points: 160
  Jaji Mkuu Augustine Ramadhani kama kiongozi mkuu wa mhimili wa serikali, MAHAKAMA, pamoja na wenzake wamefanyakosa la wazi(sijui walikuwa wanajua au hawajui) la kuuwa mhimili huu pale walipotoa hukumu yao juu kesi iliyokwisha amuliwa awali na Mahakama Kuu ya mgombea binafsi.
  Kutokana na Bunge kuanza kuleta heshima yake taratibu hasa katika awamu hii ya Mh. Sitta, na baada ya ya Jaji mkuu kutoa maelezo namna alivyoweza kukwepa kutumia bilioni ya shilingi kwa kuikarabati nyumba ya Jaji Mkuu, sasa ndio ulikuwa wakati muafaka wa kufunga goli la penati na kuutangazia umma nguvu ya mhimili huu katika Tanzania. Lakini ikawa tofauti, wakaipoteza fursa muhimu (wamepiga pembeni ya goli taratibu na kupiga kelele kipa gusa ili iwe kona; hatimae imekuwa kona). Fursa itakayoigharimu si nchi tu bali na mahakama yenyewe.Wamejimaliza.

  Tusije sikia tena mtu wa mahakama ansema serikali inawaingilia kazi za ilihali wao ni sehemu ya CCM waliopanga mkakati wa kuiangamiza haki ya wananchi na kuidhohofisha taaluma ya sheria.

  Majaji sita wameiua Mahakama katika enzi zetu mbele ya macho yetu, na kuutupa mzigo kwa Bunge lililokwisha timiza wajibu wake awali japo unadosari. Wameshindwa kutafsiri sheria, wakakubali kupindisha sheria, wakaamua kuuwa mhimili for the sake of politikisi....lol

  Wanasheria mtaibukia wapi kuonyesha mhimili wenu/wetu huu wa Mahakama una nguvu?
   
 2. F

  Fungu la kukosa Member

  #2
  Jun 21, 2010
  Joined: Jun 16, 2009
  Messages: 64
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Hapa Bongo mambo yote ni kulindana tu ndugu zangu kuanzia affisi ya mtendaji kata had Mahakama kuu. Kwanza ilikarabatiwa nyumba ya Gavana wa Benk kuu kwa mabilioni ya wavuja jacho na sasa nyumba za wanasheria siku za mbele tutaambiwa nyumba za Wakurugenzy na Mameneja wao hii ndiyo hali halisi ya nchu yetu.
  Mungu apishe mbali
   
 3. Buchanan

  Buchanan JF Diamond Member

  #3
  Jun 21, 2010
  Joined: May 19, 2009
  Messages: 13,203
  Likes Received: 371
  Trophy Points: 180
  Hawa Majaji walikuwa saba (7) sio sita (6). Hata hivyo nakuunga mkono kwamba Mahakama imejimaliza, nimepunguza imani sana na CJ na Jopo lake! Sijui tukimbilie wapi sasa, Serikali yenyewe haitaki Mgombea binafsi, Bunge lenyewe limejaa wapambe wa Serikali, Mahakama tuliyokuwa tunaitegemea kumbe ni vuvuzela!
   
 4. K

  Kilian Senior Member

  #4
  Jun 22, 2010
  Joined: Apr 26, 2009
  Messages: 147
  Likes Received: 8
  Trophy Points: 35
  Tatizo ni pale jaji anapoteuliwa na Raisi na kuthibitishwa na Rais mwnyewe, no challenge.
  On America, Raisi anamteua jaji lakini nilazima athibitishwe na Bunge. Bunge lina uwezo wa kumkataa. Hivyo huyu anawajibika kwa wananchi kwani wanauwezo wa kuhoji utendaji wake. Hapa kwetu anapewa nafasi hiyo na raisi ili amlinde yeye na waandamizi wake. No one can challenge his credibility .

  Mpaka tutakapokuwa na tume huru, mahakama huru pomoja navyombo vyote vya sheria ambavyo haviwajibiki kwa raisi bali kwa katiba ya nchi ndo tunaweza kusonga mbele.
   
 5. Mnyamahodzo

  Mnyamahodzo JF-Expert Member

  #5
  Jun 22, 2010
  Joined: May 23, 2008
  Messages: 1,854
  Likes Received: 220
  Trophy Points: 160
  Hivi ile kesi ya NCCR-Mageuzi ya kutaka tume ya uchaguzi ivunjwe kwa kuwa Mwenyekiti wake alichaguliwa na mgombea wa kiti cha urais wa sasa imeishaje?
   
 6. Mwanamayu

  Mwanamayu JF-Expert Member

  #6
  Jun 22, 2010
  Joined: May 7, 2010
  Messages: 7,945
  Likes Received: 2,090
  Trophy Points: 280
  Ni kweli mahakama imejimaliza kwani imeshindwa kutoa hukumu inayoendana na katiba ya nchi yetu. Mahakama ya katiba inashughulikia ubishi utakaozuka kati ya serikali ya TZ bara na Zanzibar na sio kati ya mwananchi na serikali kuhusu mambo ya katiba. Mbona haki nyingine wanasimamia ijekuwa ya mgombea binafsi? Sasa naweza kupanga mihimili hii mitatu kutokana na nguvu zake - kwanza 'the executive', pili 'parliament' na tatu na mwisho 'court'. Wa kwanza na wa pili kidogo wanapimana nguvu kwani kila mmojawao anaweza kupiga chini mwenziwe, ila wa kwanza anaweza kumuwahi wa pili katika kumpiga mweleka mwenziwe.

  Tunashukuru jaji mkuu kwa kuliweka wazi suala hili. Na bado tuna safari ndefu sana.
   
 7. Lutala

  Lutala JF-Expert Member

  #7
  Jun 22, 2010
  Joined: Jun 17, 2010
  Messages: 845
  Likes Received: 18
  Trophy Points: 35
  Bongo ni mkusanyiko wa matatizo tu. Yaani mahakama kuu ya Tanzania ni mali ya CCM kabisa. Kwanini mgombea binafsi anakataliwa bongo? wale jamaa wa CCM wanajua kuna vigogo kadhaa ndani yao wanataka kuwania kupitia nafasi hiyo. Mahakama Kuu kwa kuogopa lawama imeamua bunge liamua kuhusu hilo wakati wao ndo waliotakiwa kutoa hukumu. Mbona Babu Seya au Liyumba hawakupelekwa kuhukumiwa na Bunge? Shame on CJ and his mahakama Kuu
   
 8. Ringo Edmund

  Ringo Edmund JF-Expert Member

  #8
  Jun 22, 2010
  Joined: May 10, 2010
  Messages: 4,895
  Likes Received: 28
  Trophy Points: 0
  JAMANI NAOMBA MSAADA KWA WANAOLIELEWA VIZURI HILI JAMBO.TUME HURU TUMEKOSA,MGOMBEA BINAFSI TUMEPIGWA CHANGA LA MACHO,CCJ HAKUNA USAJILI,JE WAPINZANI WAKIGOMA KUSHIRIKI KWENYE UCHAGUZI NINI KITATOKEA?:dance:
   
 9. Mnyamahodzo

  Mnyamahodzo JF-Expert Member

  #9
  Jun 23, 2010
  Joined: May 23, 2008
  Messages: 1,854
  Likes Received: 220
  Trophy Points: 160
  Kirahisi nitakujibu hivi; wakigoma kushiriki kwenye uchaguzi CCM wataendelea na uchaguzi kwa kuwa kila kitu yaani kuanzia jeshi,polisi, UwT, tume ya uchaguzi, mahakama + vyombo vya habari wamekwisha vitia kwenye kapu lao, hivyo hakuna atakaye wapinga . Tume ya uchaguzi itatangaza matokeo, na Jaji mkuu atamwapisha Rais upesiupesi. Chokochoko na mikiki ya wanachi, wanaharakati na wanasiasa wa ndani na nje ikizidi basi SERIKALI ya MSETO hiyo. Kwa mlango wa mbele CCM wanakuwa tayari wameinfiltrate serikali mpya ya wana wa nchi hii.

  Anything else.........
   
 10. Mnyamahodzo

  Mnyamahodzo JF-Expert Member

  #10
  Jun 23, 2010
  Joined: May 23, 2008
  Messages: 1,854
  Likes Received: 220
  Trophy Points: 160
  Katika makala iliyoandikwa na Lula wa Ndali Mwananzela katika gazeti la Raia Mwema(juni23-30,2010) yenye kichwa MAKOSA YA HUKUMA YA MAHAKAMA YA RUFAA HAYA HAPA, amenena mambo mengi ya msingi. mimi nakuu hiki tu, "[COLOR] Katiba yetu ya Jamhuri ya Muungano inasema hivi: Mamlaka ya utoaji haki katika Jamhuri ya Muungano itakuwa mikononi mwa Idara ya Mahakama na Idara ya Mahakama ya Zanzibar, na kwahiyo hakuna chombo cha serikali wala cha Bunge au Baraza la wawakilishi la zanzibarkitakachokuwa na kauli ya mwisho katika utoaji haki(Ibara ya 107:1). Hii ina maana ya kwamba suala la haki haliwezi kuamuliwa na Bunge au na Baraza la Wawakilishi au na Ikulu!
  Unaporudisha suala la haki kwa Bunge unafanya kitu kinyume na Katiba kwani katiba inakataza kabisa kuweka suala la haki na kuachia Bunge au Baraza la wawakilishi kuwa na sauti ya mwisho[/COLOR]"

  Jaji Mkuu na timu yake ya majaji wakilitambua jukumu lao kuu ni kuitafsiri vizuri sheria ili haki itendeke (sielewi ni kwa kulewa madaraka au makusudi) wakaipindisha na kuvunja kipengere cha Katiba na matokeo yake Mhimili mzima wa Mahakama sasa unaonekana chaka a.k.a chokambaya.

  kam,a vile ambavyo watu hawataki kulisahau kosa alilolifanya Chifu Mangungo wa Msovero kwa kuingia mkataba wa kuiuza Tanganyika kwa kusaini mkataba na Karl Peters , ndivyo hivyo hivyo kosa la CJ et al litakavyokumbukwa katika historia ya Tanzania.
   
 11. mayenga

  mayenga JF-Expert Member

  #11
  Jul 8, 2015
  Joined: Sep 6, 2009
  Messages: 3,749
  Likes Received: 545
  Trophy Points: 280
  Hapo sasa
   
Loading...