Jaji Ramadhan aibua udhaifu mpya wa katiba katika kipengele cha Rais wa Zanzibar | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Jaji Ramadhan aibua udhaifu mpya wa katiba katika kipengele cha Rais wa Zanzibar

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by nngu007, Apr 13, 2011.

 1. nngu007

  nngu007 JF-Expert Member

  #1
  Apr 13, 2011
  Joined: Aug 2, 2010
  Messages: 15,871
  Likes Received: 58
  Trophy Points: 145
  Na Heri Shaaban

  JAJI Mkuu Mstaafu wa Tanzania, Augustino Ramadhan ameibua udhaifu mwingine kwenye katiba ya sasa katika kipengele cha Rais wa Zanzibar kuwa mjumbe wa Baraza la Mawaziri la Jamhuri ya Muungano, kuwa ipo siku kitazua utata mkubwa.

  Alisema kwa sasa inaonekana kama si tatizo kwa kuwa wote wanatoka chama kimoja, lakini ikiwa chama tofauti kitaingia madarakani upande wowote, itakuwa jambo la ajabu kwa Rais huyo kuingia kwenye baraza hilo.

  Jaji Ramadhani alitoa kauli hiyo jana jijini Dar es Salaam juzi katika mahojiano maalumu yaliyorushwa na Kituo cha Televisheni ya ITV wakati akielezea changamoto mbalimbali zinazokabili mahakama nchini.

  Alisema kuwa mapungufu katika katiba hiyo ni mengi, ingawa wananchi wengi hawaifahamu vyema katiba ya sasa.

  "Wananchi watoe maoni yao tuangalie itakavyokuwa, hakuna haja ya kuwepo malumbano na kuvuruga amani iliyopo nchini, na ndiyo maana serikali imeamua kuwashirikisha wananchi waweze kutoa maoni yao," alisema Jaji Ramadhan.

  Bw. Ramadhani alisema hata kwa upande wa majaji wa Mahakama Kuu katiba iliyopo inawabana katika umri kustaafu kuwa miaka 60, huku akihoji kwa nini isiwe 65 kama ilivyo kwa majaji wa Mahakama ya Rufaa.

  Hata hivyo, hakutaka kuingia kwa undani kuhumu muswada huo, hasa eneo la mgawanyo wa madaraka ya dola, mahakama na bunge, akisema anayo nafasi yake maalumu ya kutoa maoni, badala ya kuyatoa hadharani yakawavuruga wananchi.

  Kuhusu utendaji wa mahakama, alisema kuwa wananchi wasiisibebeshe lawama za kuchelewesha kesi, kwa kuwa suala la upelelezi linasimamiwa na Jeshi la Polisi si mahakama, na hakimu au jaji hulazimika kusikiliza pande zote wakati wa kusikiliza kesi.

  "Mfano wakili au mwendesha mashtaka akisema amefiwa. Jaji au hakimu hawezi kusema tuendelee hata kama umefiwa, maana ipo siku hata yeye anaweza kufiwa," alisema.

  Hata hivyo aliwataka wananchi wapatiwe elimu ya kutosha kwanza na si kubebesha lawama mahakama kwa kuwa kabla ya kufika mahakamani upelelezi unafanywa na polisi," alisema Ramadhani.
  Alisema kwa sasa hataki kushughulika na maswala ya siasa badala yake anashughulika na mahakama ya Afrika mashariki kwa kuwa taaluma yake ni mwanasheria.
   
 2. Kinyambiss

  Kinyambiss JF-Expert Member

  #2
  Apr 13, 2011
  Joined: Dec 2, 2007
  Messages: 1,372
  Likes Received: 5
  Trophy Points: 135
  Extremely good point from His Lordship.
   
 3. SMU

  SMU JF-Expert Member

  #3
  Apr 13, 2011
  Joined: Feb 14, 2008
  Messages: 7,932
  Likes Received: 2,080
  Trophy Points: 280
  Mimi nadhani issue sio tu kwa baraza la mawaziri bali pia muungano wenyewe kwa ujumla ulivyokaaa utaleta changamoto nyingi kama vyama tofauti (hasa kama ni vya mrengo tofauti) vitashika dola kwa Muungano na Zanzibar (bila ya shaka hii ilikuwa ni moja ya sababu ya ASP and TANU kuungana).
   
 4. Ngambo Ngali

  Ngambo Ngali JF-Expert Member

  #4
  Apr 13, 2011
  Joined: Apr 17, 2009
  Messages: 3,196
  Likes Received: 135
  Trophy Points: 160
  It is really sad kuwa anaona mapungufu hayo wakati akiwa nje, ni kwa nini hakuliona hilo wkati akiwa madarakani? Is it because he is not part of the status quo any more? Angekuwa serious angelifanyia kazi toka wakati huo badaka yake akakaa tu bila kufanya lolote pamoja na kuwa alikuwa na uwezo wa kufanya hivyo, kama ambavyo majaji wakuu wa jurisdiction nyingine wanavyofanya endapo suala nyeti la kikatiba linavyojitokeza.

  kuhusu wananchi kutoa maoni, wananchi walishatoa maoni kuwa wanataka haki ya kuwa na wagombea binafsi kupitia kesi aliyofungua mtikila lakini yeye akaizika bila huruma, wananchi wakatoa maoni kuhusu adhabu ya kifo kupitia kwa mbushuu akashupaa kuwa watu wanaoua lazima wanyongwe maoni gani zadi ya yale yanayokuja mbele yako wakati wewe unao uwezo wa kikatiba na kisheria kuusikiliza na bado kusikilizi maoni yao?

  Kuhusu umri wa kustaafu majaji hilo ni tatizo la status quo na hilo nadhani ndilo alilokusidia kusema vingine ni by the way tu.
   
Loading...