TANZIA Jaji Projest Rugazia afariki dunia. Kuzikwa Ijumaa Agosti 9, 2019 Kijiji cha Rwamashonga, Kata ya Mugana wilaya ya Missenyi

Kama hutojali unaweza kutupa wasifu wake au kesi yoyote yenye maslahi ya taifa aliyowahi kusimamia? Isije ikawa ni hawa majaji wanaotii amri toka juu.

Labda ya vigogo hawa kuhukumiwa kusafisha mazingira kwa kutumia fagio na kudeki vibaraza :
https://www.mwananchi.co.tz › ...
Mramba, Yona sasa kufagia hospitali Dar - Mwananchi

6 Feb 2016 · Mawaziri wawili wa zamani, Basil Mramba na Daniel Yona waliokuwa wakitumikia adhabu ya kifungo cha

... ilitoa hukumu ya rufaa dhidi ya mawaziri wastaafu, Basil Mramba na Daniel Yona ambapo Jaji Projest Rugazia, alikubaliana na hoja .

JAJI ASHANGAZWA NA SHERIA ZA TANZANIA

JAJI Projest Rugazia wa Mahakama Kuu Kanda ya Dar es Salaam, ameelezea kushangazwa na sheria za Tanzania, kwa kutoa adhabu ndogo kwa mawaziri wa zamani, Basil Mramba na Daniel Yona, ikilinganishwa na kiasi cha fedha walichosababisha hasara.

Jaji Rugazia alisema hayo wakati akiwapunguzia adhabu mawaziri hao kutoka kifungo cha miaka mitatu jela na faini ya Sh milioni tano hadi kifungo cha miaka miwili jela. “Nashangaa sheria zetu, mtu anaweza kusababisha hasara ya fedha nyingi, halafu anatoa faini ndogo na kuishia hapo...lakini nawaachia waheshimiwa wanaotunga sheria,” alisema wakati akifafanua adhabu zinazotakiwa kutolewa kutokana na kosa hilo.

Aidha, aliwafutia shitaka moja la kuisababisha Serikali hasara ya Sh bilioni 11.7 na adhabu iliyotolewa kutokana na kosa hilo. Hata hivyo, kosa hilo limeonekana katika mashitaka mengine.

Jaji Rugazia alitoa uamuzi huo jana baada ya kupitia na kuchambua hoja za pande zote katika rufaa mbili, zilizowasilishwa na mawaziri hao pamoja na Mkurugenzi wa Mashitaka (DPP).
Katika rufani hizo, Mramba ambaye alikuwa Waziri wa Fedha na Yona aliyekuwa Waziri wa Nishati na Madini, waliwasilisha hoja tano kupinga hukumu iliyotolewa Julai 6, mwaka huu katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu, na jopo la Mahakimu watatu, likiongozwa na John Utamwa.

Aidha DPP alipinga adhabu waliyopewa mawaziri hao kwa madai ni ndogo, hakimu alikosea kumuachia huru aliyekuwa Katibu Mkuu Wizara ya Fedha, Gray Mgonja na pia iliiomba mahakama iamuru washitakiwa walipe fidia ya fedha walizosababisha hasara.

Akisoma uamuzi huo jana, Jaji Rugazia alikubali hoja ya kina Mramba kuwa walipewa adhabu mbili kwa kosa moja. “Haikuwa sahihi kuwashitaki kwa kosa la kusababisha hasara wakati kosa hilo lilishakuwa kwenye makosa mengine ambayo ni la tano hadi la 10,” alisema.

Aidha, alisema Yona aliunganishwa kimakosa katika shitaka hilo, hivyo alifuta shitaka hilo pamoja na adhabu ya kifungo cha miaka mitatu jela na faini ya Sh milioni tano iliyotokana na kosa hilo. “Ninaondoa shitaka la kusababisha hasara, ninafuta adhabu ya kifungo cha miaka mitatu jela na faini ya Sh milioni tano, hivyo Yona na Mramba watatumikia kifungo cha miaka miwili kwa kila kosa,“ alisema.

Adhabu hizo ni Kifungu cha 96 (1) cha Kanuni ya Adhabu, ambapo adhabu yake ni kifungo kisichozidi miaka miwili jela, au Kifungu cha 284 (c) ambacho adhabu yake ni kifungo kisichopungua miaka mitatu jela au kulipa faini ya Sh milioni tano. Katika uamuzi huo, Jaji Rugazia alisema, “Nakubali Kifungu cha 6 cha Kanuni ya Adhabu kinachotaka mahakama itoe amri washitakiwa walipe fidia, lakini siwezi kutoa amri hiyo.”

Aidha, alikataa hoja za kina Mramba kuwa hati ya mashitaka ni batili, pia alisema hakukuwa na njama zozote kwa upande wa Jamhuri kutoita mashahidi waliosaini mkataba huo ili kuathiri upatikanaji wa haki, kwa kuwa utetezi walikuwa na haki ya kuomba watu hao wawe mashahidi wao.

Alisema wasitumie maelezo ya aliyekuwa Rais wa Awamu ya Tatu, Benjamin Mkapa, kuficha kosa kwa kuwa alitoa maelekezo kutokana na barua aliyoipata kutoka kwa Mramba na hakujua kama tayari Mamlaka ya Mapato nchini (TRA) ilishatoa angalizo la kutokutoa msamaha huo.

Kwa upande wa Mgonja, Jaji Rugazia alisema anahalalisha kuachiwa kwake huru baada ya kutopatikana na hatia. Alisema, “Siwezi kuilaumu mahakama kwa kumuachia huru”. Katika hukumu hiyo, mawaziri hao walihukumiwa kifungo cha miaka mitatu jela na kulipa faini ya Sh milioni tano, baada ya kupatikana na hatia ya matumizi mabaya ya madaraka na kuisababishia serikali hasara ya Sh bilioni 11.7.

Kwa mara ya kwanza washitakiwa hao walifikishwa mahakamani hapo mwaka 2008, wakikabiliwa na mashitaka ya kuisababishia serikali hasara ya kiasi hicho cha fedha kutokana na kutoa msamaha wa kodi kwa Kampuni ya kukagua madini ya dhahabu ya M/S Alex Stewart ya Uingereza.

MACHAPISHO NA HOPE J KABIRIGI.
 
Huyu marehemu Projest R.I.P ni mfano mzuri kwa watu kuiga kwani aliweza kujiendeleza kiellimu toka kuwa typist pale idara ya uchumi UDSM mpaka kufikia kuwa Jaji wa High court!
Nakumbuka kuwa katika kesi ya ufisadi dhidi ya Basil Pesambili Mramba a.k.a ( mzee wa kutulisha majani ili ndege ya Rais inunuliwe) yeye marehemu ndiye aliwapunguzia kifungo on appeal!!
 
[QUOTXE="Sesten Zakazaka, post: 32380050, member: 453386"]
He was a no nonsense Magistrate, though I keep forcing my brain to believe he was acting within the law atleast in two incidences when he was presiding over the cases of people I happened to know
[/QUOTE]
Alipoamua ama simamia kesi za watu uliokuwa unawafahamu basi alikuwa jaji mzuri mfuata sheria, ila alipoamua kesi dhidi ya watu ambao ni strangers kwako basi alikuwa jaji wa aina gani?

Yaani hiyo rekodi yako juu ya naamuzi ya jaji imekaa kishabiki mno.
 
Ficha upumbavu na ujinga hii ni JF kisima cha habari na maarifa lazima aulize hapa
Mkuu hiyo ndio ilikuwa JF ya zamani, kisima cha habari na maarifa. Siku hizi ni sehemu ya kupigia baragumu, kusifu na kuabudu. ( Praise and worship).

Tukirudi kwenye mada ni kweli Mheshimiwa Jaji Mstaafu wa mahakama Kuu ya Tanzania Projest Rugaziya, hatunaye, amefariki leo hapa Dar es salaam
 
Back
Top Bottom