Jaji Mwangesi abwaga Manyanga - Kesi dhidi ya Balozi Mahalu na wenzake

DoubleOSeven

JF-Expert Member
Jul 5, 2008
661
143
Habari za kuaminika ni kwamba Jaji Sivangilwa Mwangesi amejotoa leo hii kuendeshwa ile "kesi" baada ya kuombwa kufanya hivyo na utetezi. Mengine baadaye.



Mahalu amkataa Jaji - Tanzania Daima 26th, March 2011

na Happiness Katabazi




ALIYEKUWA balozi wa Tanzania nchini Italia, Profesa Costa Mahalu, na Grace Martin, wanaokabiliwa na kesi ya uhujumu uchumi wa zaidi ya euro milioni 2, jana walimwomba Jaji Sivangilwa Mwangesi ambaye anaendesha kesi hiyo ajitoe kwa sababu amekuwa akikiuka sheria kwa malengo anayoyajua yeye.

Ombi hilo lilitolewa jana na mawakili wa washtakiwa hao Mabere Marando aliyekuwa akisaidiwa na Beatus Malima na Alex Mgongolwa ambao walianza kwa kuikumbusha mahakama hiyo kuwa wanafahamu kuwa kesi hiyo ilikuja jana kwa ajili ya jaji huyo kupanga tarehe ya washtakiwa hao kuanza kujitetea.

Marando alidai kuwa wana sababu sita za kumuomba Jaji Mwangesi ajitoe. Sababu hizo ni kwanza kwamba upande wa utetezi ulishatoa mahakamani hapo Ansard ya Bunge ya mwaka 2004 iliyomnukuu aliyekuwa Waziri wa Mambo ya Nje katika serikali ya awamu ya tatu ambaye kwa sasa ni Rais Jakaya Kikwete akilieleza Bunge kuwa manunuzi ya jengo la ubalozi wa Tanzania nchini Italia ulikidhi matakwa ya sheria ya manunuzi ya umma na kwamba hakukuwa na wizi katika ununuzi huo lakini jaji huyo hakuzingatia ansard hiyo.

Sababu ya pili ni kwamba Mwangesi alivunja Sheria ya Ushahidi ya mwaka 2002 wakati akipokea ushahidi wa shahidi wa jamhuri kwa njia ya video na kwamba shahidi huyo ambaye ni wakili wa Italia alitoa ushahidi wake katika kesi hiyo inayoendeshwa hapa nchini akiwa nchini Italia, kitendo ambacho kinakiuka sheria hiyo ya ushahidi.

Sababu ya tatu ni kitendo cha Jaji Mwangezi kung’angania upande wa jamhuri umlete mlalamikaji wa kesi hiyo licha ya upande huo kumueleza kuwa kesi hiyo haina mlalamikaji, hatua ambayo Marando alisema imewanyima kuwasilisha ombi la kutaka kesi hiyo ifutwe kwa sababu ilikuwa haina mlalamikaji.

Sababu ya nne ni kwamba jaji huyo aliunyima haki upande wa utetezi wa kuwasilisha majumuisho ya kuwaona hawana kesi ya kujibu pale jaji huyo kwa malengo yake anayoyajua yeye siku jamhuri ilipofunga kesi yake na ndipo akatoa uamuzi wa kuwaona washtakiwa wana kesi ya kujibu.

“Sababu ya tano ya kukukataa jaji wewe ni kwamba wewe unasikiliza kesi hii kama hakimu wa mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu kwa sababu mahakama zote zina mipaka ya ardhi ya kufanya kazi zake isipokuwa Jaji Mkuu anaweza kutoa kibali maalum kwa mahakama husika kusikiliza kesi iliyo nje ya mamlaka yake … lakini wewe mheshimiwa jaji hukupata kibali cha Jaji Mkuu na ukadiriki kupokea ushahidi wa shahidi wa jamhuri aliyekuwa nchini Italia kwa njia ya video jambo ambalo tunaliona ulikiuka makusudi sheria za nchi kwa malengo yako binafsi,” alidai Marando.

Alitaja sababu ya sita kuwa jaji huyo alikiuka kwa makusudi sheria za Tanzania kwa kukubali kwake kupokea nakala kivuli ya mkataba wa mauzo ya ununuzi wa jengo la ubalozi wa Italia, jambo ambalo ni kinyume cha sheria za hapa nchini.

Jaji Mwangesi badala ya kusikiliza hoja hizo aliahirisha kesi hiyo hadi Jumatatu Machi 28 mwaka huu, ambapo atatoa uamuzi wa kujitoa au kutojitoa katika kesi hiyo.
 
.....maskini Babu Seya alikosa watetezi wazuri....labda huyu atashinda visasi vya mkulu!!!
 
mi nampenda sana mabere marando....yuko makini sana kwenye kutoa tetezi zake nyingi mahakamani....
 
.....maskini Babu Seya alikosa watetezi wazuri....labda huyu atashinda visasi vya mkulu!!!

... talking of visasi, the TRUTH will prevail.
Uchafu unaoibuka kila kona siku hizi ni mojawapo ya MATOKEO ya UPUUZI ulioarasimishwa 2005. Malipo hapa hapa!!
 
Back
Top Bottom