Bams
JF-Expert Member
- Oct 19, 2010
- 16,489
- 40,999
Hapo zamani, enzi za akina Jaji Nyalali, Augustino Ramadhani, Rugakingira, Jaji Warioba, ukisikia jaji anasema kitu, unakaa chini ili usikie anasema nini. Kama ni gazeti, lazima utanunua ili ujue anachokitamka jaji.
Ujaji ilikuwa ni nafasi ya heshima kubwa, ilikuwa inaonekana ni kazi takatifu, kwa sababu ilikuwa inaashiria uwezo wa hali ya juu, akili ya kiwango cha juu, maadili ya hali ya juu, na weledi wa masuala ya haki kwa kiwango cha hali ya juu.
Siku za karibuni, nafasi hii ya ujaji, si chochote wala si lolote. Wapo watu wa aina zote, wakiwemo wanafiki, waongo, wala rushwa, wapindisha haki na wapambe wa siasa na wanasiasa. Hakuna weledi wala maadili.
Namshangaa sana Mutungi, na kwa kweli mtu mwenye uweledi wa ujaji asingefanya kama alivyofanya katika kuunda aliyoiita Kamati ya kuyapitia mapendekezo ya namna ya kufanya shughuli za siasa pamoja na kupata Tume huru ya uchaguzi.
Jaji wa kweli angeanza na kanuni zitakazotumika kuwapata wajumbe wa hiyo kamati, na kanuni hizo zikubaliwe na wadau. Hakufanya hivyo. Sijui kama ni tatizo la weledi au dhamira mbaya.
Nchi hii anayelalamikiwa kuvuruga mfumo wa demokrasia, kuiba kura, kutangaza wagombea ambao hawakushinda, kuiba maboksi ya kura, kubambikia wagombea wa vyama vya upinzani kesi, kupora fomu za wagombea wa kutoka vya vya upinzani, kukataa kupokea fomu za wagombea, kukata majina ya wagombea kwa sababu za uwongo, ni CCM kwa kutumia Serikali ikizihusisha kwa karibu taasisi kama:
1) Tume ya uchaguzi
2) Wakurugenzi wa Wilaya na WEOs
3) Polisi
4) Wakuu wa Mikoa
5) Wakuu wa Wilaya
6) Usalama wa Taifa
7) Msajili wa vyama vya siasa
Leo eti unaunda Kamati ya kuangalia namna ya kupata Tume Huru ya Uchaguzi, kurudishamfumo wa kidemokradia wa kufanya shughuli za siasa, halafu wajumbe wa kufanya hayo, ni hao hao au kutoka kwenye taasisi hizo hizo chafu dhidi ya demokrasia.
Mutungi, nasita hata kukutaja Jaji, kanuni za haki na neutrality unazifahamu? Umefanya kwa kutokufahamu au una dhamira chafu ndani yako?
Kama utaratibu wenyewe wa kuipata Tume Huru ya Uchaguzi ndiyo huu wa kutumia watu wale wale waliokuwa wanaangamiza demokrasia, zoezi zima halima maana, ni upotezaji wa muda na fedha.
Ni tangu lini jambazi akaweka kanuni nzuri za kuzuia ujambazi?