Jaji Mutungi: Rais Magufuli hajafuta mikutano ya kisiasa

jingalao

JF-Expert Member
Oct 12, 2011
35,035
28,202
Msajili wa vyama vya siasa nchini Jaji mstaafu Francis Mutungi amewataka wanasiasa kutoitafisri vibaya hotuba ya Rais kwamba amepiga marufuku shuguli za kisiasa na badala yake watambue kuwa alichosema Rais ni kwamba amefungua milango ya mashirikiano na wanasiasa katika kuendeleza Taifa kwa kufanya kazi na siyo muda wote kuhubiri siasa

Amesema kuwa wanasiasa wasipotoshe wito wa Rais kisiasa kwa kudai kuwaRais amefuta harakati za siasa nchini.

amesema wito wa Rais ni kuwakaribisha wanasiasa katika maswala ya maendeleo na sio siasa zisizo na tija.

source:ITV
 
atatue kwanza issue ya sukari na ongezeko la tozo kwenye mitandao ya simu hasa ktk huduma zakifedha kwani hili ongezeko humuathiri mwananchi moja kwa moja na hili halihitaji mpaka wapinzani wakamshaur raisi
 
Nani huyo jaji Mutungi au?
 
Tumemsikia sote bila chenga Magu akieleza bayana kuwa wanasiasa wasubiri 2020 ndiyo warejee kwenye harakati za siasa.

Sasa yeye Jaji Mutungi anajaribu kuiedit hotuba ya Mkuu wa nchi kwa kuwa anajua kwa nafasi yake ya usajili wa vyama na kusimamia shughuli za vyama vya siasa, kwa Rais kutangaza kusitisha shughuli zote za siasa hadi baada ya miaka 5, ni kama vile Presidaa kamtangazia redundancy nafasi yake.....
 
Huyu mtungi anajua kiswahili au no???, JPM alitumia kiswahili ambacho ni highly transparent na hakihitaji kufafanuliwa na mtu yeyote yule.Msajiri hata asijisumbue kutetea au kuchengesha yaliyo dhahiri.
 
Tumemsikia sote bila chenga Magu akieleza bayana kuwa wanasiasa wasubiri 2020 ndiyo warejee kwenye harakati za siasa.

Sasa yeye Jaji Mutungi anajaribu kuiedit hotuba ya Mkuu wa nchi kwa kuwa anajua kwa nafasi yake ya usajili wa vyama na kusimamia shughuli za vyama vya siasa, kwa Rais kutangaza kusitisha shughuli zote za siasa hadi baada ya miaka 5, ni kama vile Presidaa kamtangazia redundancy nafasi yake.....
Ndio huu upotoshaji alioukataa mkuu...tupime uelewa wa viongozi wa Ukawa
 
Jaji Mutungi alikaa kimya wakati Polisi wanawatembezea wapinzani virungu na kuwamwagia maji ya kuwasha akijua wazi kuwa huo ni uvunjaji wa wazi kabisa wa Katiba ya nchi, lakini kwa kuwa na yeye ni 'kada' aliamua kuwa bubu.....

Lakini baada ya jana Rais kutangaza kusitisha shughuli zote za kisiasa kwa kipindi cha miaka 5 na kuona kuwa kibarua chake kipo hatarini ndiyo anakurupuka na kukanusha maelezo ya Rais kama vile yeye ndiye Kurugenzi ya habari ya Magogoni...
 
Hivi mbona awamu hii hata watu waliokuwa wanafikiri vizuri hapo kabla sasa wanaonekana kana kwamba akili zao wameziacha awamu iliyopita na kuingia awamu nyingine wakiwa watupu kichwani? !
Kama magufuri na serikalini yake hawataki mfumo wa siasa uliopo si wapeleke mswaada bungeni kuufuta na kubaki na chama chao? Wako wengi bungeni hivyo watakacho kupitia bunge watakipata.
 
6 Reactions
Reply
Back
Top Bottom