Jaji Mutungi ni Mlezi wa CCM au Vyama vyote vya Siasa? Maana kwenye Mikutano Mikuu ya Wapinzani haonekani

johnthebaptist

JF-Expert Member
May 27, 2014
82,754
139,561
Nauliza tu kwa nia njema kwa sababu malezi yana maana pana.

Mara ya mwisho nilimuona msajili wa Vyama vya Siasa Jaji Mutungi kwenye mkutano mkuu wa CCM.

Baada ya hapo amekuwa akiwakilishwa na msaidizi wake mh Nyahoza katika Mikutano yote ya Vyama vya Upinzani iliyofuatia huku akitoa udhuru kuwa msajili ana majukumu " muhimu"

Hali hii sikuwahi kuiona kwa msajili mstaafu Jaji Tendwa ndio maana nauliza labda kanuni na taratibu zimebadilika.

Kuna uzito wa pekee pale msajili " mwenyewe' anapohudhuria mikutano hii na kutoa nasaha kama mzazi badala ya kumtuma baba mdogo.

2020 Hakunaga kama Dkt. Magufuli!
 
Mimi huwa sometimes nashindwa kuelewa. Hivi inakuweje mtu ni Jaji tena mstaafu lakini bado muoga na anapokea maelekezo toka juu .... Only in Tanzania.
 
Jambo moja nina hakika nalo ni kuwa Mutungi hajawahi kufanya kazi kiuweledi wala busara. Uzoefu wangu wa kuwa naye karibu Dodoma miaka hiyoo,unaonyesha hana uwezo wa chochote kinachohitaji werevu, weledi, akili na busara.
 
Kwanza huyo ni kama mlevi afadhali aendelee kutokuonekana! Kazi yake kubwa kubabikizia makosa vyama vya upinzani!
 
Huwa anamtuma naibu...si lazima yeye!! Cha msingi office ifike mkutanoni.

Sema tu namuonea huruma maana dhamana ya amani ya nchi kwa sasa ipo mikononi mwake!!
 
1 Reactions
Reply
Back
Top Bottom