Jaji Mutungi Amwambia DC Aliyetaka Taarifa za Mahakama Huu Mchezo Hauitaji Hasira

OFISI ya Mkuu wa Wilaya ya Mwanga inadaiwa kumwandikia barua Hakimu Mfawidhi wa Wilaya ya Mwanga kutaka taarifa mbalimbali za kesi zinazoendeshwa mahakamani kila mwezi.

Inadaiwa ofisi hiyo iliandika barua yenye kumbukumbu namba CAB40/229/01/25 ya Julai 8 mwaka huu kwenda kwa Hakimu Mfawidhi wa Wilaya.

Hatu hiyo ya mkuu wa wilaya imekuja wiki mbili baada ya Katibu Mtendaji wa Sekretarieti ya Maadili ya Viongozi wa Umma, Jaji Salome Kaganda kuwatahadhalisha wakuu wa wilaya nchini wawe makini katika utendaji wao ili wasije wakaingilia mihimili mingine.

Jaji Kaganda aliyasema hayo wakati wakuu hao wa wiala walipokula kiapo cha utumishi, Ikulu Dar es Salaam hivi karibuni.

Alisema anao uzoefu na amekuwa akipokea malalamiko mengi yanayohusu manyanyaso na uvunjifu wa maadili unaowahusu wakuu wa wilaya.

Jaji Kaganda pia alikemea ulevi kupita kiasi, matumizi mabaya ya madaraka na tatizo la viongozi wa umma kutumia vibaya madaraka yao kwa kuingilia mihimili mingine.

Barua hiyo ilitaka taarifa mbalimbali za mahakama zikiwamo idadi ya kesi zilizopo, zilizosikilizwa na changamoto zilizojitokeza zikiwamo za sheria, fedha na vitendea kazi.

Taarifa nyingine ni kiasi cha fedha za mashahidi zilizopokelewa na zilichotumika kuwalipa kwa mwezi husika ikibainisha majina na fedha.

Kwa sababu hiyo, MTANZANIA lilimtafuta aliyewahi kuwa Msajili wa Mahakama Kuu, Jaji Francis Mutungi ambaye ni Msajili wa Vyama vya Siasa kwa sasa kujua utaratibu wa mahakama wa kutoa taarifa zake za uendeshaji wa kesi.

“Kuna kitu kinaitwa taarifa ya marejesho…kila mahakama ina utaratibu wake, taarifa zinakusanywa na kupelekwa Mahakama Kuu Kanda.

“Mahakama Kuu Kanda inakusanya taarifa za mahakama zote na kuziwasilisha Makao Makuu ambayo ni Mahakama Kuu ya Tanzania, Dar es Salaam.

“Kazi hizi hazihitaji hasira, inawezekana huu ni utaratibu wake yeye huyo Mkuu wa Wilaya…wanatakiwa kuelimishwa kazi za utawala zinaendaje.

“Kwa mazingira hayo hakimu anaweza kujibu ovyo kwa sababu hawajibiki kwa DC.

“DC naye anataka kujua taarifa za wilaya yake kwa sababu ofisi yake inapokea malalamiko mbalimbali yakiwamo ya kesi…kufanya hivyo anakuwa na nia njema tu.

“Lakini ni kosa kuandika moja kwa moja kwa Hakimu Mfawidhi, hakimu naye ni kosa kujibu ovyo.

“DC alitakiwa kuandika barua kwa msajili akiomba hizo taarifa na msajili naye ataziomba makao makuu,”alisema.

Alisema mihimili wa mahakama na utawala haitakiwi kuingiliana bali inatakiwa kuwasiliana.

“Ofisi ya Mkuu wa Wilaya ilitakiwa kupeleka taarifa hizo kwa Msajili ikijieleza kwamba katika wilaya hiyo wamejiwekea utaratibu wa kupata taarifa za mahakama kupunguza malalamiko kutoka kwa wananchi, hilo linaweza kufanyika kwa nia njema tu,”alisema Jaji Mutungi.

Pamoja na hayo, MTANZANIA lilimtafuta kwa simu Mkuu wa Wilaya ya Mwanga, Aaron Mmbago ili atoe ufafanuzi wa barua hiyo.

Katika majibu yake kwa simu Mmbago alisema: “Nipe hiyo barua niione ndipo nitaweza kusema. Kwa simu siwezi kusema ….nitumie nakala ya hiyo barua inayosema haya kwani kuna ugumu gani?”alihoji Mmbago.

Alipotakiwa afafanue kama ofisi yake imeanzisha utaratibu huo wa kumtaka Hakimu Mfawidhi kumpa taarifa za mahakama wilayani kwake, aliendelea kujibu kwamba mpaka aione hiyo barua inayodaiwa kutoka ofisini kwake ndipo ataweza kuizungumzia.

Barua hiyo iliyotoka Ofisi ya Mkuu wa Wilaya ina kichwa cha habari kisemacho, Taarifa za uendeshaji wa shughuli za mahakama ya wilaya na mahakama za mwanzo katika Wilaya ya Mwanga kwa kila mwezi’.

Pamoja na mambo mengine barua hiyo inasema: “Mahakama wakati mwingine inakutana na vikwazo ambavyo wananchi wa kawaida hawawezi kuelewa kwa kuzingatia kuwa ni masuala ya sheria.

“Wakati mwingine ni masuala ya fedha au vitendea kazi, hali hiyo huleta maswali mengi na malalamiko pasipo wao kujua.

“Kutokana na hoja hizo, ofisi ya mkuu wa wilaya inahitaji taarifa za kila mahakama iliyopo na taarifa hizo zibainishe jina la mahakama, jumla ya kesi zilizopo, jumla ya idadi ya kesi zilizosikilizwa na changamoto zilizojitokeza zikiwamo za sheria, fedha na vitendea kazi.

“Taarifa nyingine ni kiasi cha fedha za mashahidi zilizopokelewa kwa mwezi husika na kiasi cha fedha kilichotumika kuwalipa mashahidi kwa mwezi husika kwa kubainisha majina na fedha”.

Chanzo:MTANZANIA
Akina makonda wako wengi
 
Kuna Mkuu mmoja wa Wilaya ya kinondoni alizivamia kesi za ardhi ambazo baadhi zilikuwa mahakamani, bahati mbaya akiongea na mmoja anampa haki bila kujua mwenzake alishashinda muda mreeefu mahakamani tena wakiwa na aliyekwenda kwa Mkuu wa wilaya,Mkuu yule wa Wilaya alimalizia hasira kwa maafisa ardhi wa halmashauri kwa kuwaweka ndani.
Makonda
 
Ndugu yangu, si umeambiwa 'mchezo huu hauhitaji hasira'??? punguza hasira ndugu yangu...
Ndg nitapunguza hasira lakini nchi inaharibika maana kila mtu anafanya lile analooma linafaa machoni pake utadhani hatuna miongoza na inafika mahali unaweza hata kukufuru kwa Mungu kwamba kwanini nilizaliwa ktkt taifa la watu wa hovyo kiasi hiki
 
DC ni Mwenyekiti wa baraza la mahakama ya wilaya km mwenyekiti anapaswa kuelewa kinachoendelea wilayani huyo hakimu km alimjibu ovyo dc anapaswa kuwajibishwa. Lkn barua hiyo haina makosa vitu alivyotaka dc ni vya kawaida mahakama haikusanyi kodi kwahiyo dc kutaka kujua changamoto ya pesa ktk mahskama yake kuna kosa gani na je barua hiyo imefikaje kwa waandishi wa habari?
 
Ipo siku wataamuru hata ikulu ipeleke ripoti juu ya utendaji wake, kisa ipo kwenye wilaya ya huyo dc....!
 
kwani dc kaingilia maamuzi ya mahakama au kaomba taarifa kama kiongozi wa wilaya husika. tuwe makini kwenye hili.
 
Sioni tatizo lolote kwa mkuu wa wilaya kuomba taarifa, nadhani hakimu mfawidhi alikuwa na nafasi nzuri ya kumjibu DC kwa kumpa utaratibu sahihi wa kufuatwa kama alivyofafanua jaji.

Tatizo kunapokosekana busara huwa full kutunishiana misuri na kudhalilishana, ikiwa barua ile ni mawasiliano ya siri na ya ndani! Kulikuwa na haja gani Hakimu Mfawidhi kuitoa hadharani, bado namuona DC Aaron ni mtu anaejitambua kwa kukataa kumjibu mwandishi mpaka aonyeshe Ushahidi wa barua ile, isije ikawa ni mjinga fulani aliinyofoa toka ofisi ya masjala ya HM na kuirusha kwa mwandishi

Hivyo majibu yake uenda yangezalisha negative perception kwa HM na jamii kwa ujumla.

DC bado ukiangalia alikuwa na nia njema ya kuwasaidia watu wa wilaya yake na hakimu akiwemo. Watu tunashadidia utadhani hatufanyi kazi na wala huwa hatuandiki barua kutaka taarifa fulani ni full kunanga tu. Pathetic
 
Alipoona JPM amekurupuka KUULIZIA idadi ya kesi akajua na yeye anatakiwa kuwatumbua mahakimu!! Hajui kuwa mfalme juha nae alichemka na mwendo kasi wake?? Ndio ma DC wa mwendo kasi hao!!!
 
Hakuna watu ninaowachukia kama MADC na RC wote wanakula mishahara ya bure
Ni afadhali wewe kidogo utakuwa unawapenda yaani mm naona hawa ndo chanzo cha kuleta umasikini nchini mf.madc wote Tz ni 250 na kila mmoja anpata mshahara wa 2 500 000 jumlisha na magari yenye thamani ya Tsh.150 000 000 kwa kila gari
 
Duh! Yaleyale ya mwendo wa vruuuuuuum! Kuna haja ya hawa jamaa kupewa vitabu vya kufanyia rejea kama siyo moduli zinazoelekeza kazi zao. Job description ni muhimu kwa nafasi yoyote ya utendaji wa umma. Ni wakati sasa wa ofisi ya waziri mkuu kuendesha semina kwa wakuu wa wilaya.
Job description wanapewa,
 
Hawa madc wa ukada wana tabu sana. Wanafosi kiki..
06f8303101090314ad2ed613efe44cf4.jpg
 
Back
Top Bottom