Jaji Mustapha Siyani ataanza upya kusikiliza mapingamizi yaliyomfanya Jaji Elinaza kujitoa au anaendeleaje na kesi?

Upande wa mlalamikaji ulieleza mahakama kwa ushahidi na facts kwamba mashtaka yaliyowasilishwa na Jamuhuri hayapo au hayana nguvu na msingi wa kisheria. Jaji alinaza baada ya kusikiliza pande zote mbili alikubali kuwa hati ya mashtaka ina makosa lakini pamoja na kubaini makosa kwenye hati ya mashtaka hakutaka kuifuta kesi. Kitendo Cha kukubali kwamba mashtaka yamekosewa lakini hapohapo akaielekeza Jamhuri ikaandae mashtaka upya kilileta picha kwamba yeye Jaji anajua mashtaka sahihi ya mtuhumiwa kitu ambacho nikinyume kabisa na sheria. Jaji apaswi kuelekeza jamhuri ikatafute makosa maana kama Jamhuri ingelikuwa na makosa sahihi walipoletewa pingamizi walipaswa kukubali kwamba hati ina mapungufu na waje na chaji nyingine. Kama katika kipindi chote Cha uendeshaji mashtaka Jamhuri haikuwahi kuomba ikabadilishe hati ya mashtaka, jaji Elinaza aliielekeza Jamhuri ikarekebishe vipi hati ya mashtaka? Mazingira haya ya Jaji kujielekeza kutoa maamuzi ya hoja kinyume na utaratibu ndiyo yaliyopelekea Mtuhumiwa Mbowe kumwomba ajiondoe.

Je, jaji mpya anakuja kutolea maamuzi hoja za ubovu wa hati ya mashtaka au anakuja kufanya kazi gani? Kama anakuja kuendelea na ushauri wa jaji aliyepita kwa Jamhuri nini nafasi ya Malalamiko ya Mbowe kuhusu maamuzi mabovu yaliyotolewa na Jaji Elinaza?

Ni sahihi kwa mahakama kuelekeza Jamhuri namna yakuandaa mashtaka? Endapo Jamhuri itaelekezwa na Mahakama namna yakurekebisha hati ya mashtaka, je jaji atakapofika hatua ya kutoa hukumu atapingana na ushauri alioutoa? Maana kitendo Cha jaji kuielekeza Jamhuru ikarekebishe hati ya mashtaka kinaashiria kwamba mahakama tayari inayajua makosa ya mtuhumiwa na imeshajiridhisha kuwa makosa yalitendwa ila tu Jamhuri ilikosea kuyaandaa mashtaka hayo........kwa ukakasi huu tutegemee mahakama kutoa Haki wakati imejipa kazi yakushauri mashtaka yaweje?
Uko sahihi kabisa rejea kesi ya kina Zombe Jaji Salum Masati akitoa hukumu alisema siyo kazi yake kuwafundisha Jamhuri namna ya kushtaki na aliwaachia huru na kuwaambia wamefanya uzembe wenyewe kwa kung'ang'ania shtaka ambalo linahitaji ushahidi mzito kuishawishi mahakama.
 
Mkuu 'Beatrice', hiyo aya uliyoandika hapo ni ngumu sana.

Na pia itakuwa ngumu sana kwa huyu Jaji mpya kuendelea kusikiliza kesi ambayo mtangulizi wake tayari amekwishaona kwamba hati ya mashtaka ina makosa. Ataendelea vipi kusikiliza kesi ambayo tayari hati yake ya mashtaka imekosewa?

Au wewe una maana ya kwamba Jaji mpya hatalazimika kuona hayo mwenzake aliyoyaona?

Kwa hiyo akina Kibatala na wao wataanza upya kabisa, kuleta lile pingamizi lao la mwanzo kuhusu uwezo wa mahakama hiyo kuisikiliza kesi hiyo?

Mbona huu utakuwa mzunguko wa ajabu sana!
Ili haki itendeke (au ionekane kwamba inatendeka), ingekuwa vizuri kwa Jaji mpya kuanzia kwanzoni ili ajiridhishe kwamba Mahakama yake inao uwezo wa kusikiliza na kuhukumu kesi ya ugaidi au la ukizingatia kwamba lengo la mwendazake lilikuwa ni kuanzisha mahakama maalum ya mafisadi na wahujumu uchumi sasa hatujui kama na kipengele cha ugaidi kiliingizwa kwenye muundo wake. Kimsingi majaji wote wa hiyo mahakama wakae ili watoe hukumu jumuishi juu ya uwezo wa mahakama yao au vinginevyo mahakama kuu ingetoa maamuzi kama ingehusishwa.
 
Jaji mpya anaendelea kesi ilipoishia, Jamhuri wataleta mashtaka mapya kama yana kasoro Kibatala ataweka pingamizi tena, na hata akishinda hilo pingamizi itaishia Jamhuri kufanya marekebisho tu, hakuna kesi itakayo ondolewa kwa minor mistakes za charge sheet.
Kwa hiyo mradi tu ashtakiwe hata kama kesi ni ya kubumba ?!. Wafuasi wa watawala mnavunja mioyo sana kwa fikra zenu na roho mbaya mliojivika
 
Sijui una maana gani na "minor mistakes" kwenye kesi nzito kama hii ya ughaidi!

"minor mistakes"? ya kuweka vituo kwenye sentensi, au kuosea jia la mtuhumiwa? au ni zipi hizo unazozifikiria wewe?

Kwamba Jamhuri walisahau kutaja vituo vya mafuta vilivyokuwa vimepangwa kulipuliwa?

Kwamba mshtakiwa wa nne ilitakiwa kiasi cha pesa kilichotolewa kiwe zaidi ya hicho kinachodaiwa alitoa?

Kwamba mikutano iliyofanywa na washtakiwa sehemu mbalimbali wakipanga njama za ughaidi inapaswa ieleze kiubagaubaga yaliyozungumzwa kati yao?

Jamhuri ikirekebisha haya, bado utaona ni "monor mistakes"? Ilikuwaje wakasahau kuyanyoosha maelezo awali, hadi walelekezwe ndiyo ionekane kuna kesi nzito!

Unamwambia mtu aliyeko jela na ambaye hatma ya kesi hata kama ni ya kubambikiza hukumu ya maisha yake jela itakuwa miaka kadhaa, halafu umwambie marekebisho ni "minor mistakes"? HAKI hapo iko wapi?
Sahihi kabisa mkuu
 
Uko sahihi kabisa rejea kesi ya kina Zombe Jaji Salum Masati akitoa hukumu alisema siyo kazi yake kuwafundisha Jamhuri namna ya kushtaki na aliwaachia huru na kuwaambia wamefanya uzembe wenyewe kwa kung'ang'ania shtaka ambalo linahitaji ushahidi mzito kuishawishi mahakama.
Ilikuwa utawa wa JK mahakama zilikuwa huru siyo wa huyu dikteta
 
Sijui una maana gani na "minor mistakes" kwenye kesi nzito kama hii ya ughaidi!

"minor mistakes"? ya kuweka vituo kwenye sentensi, au kuosea jia la mtuhumiwa? au ni zipi hizo unazozifikiria wewe?

Kwamba Jamhuri walisahau kutaja vituo vya mafuta vilivyokuwa vimepangwa kulipuliwa?

Kwamba mshtakiwa wa nne ilitakiwa kiasi cha pesa kilichotolewa kiwe zaidi ya hicho kinachodaiwa alitoa?

Kwamba mikutano iliyofanywa na washtakiwa sehemu mbalimbali wakipanga njama za ughaidi inapaswa ieleze kiubagaubaga yaliyozungumzwa kati yao?

Jamhuri ikirekebisha haya, bado utaona ni "monor mistakes"? Ilikuwaje wakasahau kuyanyoosha maelezo awali, hadi walelekezwe ndiyo ionekane kuna kesi nzito!

Unamwambia mtu aliyeko jela na ambaye hatma ya kesi hata kama ni ya kubambikiza hukumu ya maisha yake jela itakuwa miaka kadhaa, halafu umwambie marekebisho ni "minor mistakes"? HAKI hapo iko wapi?
Achana na huyo mjinga.
 
Usidanganye wala kufikiri majaji wanaendesha kesi kwa mujibu wa fraternity kama wana CCM wanavyoteteana au kama ma lecturer wa UDSM wanavyotetea ujinga humu JF ili wapewe teuzi na kama walisoma FOE wapewe tender.

Ungekuwa umesoma masomo mliyoyaita ya "ungwini" akili yako ingetambua kuwa High Court na Court of Appeal kuna dissenting decision nyingi tu za jaji kukataa maamuzi ya wenzake.

Ukiachilia mbali dissenting judgment kuna Review ambazo jaji anaweza kugeuza maamuzi yake.

Hii yote ni kwa sababu jaji anafanya kazi kwa mujibu wa sheria na siyo fraternity iliyokunata kichwani mwako.

Ni vigumu sana kumkataa Jaji kwenye kesi yako, halafu ukategemea kuwa huyo jaji mwingine atakayeichukua atakuwa tofauti sana na uliyemkataa; wana fraternity yao.
 
Wakati fatma karume akiwa wakili akueambie kuwa alimkataa hakimu Mingi ni nini kilichofuatia kwa mahakimu wengine waliochukua kesi yake akiwemo Mahai, Lyamuya na wengine waliiendesha vipi. Wakaili nzuri huwa hashambulii credibility ya mahakimu, hilo hufanywa na mawakili wa harakati tu ambao kwa kiasi kikubwa interests zao kubwa ni kumtangaza mteja kwenye umma badala ya kumnasua mteja kutoka kwenye kibano cha sheria.
Jaji au Hakimu ni muamuzi wa mchezo hayuko hapo kwaajili yakuamua upande mmoja na maamuzi yanatokana na Hoja zinazowasilishwa na pande zote Mbili uliona wapi muamuzi anatoa maelekezo ya namna yakufungua kesi

Sent from my CPH2179 using JamiiForums mobile app
 
Usidanganye wala kufikiri majaji wanaendesha kesi kwa mujibu wa fraternity kama wana CCM wanavyoteteana au kama ma lecturer wa UDSM wanavyotetea ujinga humu JF ili wapewe teuzi na kama walisoma FOE wapewe tender.

Ungekuwa umesoma masomo mliyoyaita ya "ungwini" akili yako ingetambua kuwa High Court na Court of Appeal kuna dissenting decision nyingi tu za jaji kukataa maamuzi ya wenzake.

Ukiachilia mbali dissenting judgment kuna Review ambazo jaji anaweza kugeuza maamuzi yake.

Hii yote ni kwa sababu jaji anafanya kazi kwa mujibu wa sheria na siyo fraternity iliyokunata kichwani mwako.
Jaji au Hakimu ni muamuzi wa mchezo hayuko hapo kwaajili yakuamua upande mmoja na maamuzi yanatokana na Hoja zinazowasilishwa na pande zote Mbili uliona wapi muamuzi anatoa maelekezo ya namna yakufungua kesi

Sent from my CPH2179 using JamiiForums mobile app

Ni kwa kutokana na kuwa wanategemewa kuwa objective, ndiyo maana hawapendi kuletewa mambo ya kiharakati ya kupinga kuwa hatuna confidence na hakimu au juji fulani bila kuwa na sababu yoyote ya maana bali kwa kuhuisi tu.

Jiulie, kwani kesi iliyokuwa inatetewa na fatma karume kiharakati niliyoweka hapo iliishia wapi
 
Sijui una maana gani na "minor mistakes" kwenye kesi nzito kama hii ya ughaidi!

"minor mistakes"? ya kuweka vituo kwenye sentensi, au kuosea jia la mtuhumiwa? au ni zipi hizo unazozifikiria wewe?

Kwamba Jamhuri walisahau kutaja vituo vya mafuta vilivyokuwa vimepangwa kulipuliwa?

Kwamba mshtakiwa wa nne ilitakiwa kiasi cha pesa kilichotolewa kiwe zaidi ya hicho kinachodaiwa alitoa?

Kwamba mikutano iliyofanywa na washtakiwa sehemu mbalimbali wakipanga njama za ughaidi inapaswa ieleze kiubagaubaga yaliyozungumzwa kati yao?

Jamhuri ikirekebisha haya, bado utaona ni "monor mistakes"? Ilikuwaje wakasahau kuyanyoosha maelezo awali, hadi walelekezwe ndiyo ionekane kuna kesi nzito!

Unamwambia mtu aliyeko jela na ambaye hatma ya kesi hata kama ni ya kubambikiza hukumu ya maisha yake jela itakuwa miaka kadhaa, halafu umwambie marekebisho ni "minor mistakes"? HAKI hapo iko wapi?
Mkuu unawezaje kuuliza jitu jinga kama hilo maswali yote hayo?! Kama akijibu itakuwa upupu mwingi mwingine tu!!
 
Upande wa mlalamikaji ulieleza mahakama kwa ushahidi na facts kwamba mashtaka yaliyowasilishwa na Jamuhuri hayapo au hayana nguvu na msingi wa kisheria. Jaji alinaza baada ya kusikiliza pande zote mbili alikubali kuwa hati ya mashtaka ina makosa lakini pamoja na kubaini makosa kwenye hati ya mashtaka hakutaka kuifuta kesi. Kitendo Cha kukubali kwamba mashtaka yamekosewa lakini hapohapo akaielekeza Jamhuri ikaandae mashtaka upya kilileta picha kwamba yeye Jaji anajua mashtaka sahihi ya mtuhumiwa kitu ambacho nikinyume kabisa na sheria. Jaji apaswi kuelekeza jamhuri ikatafute makosa maana kama Jamhuri ingelikuwa na makosa sahihi walipoletewa pingamizi walipaswa kukubali kwamba hati ina mapungufu na waje na chaji nyingine. Kama katika kipindi chote Cha uendeshaji mashtaka Jamhuri haikuwahi kuomba ikabadilishe hati ya mashtaka, jaji Elinaza aliielekeza Jamhuri ikarekebishe vipi hati ya mashtaka? Mazingira haya ya Jaji kujielekeza kutoa maamuzi ya hoja kinyume na utaratibu ndiyo yaliyopelekea Mtuhumiwa Mbowe kumwomba ajiondoe.

Je, jaji mpya anakuja kutolea maamuzi hoja za ubovu wa hati ya mashtaka au anakuja kufanya kazi gani? Kama anakuja kuendelea na ushauri wa jaji aliyepita kwa Jamhuri nini nafasi ya Malalamiko ya Mbowe kuhusu maamuzi mabovu yaliyotolewa na Jaji Elinaza?

Ni sahihi kwa mahakama kuelekeza Jamhuri namna yakuandaa mashtaka? Endapo Jamhuri itaelekezwa na Mahakama namna yakurekebisha hati ya mashtaka, je jaji atakapofika hatua ya kutoa hukumu atapingana na ushauri alioutoa? Maana kitendo Cha jaji kuielekeza Jamhuru ikarekebishe hati ya mashtaka kinaashiria kwamba mahakama tayari inayajua makosa ya mtuhumiwa na imeshajiridhisha kuwa makosa yalitendwa ila tu Jamhuri ilikosea kuyaandaa mashtaka hayo........kwa ukakasi huu tutegemee mahakama kutoa Haki wakati imejipa kazi yakushauri mashtaka yaweje?
Mbwa hata awe mkali vipi haumi mkia wake
 
Unarudi kwenye mawazo yaleyale. Hakuna kesi duniani inaamriwa kiharakati. Kesi zinaamriwa kwa mujibu wa sheria.

Ni kama mambo uliyoyasoma ya engineering hayaamuliwi kama uanaharakati wa kuongoza migomo ya FOE bali kwa sheria kama Newton's law, Avogadro's law, Archimedes Principle nk.

Ni kwa kutokana na kuwa wanategemewa kuwa objective, ndiyo maana hawapendi kuletewa mambo ya kiharakati ya kupinga kuwa hatuna confidence na hakimu au juji fulani bila kuwa na sababu yoyote ya maana bali kwa kuhuisi tu.

Jiulie, kwani kesi iliyokuwa inatetewa na fatma karume kiharakati niliyoweka hapo iliishia wapi
 
Unarudi kwenye mawazo yaleyale. Hakuna kesi duniani inaamriwa kiharakati. Kesi zinaamriwa kwa mujibu wa sheria.

Ni kama mambo uliyoyasoma ya engineering hayaamuliwi kama uanaharakati wa kuongoza migomo ya FOE bali kwa sheria kama Newton's law, Avogadro's law, Archimedes Principle nk.
Ndiyo maana ni makosa kujitetea kesi mahakamani kiuharakati kwani bado itaamriwa kisheria, siyo kiuharakati.
 
Kesi hii imepoteza uhalisia wake. Kitakachofuata ni Mbowe kufutiwa kesi.
 
Jaji mpya anaendelea kesi ilipoishia, Jamhuri wataleta mashtaka mapya kama yana kasoro Kibatala ataweka pingamizi tena, na hata akishinda hilo pingamizi itaishia Jamhuri kufanya marekebisho tu, hakuna kesi itakayo ondolewa kwa minor mistakes za charge sheet.
Kisheria,minor mistakes ni nini?
Akili ndogo sana hizi.
 
Ni kwa kutokana na kuwa wanategemewa kuwa objective, ndiyo maana hawapendi kuletewa mambo ya kiharakati ya kupinga kuwa hatuna confidence na hakimu au juji fulani bila kuwa na sababu yoyote ya maana bali kwa kuhuisi tu.

Jiulie, kwani kesi iliyokuwa inatetewa na fatma karume kiharakati niliyoweka hapo iliishia wapi
Unataka kuniambia mawakili wa Utetezi hawakuw na Hoja?

Sent from my CPH2179 using JamiiForums mobile app
 
Unataka kuniambia mawakili wa Utetezi hawakuw na Hoja?

Sent from my CPH2179 using JamiiForums mobile app
Wanasheria wana kitu wanaita technicalities kwenye paperwork za kesi; wanasheria wasiokuwa na nguvu hupenda kuiambia mahakama ifute kesi kwa sababu ya makosa ya technicalities. Lakini sijawahi kuona mtuhumiwa anaachiwa huru kwa sababu aliyemfikisha mahakamani alifanya makosa ya technicalities, na hivyo kufanya shauri lote lisisikikilizwe na mhakama. kazi ya mahakama ni kutafuta ukweli wa shauri lote, huwa haitafuti technicalities katika presentation ya shauri hilo.

Miaka ya hivi karibuni utetezi mkubwa wa Kibatala umekuwa ni kwenye technicalities tu, siyo kwenye facts za kesi. Ningependa nimwone Kibatala anavyofanya cross examination kwani ndiyo njia pekee ya kiufundi ambayo wanasheria hutumia kupata ukweli wa shauri la kesi, siyo technicality kwenye paperwork
 
Back
Top Bottom