Jaji Mstaafu Stephen Ihema - macho ya Watanzania yanakuangalia, kazi unayo! | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Jaji Mstaafu Stephen Ihema - macho ya Watanzania yanakuangalia, kazi unayo!

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by Mag3, Sep 13, 2012.

 1. Mag3

  Mag3 JF-Expert Member

  #1
  Sep 13, 2012
  Joined: May 31, 2008
  Messages: 9,094
  Likes Received: 6,188
  Trophy Points: 280
  daudi4.jpg

  Mhe. Jaji Mstaafu Stephen Ihema, hapo juu anaonekana marehemu Daud Mwangosi akiwa na vifaa vyake vya kazi akimhoji Kamanda wa Polisi wa Mkoa wa Iringa, Michael Kamuhanda kabla ya kufikiwa na mauti mikononi mwa polisi wakiongozwa na huyo huyo kamanda wao.

  Mh. Jaji Mstaafu Stephen Ihema, umeteuliwa na umekubali kuongoza kamati ya kuchunguza kifo hicho cha mwandishi ingawa waliokuteua ndio hao hao watuhumiwa ambao mwanzoni walitaka kuuaminisha umma kuwa hawakuhusika na kifo hicho na walijaribu kutupa lawama kwa chama cha siasa.

  Mh. Jaji Mstaafu Stephen Ihema, licha ya wengine wetu kuonesha kutokuwa na imani na jinsi kamati ilivyoundwa na kuwa na wasi wasi na uteuzi wako kuiongoza, ulijitokeza na kutuomba tuwe na subira na tusitilie shaka na utendaji wako pamoja na kwamba historia haiko upande wako.

  Mh. Jaji Mstaafu Stephen Ihema, hili halikuwa tukio la kwanza wala la kipekee, hapana, huko nyuma tumeshuhudia kazi za kamati au tume za aina hii kama uliyopewa. Ni matumaini ya wengi kuwa utasimamia ukweli na kama utakumbana na tatizo lolote lile, utapata ujasiri wa kukabiliana nalo.

  Ombi langu kwako Mh. Jaji Mstaafu Stephen Ihema, kumbuka marehemu Daudu Mwangosi keshazikwa hawezi kujitetea kwa mdomo. Hata hivyo ushahidi wa wazi anao marehemu Mwangosi mkononi na begani hadi kifo kinamkuta...vifaa vyake hivyo vya kazi, camera na laptop, hakikisheni mmevipata.
   
 2. C

  Curriculum Specialist JF-Expert Member

  #2
  Sep 13, 2012
  Joined: Oct 8, 2007
  Messages: 2,736
  Likes Received: 3
  Trophy Points: 0
  Jaji aache kuchunguza jambo lililoko mahakamani tayari anaingilia uhuru wa mahakama!
   
 3. Lokissa

  Lokissa JF-Expert Member

  #3
  Sep 13, 2012
  Joined: Nov 20, 2010
  Messages: 7,079
  Likes Received: 155
  Trophy Points: 160
  kiini macho tu kwanini hawakusuburi kazi ya kamati ndio wampeleke?
  na Tanzania huwa polisi wanakurupuka kupeleka watu mahakamani wakati ushahidi bado
  nchi pekee duniani watu wanapelekwa mahakama bila ushahidi.
   
 4. KOMBAJR

  KOMBAJR JF-Expert Member

  #4
  Sep 13, 2012
  Joined: Nov 15, 2011
  Messages: 5,848
  Likes Received: 8
  Trophy Points: 135
  Ihema anatakiwa kufuata nyao za Jaji Kipenka. Sasa sijui atajipendekeza kwa mteule wake au kulinda heshima yake mbele ya umma wa watanzania. Wameanza kwa kuwaibia wajumbe wa kamati vifaa ili wasifanikiwe.

  Ihema u need to prof them wrong wote wanaokutilia mashaka ueledi wako otherwise utakuwa umejiaribia hasa baada ya statement yako kwa umma,
   
 5. MATESLAA

  MATESLAA JF-Expert Member

  #5
  Sep 13, 2012
  Joined: Aug 11, 2011
  Messages: 1,252
  Likes Received: 6
  Trophy Points: 0
  Makubwa paka kapewa gereza awalinde panya
   
 6. K

  KINUKAMORI Member

  #6
  Sep 13, 2012
  Joined: Sep 11, 2012
  Messages: 39
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Ninapooona picha ya mwangosi wakati akiwa hai roho inaniuma sana jamani:A S cry:, sioni hata kitu knachochunguzwa,maana kila kitu kiko wazi mno mwanzo hadi mwisho wa kifo chake, tunapotezeana muda tu, ila vile ni sheria hebu tusubiri jaji atoe maamuzi ya busara
   
 7. Julius Kaisari

  Julius Kaisari JF-Expert Member

  #7
  Sep 13, 2012
  Joined: Oct 12, 2010
  Messages: 1,174
  Likes Received: 34
  Trophy Points: 145
  Wewe Jamaa wewe... umekomaa hapo Jaji "MSTAAFU"..lol.. Mag3
  Haya bwana mkubwa. Watz tushazoea kuuziwa Mbuzi kwenye viroba. Hatutegemei jipya.
   
  Last edited by a moderator: Jan 4, 2016
 8. Mag3

  Mag3 JF-Expert Member

  #8
  Sep 14, 2012
  Joined: May 31, 2008
  Messages: 9,094
  Likes Received: 6,188
  Trophy Points: 280
  Mkuu ukwelikitugani, nakomaa na huyu jamaa kwa sababu watu tangu awali kabisa walionesha wasi wasi kwa vigezo vilivyotumika katika kuunda kamati na kumteua Mh. Jaji Mstaafu Stephen Ihema kuongoza hiyo kamati. Lakini yeye mwenyewe alijitokeza akituomba tusiwe na shaka juu yake kwani alidai anazo sifa achilia mbali rekodi yake katika utumishi ambayo pia anadai imetukuka. Wengine hiyo rekodi anayoongelea inakuwa shida kuiamini ingawaje tunajua amewahi kuwa Kamishna wa Maadili na Mwenyekiti wa Mfuko wa Uadilifu, Uwajibikaji na Uwazi.

  Lakini kusema kweli hatuna cha kujivunia kimaadili, kiuwajibikaji wala kiuwazi... matendo ya viongozi wetu hayana cha uadilifu, uwajibikaji wala uwazi. Hivi sasa huenda hata kiswahili kimebadilika...huko TAKUKURU kuzuia rushwa ni sawa na kubariki rushwa, huko vyombo vya Usalama kuzuia fujo kumebadilika na kuwa kuanzisha fujo na kulinda raia na mali zake tafsiri yake sasa ni kuua, huko serikalini ufisadi na wizi ndio utumishi bora na mahakamani haki inageuzwa kuwa dhuluma. Mh. Jaji Mstaafu Stephen Ihema, damu ya Daud Mwangosi inakulilia, inalilia ukweli na inalilia haki.
   
 9. Cynic

  Cynic JF-Expert Member

  #9
  Sep 14, 2012
  Joined: Jan 5, 2009
  Messages: 5,154
  Likes Received: 628
  Trophy Points: 280
  Huyo Kamanda ana roho ngumu mno. Angekuwa na akili timamu angekuwa ameshaachia ngazi zamani tu.
   
Loading...