Jaji Mstaafu Mark Bomani alonga, CCM yahofu Katiba Mpya

Rutashubanyuma

JF-Expert Member
Sep 24, 2010
217,039
728,455
SIKU chache baada ya Waziri wa Sheria na Mambo ya Katiba, Cellina Kambani kuseam hakuna haja ya kuwa na katiba moya, Jaji Mkuu Mstaafu, Mark Bomani amesema kinachoisumbua serikali ya CCM ni uwoga ambao hauna msingi wowote. Katiba inyotumiwa hivi sasa, kwa kiasi kikubwa imepitwa na wakati na inakinzana yenyewe katika baadhi ya vifungu, huku ikishindwa kutoa picha halisi ya demokrasia na utawala bora. Waziri wa Sheria na Katiba, Celina Kombani wiki hii alikaririwa na vyombo vya habari akisema suala la kuunda katiba mpya haliwezekani kwa kuwa serikali haina fedha na kwamba itaendelea na utaratibu uliozoeleka wa kufanya marekebisho ya katiba pale inapohitajika.

Jaji Bomani alisema kinachotakiwa hivi sasa ni kufanyika kwa mapitio ya kina ya katiba iliyopo na kuainisha upungufu wote, kisha kufanya mabadiliko kwa mujibu wa mahitaji. "Nadhani ni woga ambao hauna msingi wowote, wanahofia kile ambacho watu watapendekeza katika katiba mpya, lakini mimi naamini watu wakikaa chini na kutulia, hawawezi kuja na vitu vya ajabu," alisema Jaji Bomani.

Madai ya serikali ya CCM kuhofia kitakachofuata baada ya kupatikana kwa katiba mpya, pia yalitolewa na Mhadhiri wa Sheria wa Chuo Kikuu cha Mzumbe, Profesa Mujwahuzi Njunwa, ambaye aliongeza kuwa hata CCM kama wakija kushindwa katika uchaguzi mkuu, watakuwa mstari wa mbele kudai mabadiliko ya katiba. "Hii ni tabia ya watawala wengi, kuwa na woga na kutokukubali mabadiliko, jambo hili linatoa picha kuwa serikali haipo kwa maslahi ya wananchi na taifa," alisema Profesa Njunwa.

Hata hivyo, akizungumzia hoja ya matumizi ya nguvu ya umma iliyotolewa na Chadema hivi karibuni, iwapo CCM watagoma kusikiliza hoja za mabadiliko ya katiba, Profesa Njunwa alisema serikali haiwezi kungojea hali hiyo itokee. "CCM wanabusara, hawatapenda kuona nchi ikiingia katika matatizo, nina uhakika hivi sasa wanaangalia upepo unavyovuma na kasi ya watu kudai katiba mpya," alifafanua Profesa Njunwa. Jaji Bomani ambaye aliwahi pia kuwa Mwanasheria wa serikali, aliishauri serikali kuunda jopo la wataalam kutoka sekta mbalimbali watakao pitia sheria iliyopo na kuja na mapendekezo ya kuwa na katiba mpya, jambo ambalo alisema litamaliza mvutano uliopo. Kwa upande wake, aliyekuwa Mbunge wa Jimbo la Vunjo kwa tiketi ya CCM katika Bunge lililopita, Aloyce Kimaro alisema ni vema serikali ikapewa muda wa kujipanga, lakini alisema kuna ulazima wa kuwa na mabadiliko kwa katiba. "Hakuna nafasi kwa serikali kutosikia, na kama wataziba masikio, wananchi watawalazimisha kusikia. Lazima kuwe na mfumo unaoleweka, hizi si zama za watu wachache kuamua juu ya mambo ya nchi," alisema Kimaro. Utata wa katiba

Naye Mhadhiri wa Kitivo cha sheria, Chuo Kikuu cha Dar es Salaam, Profesa Chris Maina alipozungumza na Mwananchi Jumapili, alifafanua kwa kina baadhi ya maeneo yenye utata katika katiba iliyopo. Profesa Maina alisema Tanzania ni Jamhuri ya Muungano wa nchi mbili, serikali mbili na katiba mbili, katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania ya 1977 na Katiba ya Zanzibar ya 1984. Alisema kwamba hivi sasa kuna kero nyingi za muungano. "Tunaweka vyombo visivyo vya kikatiba kuyashughulikia mambo haya mazito,ukiangalia kamati ya Waziri Mkuu na Waziri Kiongozi wa Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar, kamati hii haina chanzo chake kwenye Katiba wala sheria yoyote ile. Hivyo uhai wa Kamati hii haufahamiki, kwa mfano kwa sasa Zanzibar haina Waziri Kiongozi kikatiba ni nani anawakilisha Zanzibar katika Kamati hiyo, Makamu wa Kwanza au wa Pili wa Rais au ndiyo imekufa?," alihoji Profesa Maina na kuongeza:
"Hivi karibuni Katiba ya Zanzibar ilifanyiwa mabadiliko ya Kumi ya mwaka 2010, mabadiliko haya yakaanzisha Serikali ya umoja wa Kitaifa. Mabadiliko haya yapo tofauti kabisa na serikali ya Zanzibar inavyoelezwa katika sura ya nne ya Katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania (Sura hii ina Sehemu Tatu, inahusu Serikali ya Mapinduzi na Rais wa Zanzibar; Baraza la Mapinduzi na Baraza la Wawakilishi – Ibara ya 102 hadi 207). Hivyo, Katiba hizi mbili zinaongea vitu viwili tofauti na hivyo kuchanganya wananchi".

Maina alitaja mgongano mwingine wa kisheria katika katiba iliyopo ni mabadiliko ya kumi yaliyofanywa katika katiba ya Zanzibar.
Katika mabadiliko hayo, Mahakama ya Rufaa imeondelewa uwezo, lakini mahakama hiyo ilianzishwa na Katiba ya Jamhuri ya Muungano na kutangazwa kuwa ni chombo cha muungano (Union Matter).

"Pia mabadiliko ya Kumi ya Katiba ya Zanzibar yamevichanganya vyama vya siasa. Kwa mfano, Chama Cha Wananchi (CUF) kwa upande mmoja (Zanzibar) ni sehemu ya utawala kama mshirika katika Serikali ya Umoja wa Kitaifa. Lakini, katika Bunge la Jamhuri ya Muungano kinataka kiwe sehemu ya upinzani dhidi ya chama tawala ambacho ni mshirika wake huko Zanzibar".

Kwa mujibu wa Prof Maina, kuna Ibara na vifungu kadhaa vimefutwa katika katiba zote mbili na kuachwa hivi hivi.

"Angalia kwa mfano Ibara ya 10; 80; 82 ya katiba ya Jamhuri ya Muungano; na Vifungu 98; 102A; 103 vya Katiba ya Zanzibar. Vile vile, kuna vifungu vya Katiba ambavyo havitumiki na haviwezi kutumika katika hali halisi ya nchi yetu," alisema Prof Maina. Pia alitoa mfano wa sehemu inayohusu Mahakama Maalum ya Katiba ya Jamhuri ya Muungano ambayo wanaoweza kushtakiana ni Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar na Serikali ya Jamhuri ya Muungano tu (Sehemu ya Saba ya Sura ya Tano ya Katiba – Ibara ya 125 hadi 128) na kuangaliza kuwa katiba ya nchi haitakiwi iwe hivyo.

"Hivyo, kuna haja ya kuachana na mabadiliko na kutafuta utaratibu wa kutafuta Katiba zilizo bora kwa pande zote mbili za Jamhuri ya Muungano," alishauri.

Katika juhudi za kupata katiba mpya Mwaka 1991, Tume ya Jaji Nyalali ilipendekeza kuanzishwa kwa mfumo wa utawala wa vyama vingi vya siasa, na kupendekeza kuwepo kwa katiba mpya na si kurithi katiba ya chama kimoja ambayo muhimili wake ulikuwa tofauti. Hoja hizo hazikupewa majibu na vyama vingi vya siasa viliingizwa ndani ya katiba ya mwaka 1977, kupitia mabadiliko ya Nane ya mwaka 1992, yaliyotungiwa Sheria ya Vyama vya Siasa Namba 5 ya 1992. "Mwaka 1998 Kamati ya White Paper ilipoundwa chini ya Jaji wa Mstaafu wa Rufani Robert Kisanga pia ilipendekeza umuhimu wa kuwa na katiba mpya. Lakini kamati hiyo ilipowasilisha ripoti yake ilikemewa eti imevuka mipaka yake kwa sababu ilikuwa Kamati na siyo Tume.
 

tanga kwetu

JF-Expert Member
May 12, 2010
2,194
1,432
...tukisubiri chama tawala CCM kuleta katiba mpya, hawataileta kamwe so wenyenchi watanzania wakweli rtuidai kwa gharama yoyote! mimi nipo tayari wewe je?
 

Bams

JF-Expert Member
Oct 19, 2010
10,766
23,679
Mamlaka ya serikali, bunge na mahakama hutoka kwenye katiba, na juu ya vyote ni jamhuri (wananchi). Wengi tunafanya makosa tukiamini kuwa wajibu wa kuruhusu katiba mpya ni wa serikali na CCM. Hilo ni kosa kubwa. Wananchi wanatakiwa kuamua kuwa wanataka katiba mpya, mwisho. Baada ya hapo serikali, mahakama, bunge na vyombo vingine vielekezwe majukumu yao katika kutekeleza hilo.

Katika kufikia uamuzi huo, tunatakiwa tukumbuke maneno ya mwalimu kuwa, 'ukitaka haki kutoka kwa mtawala na hasa inayoenda kinyume na matakwa yake, ni lazima udhihirishe kwa vitendo kuwa hiyo ni haki yako, na unaihitaji', kama hatuwezi kufanya hivyo tusiwe na mategemeo kuwa serikali hii na chama chake cha CCM ndiyo watakaotuongoza kupata katiba mpya. Tuwaoneshe kuwa tunataka katiba mpya, na wao hawana uamuzi wa kusema ndiyo au hapana bali waliongoze zoezi katika kufikia uamuzi wetu.
 

Mgeninani

Senior Member
Jan 3, 2010
191
9
Mie ndo nashangaa wakuu humu badala ya kujadili watadai vipi hili wanakesha wakijadili nani muislam na nani mkristu, kwani TANESCO wakitangaza mgao wa umeme wanaumia kina nani? bei ya mafuta? sembe na maharagwe?haya mambo ya dini si mkajadili kwenye blog za dini huko kama hakuna anzisheni za kwenu!
 

Rogers_ic

Member
Nov 7, 2010
51
0
Mie ndo nashangaa wakuu humu badala ya kujadili watadai vipi hili wanakesha wakijadili nani muislam na nani mkristu, kwani TANESCO wakitangaza mgao wa umeme wanaumia kina nani? bei ya mafuta? sembe na maharagwe?haya mambo ya dini si mkajadili kwenye blog za dini huko kama hakuna anzisheni za kwenu!

mimi huoudini nausikia kwenye vyombo vya habari, bado sijauona
 

Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Similar Discussions

0 Reactions
Reply
Top Bottom