Jaji Mkuu wa Tanzania, Prof. Ibrahim Juma atangaza kufuta ada kwa nyaraka mbalimbali za kimahakama nchini

Makambo zali

Senior Member
Sep 23, 2017
180
433
jaji mkuu.jpg

--------------------
MAONI YANGU

Jaji Mkuu,unapofuta gharama za mahakama hizo mahakama zitoe wapi pesa za kujiendesha?

Naona Jaji Mkuu kaamua watu wafungue kesi bure,nakala za hukumu bure,kila kitu bure,kwa hiyo kuanzia sasa mtu yeyote hahofii gharama,anakushitaki bure anavyotaka,mahakama inatoa karatasi za bure ushtakiwe,inatoa nakala za hukumu bure.

Mahakama na hasa Jaji Mkuu anadhani Tanzania inaogelea kwenye bahari ya hela,kasamehe gharama zote,kompyuta za mahakama zinatumia wino,makaratasi,maji,umeme,mishahara,

Yeye kaamua kugawa sandakalawe ya kila kitu!!

Huyu mtu azuiwe haraka sana
 
Vizuri sana kama hizi taarifa ni za kweli...

Itasaidia wale wasiokua na uwezo wa kutetea haki zao sasa kupata fursa...

Cc: mahondaw
 
Mleta mada umekurupuka kwa umasikini wa nchi hii unadhani hicho kitu ni kama ulivoandika.Kwa kifupi ni kila kitu kinalipiwa na world bank mwisho wa siku zinapelekwa idadi ya hukumu na kesi zote za madai mzungu analipa.
 
Mleta fafanua kwa nini unahisi haiwezekani kwa huu utaratibu mpya
 
Naona Jaji Mkuu kaamua watu wafungue kesi bure,nakala za hukumu bure,kila kitu bure,kwa hiyo kuanzia sasa mtu yeyote hahofii gharama,anakushitaki bure anavyotaka,mahakama inatoa karatasi za bure ushtakiwe,inatoa nakala za hukumu bure.

Mahakama na hasa Jaji Mkuu anadhani Tanzania inaogelea kwenye bahari ya hela,kasamehe gharama zote,kompyuta za mahakama zinatumia wino,makaratasi,maji,umeme,mishahara,

Yeye kaamua kugawa sandakalawe ya kila kitu!!

Huyu mtu azuiwe haraka sana
Kwa taarifa yako mahakama haiendeshwi kwa tozo na faini inazotoza, bali inaendeshwa na mfuko mkuu wa serikali. Hizo tozo na faini zinazotozwa na mahakama zinaingia katika mfuko mkuu wa serikali sawa na tozo na faini za polisi!
 
mleta mada huna akili na umekurupuka kwa umasikini wa nchi hii unazan icho kitu n kama ulivoandika..kwa kifupi n kila kitu kinalipiwa na world bank mwisho wa siku zinapelekwa idadi ya hukumu na kesi zote za madai mzungu analipa
Huu ni uongo mtakatifu! Umeamua kuidhalilisha serikali!!
 
Back
Top Bottom