Jaji mkuu wa Kenya amewataka wanasiasa kutii sheria

kirerenya

JF-Expert Member
Aug 27, 2013
1,696
2,252
maraga.jpg

Jaji mkuu wa Kenya,David Maraga ameilaumu serikali ya nchi hiyo kwa kufanya maamuzi kinyume cha sheria na katiba ya kenya katika kukabiliana na upinzani .

Tamko hilo limekuja mara tu baada ya kiongozi mmoja wa upinzani wakili Miguna Miguna kufukuziwa nchini Canada,baada ya kuzuiliwa na polisi kwa siku tano hata baada ya mahakama kutoa amri kwamba aachiliwe kwa dhamana .

Katika maelezo yake jaji David Maraga ,amesema malalamiko yaliyopelewekwa mahakamani yalikuwa wazi ,na yalikuwa majukumu ya mahakama kufanya maamuzi kwa kuwa ndio chombo pekee cha kutetea haki kwa kila mmoja pamoja na serikali yenyewe.

Jaji huyo ametoa tamko hilo la kuionya serikali kwa kushindwa kutii sheria kutokana na kitendo cha serikali ya kenya kuonekana kudharau maamuzi ya mahakama.

Licha ya kuwa serikali ya Kenya kupitia wizara ya mambo ya ndani kujitetea kwa ufafanuzi juu ya uraia wa wakili huyo wa upinzani Miguna Miguna,kwa msemaji wa wizara hiyo Mwenda Njoka kusema kwamba kiongozi huyo "kwa makusudi alishindwa" kuweka wazi kuwa alikuwa na uraia wa nchi nyingine wakati alipopatiwa hati ya kusafiria ya Kenya mnamo Machi 2009,wakati ambao uraia wa nchi mbili ulikuwa hauruhusiwi .
 
Ana piont ila lawama angewalimbikizia NASA na mzee Raila. Kwa kubaka katiba na sheria zote kwa kile kioja chao tarehe thelathini januari pale bustani ya Uhuru Park! Sasa wenzao kwenye upande wa pili ndo wameanza kuiga mtindo huo. Kwenye kumbukumbu za historia itakumbukwa kwamba rais mstaafu Daniel Toroitich Arap Moi alianza wazimu na udikteta wake 1982. Hii ni baada ya jaribio la kwanza la kupindua serikali, kabla ya hapo alikuwa mzee mwenye heshima zake! Walimuita Nyayo, ila Raila akisaidiwa na wanajeshi wa kitengo cha Airforce walimvuruga akili kwa jaribio lao hilo la kupindua serikali. Hapo ndo alianza kuwatupa wapinzani korokoroni na kujihusisha na viongozi wa kabila lake pekee yake. Imefika wakati wa Raila kustaafu. Ameletea nchi yetu tukufu ya Kenya majonzi tupu, miaka nenda miaka rudi!
 
Ana piont ila lawama angewalimbikizia NASA na mzee Raila. Kwa kubaka katiba na sheria zote kwa kile kioja chao tarehe thelathini januari pale bustani ya Uhuru Park! Sasa wenzao kwenye upande wa pili ndo wameanza kuiga.
Kwa siasa za Kenya mkuu ni kheri utangulie kuuliza aliyesema ni kabila gani?
Yani judge kakaa kimya kuhusu raila kujiapisha ila kakomaa na serikali
 
Kwa siasa za Kenya mkuu ni kheri utangulie kuuliza aliyesema ni kabila gani?
Yani judge kakaa kimya kuhusu raila kujiapisha ila kakomaa na serikali
Wala sidhani huyu mlokole ana ukabila wa aina yeyote, anafanya kazi yake ipasavyo. Ila wadogo zake ndo wameshindwa kufanya kazi zao kwa haki. Itabidi awapige kiboko ndo heshima irejee. Rudi kwenye comment yangu hapo juu utaelewa kuna mengi tu ambayo yamebaki yanajirudia rudia kwenye siasa za Kenya.
 
Back
Top Bottom