Jaji Mkuu Ramadhani: Chadema hawana makosa!!

Luteni

JF-Expert Member
Jan 9, 2010
2,274
0
Jaji Mkuu Agustine Ramadhani amesema kisheria hakuna kosa lililofanywa na wabunge wa Chadema kutoka nje wakati wa hotuba ya Rais, akaongeza hata kanuni za bunge ziko kimya kuhusu kitendo hicho ndiyo maana hata Spika hakusema lolote "labda tunaweza kulieleza ni suala la kimaadili tu lakini si kisheria"

Source TBC 1.

Nafikiri hili ni jibu kwa Chaligati na wote waliokuwa wanadhani wabunge wa Chadema wamevunja sheria.
 
PayGod

JF-Expert Member
Mar 4, 2008
1,259
1,225
Ujumbe huu namtumia chiligati , ambaye ni hazijui sheria za bunge na hata katiba ya nchi
 
MkamaP

JF-Expert Member
Jan 27, 2007
8,080
2,000
Mie ningependa kuuliza. Je wabunge wa chadema baadhi yao wakipewa uwaziri watagoma ama itakua je? Naomba mtazamo wenu.
 
Mungi

JF Gold Member
Sep 23, 2010
16,980
2,000
Kuna watu katika watu huwa hawajui, lakini hawajui kama hawajui ( John Chiligati hajui hata katiba) - Hao tunawaita wapumbavu.

Kuna watu katika watu huwa wanajua, na wao wanajua kuwa wanajua ( CHADEMA wanaijua Katiba ) - Hao tunawaita Werevu

Kuna watu katika watu huwa hawajui, na wao wanajua hawajui ( CCM hajisomei katiba ) - Hao tunawaita Wajinga
 
Pasco_jr_ngumi

JF-Expert Member
Nov 20, 2010
1,804
1,225
Chiligati, Makamba, jiuzulu muende mkapumzke vjijn...mkalme. Nyerere alfanya hvo.
Siasa za mwaka 47 sio sawa na 2010
 
Oxlade-Chamberlain

JF-Expert Member
May 26, 2009
8,584
2,000
Hivi kweli wakuu kuna watu walikuwa hawajui kwamba wabunge ku-walk out ni jambo la kawaida bungeni kokote duniani? au ni watoto mno kiasi cha kwamba hawajawai kuona kokote duniani kutokea? au ndio tunapenda kujifanya wajinga hata kama tunajua jambo?
 
Tofty

JF-Expert Member
Nov 6, 2008
206
195
Jaji Mkuu Agustine Ramadhani amesema kisheria hakuna kosa lililofanywa na wabunge wa Chadema kutoka nje wakati wa hotuba ya Rais, akaongeza hata kanuni za bunge ziko kimya kuhusu kitendo hicho ndiyo maana hata Spika hakusema lolote "labda tunaweza kulieleza ni suala la kimaadili tu lakini si kisheria"

Source TBC 1.

Nafikiri hili ni jibu kwa Chaligati na wote waliokuwa wanadhani wabunge wa Chadema wamevunja sheria.

Asante sana.......
 
gomezirichard

Member
Nov 2, 2010
71
0
Warioba naye ameona kuwa still kuna tatizo la katiba by the way huwa yeye hayupo na ,mambo yanayofanywa na sisiem ila ukweli ndio huo amesema katiba imetungwa miaka mingi na ni haki yao kudai katiba ibadilike.

Mfano sera ya Michezo na habari inasema michezo yote itakua ikifanyika kwenye vijiji vya ujamaa hii nisera ya miaka hiyooooooo,
wapi leo kuna vijiji vya ujamaa leo ukiongea vijiji vya ujamaa tunajua viraka vya suruali

Mzee GOMEZI
 
Quinine

JF-Expert Member
Jul 26, 2010
20,129

Kwenye bold inaonyesha kweli katiba imepitwa na wakati, hivi kwa nini Kikwete asiweke historia kwamba Tanzania ilibadili katiba peacefully au anasubiri tutwangane kwanza.
 
Taso

JF-Expert Member
Jun 12, 2010
2,269
2,000
Jaji zembe hili. Si kazi yako kutoa viji comment vya kuhukumu ni nini sawa na nini si sawa kisheria ukiwa nje ya mahakama.
 
Tanzania

Senior Member
Jun 6, 2008
115
195
Jaji Mkuu Agustine Ramadhani amesema kisheria hakuna kosa lililofanywa na wabunge wa Chadema kutoka nje wakati wa hotuba ya Rais, akaongeza hata kanuni za bunge ziko kimya kuhusu kitendo hicho ndiyo maana hata Spika hakusema lolote "labda tunaweza kulieleza ni suala la kimaadili tu lakini si kisheria"

Source TBC 1.

Nafikiri hili ni jibu kwa Chaligati na wote waliokuwa wanadhani wabunge wa Chadema wamevunja sheria.

Wabunge wa CHADEMA, msiyumbishwe na maneno yoyote. Naomba mjue kuwa nyuma yenu kuna watanzania wengi wenye ufahamu wa nini ninaendelea katika nchi. Jueni kwamba mnapigania uhuru na si vinginevyo. Tanzania iko kwenye giza nene na ni wacahache wanaweza kuikomboa. Amabo ni ninyi. Mungu awatangulie.
 
Mzee Dogo

JF-Expert Member
Nov 13, 2010
395
250
Jaji zembe hili. Si kazi yako kutoa viji comment vya kuhukumu ni nini sawa na nini si sawa kisheria ukiwa nje ya mahakama.
Huku ni kujaribu kuwafumba macho watanzania wasioijua katiba, ccm wamesema yao lakini huyu waliyemweka kuhakikisha sheria inafuatwa ndivyo kasema hali ya mambo ilivyo kulingana na taaluma yake, kama huwezi kutoa kitu chenye mantiki ni bora ukatunza charge yako uitumie next time....
Rudi kasome tena katiba kama utapenda lakini, just kwa faida yako!
 
Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Top Bottom