Uchaguzi 2020 Jaji Mkuu: Ni marufuku kwa Jaji, Msajili wa Mahakama na Hakimu kujiunga na Chama cha Siasa

Hizi ni Sarakasi zile zile..alitakiwa kuwaagiza wajivue uanachama kutoka vyama vya siasa kwani zaidi ya 50% ya Majaji&Mahakimu wa nchi hii wana kadi za CCM.Watakuja kujitetea baadae kuwa walioambiwa ni wale ambao hawajajiunga na sio kwa wale ambao tayari ni wanachama. Jaji Mkuu awe wazi kuwa wajivue uanachama kuanzia lea na akianzia na Hakimu Simba anayepewaga kesi za upinzani...
Ni wale wazee, vijana wako neutral.
 
Haya yako wazi hata kwenye Katiba na Sheria ya vyama vya siasa, alichofanya Prof Ibrahim Juma ni kukumbusha tu. Bahati mbaya anakumbusha mambo ya msingi wakati uongozi wa JPM haujali misingi ya utawala wa Sheria, demokrasia na katiba yenyewe.

Yeye mwenyewe Prof Juma kama Chief Justice yuko mfukoni mwa JPM. Hawezi kuamua kwa namna anavyoelewa na anavyoamini bali kwa vile anavyotaka JPM. Mfano ni maamuzi ya kesi ya kikatiba iliyofunguliwa na Advocate Sanga vs AG juu ya haki ya dhamana. Au kesi ya Bob Wangwe vs Ag juu ya Wakurugenzi kuwa wasimamizi wa uchaguzi.

Tukubali tu JK alituingiza mkenge kutomaliza mchakato wa Katiba Mpya mwaka 2015.
 
Back
Top Bottom