Kaveli
JF-Expert Member
- Dec 4, 2012
- 5,412
- 8,813
Kwa jinsi madudu ya ufisadi yanavyozidi kuibuliwa kwenye Taasisi/Office za serikali, ni wazi kuwa we 'urgently' need in place ile Mahakama ya Mafisadi.
Ufisadi mkubwa katika Taasisi hizi: TANAPA, TRA, TPA, NIDA, TRL, n.k. unazidi kutushtua watanzania. Sasa tunaanza kuona jinsi nchi hii inavyoliwa na 'wenye nchi' wachache huku 'wananchi' wakibakia kwenye lindi la umaskini.
Leo tena huko ATCL (shirika la ndege Tanzania) napo kumeibuliwa ufisadi wa kutisha !
Wazungu wanatunyonya, na watanzania pia nao wanatuibia na hawachukuliwi hatua sitahiki. WHY hii linchi limekuwa 'shamba la bibi' kiasi hiki? Hakika haya mambo yanazidi kujenga chuki kubwa sana kwa wananchi dhidi ya serikali.
Tusitegemee lolote kwenye hizi Mahakama za kawaida zilizopo, maana zishakuwa corrupt, majaji ni wale wale, na truly zipo over-burdened na mrundikano wa kesi.
RAI yangu kwa Jaji Mkuu & Tume ya Mahakama, harakisheni kuuanzisha hiyo Mahakama ya Mafisadi ili huu 'upigaji' unaoibuliwa upelekwe kwenye hiyo Mahakama.
Mafisadi na Mapigaji yanazidi kuichezea hii nchi. Watu wafikishwe Mahakamani haraka under 'urgency' procedure na Hukumu itolewe haraka.
DPP, Police, Jaji Mkuu, please msirudishe nyuma jitihada njema za Rais wetu za kurejesha heshima na weledi kwenye utumishi wa umma. Wajibisheni haraka hayo majizi ili jamii ijifunze.
Hili Taifa kwa jinsi linavyonuka rushwa na ufisadi wa rasimali za umma, sio muda wa kuchekeana chekeana tena! Tunataka kuona majizi ya mali za umma yanafikishwa mahakamani, haki inatendeka, yanafilisiwa kwa mujibu wa sheria, na yanapelekwa jela.
Fanyeni vitendo ili Taifa lirejeshe imani juu yenu. Wananchi wamechoka sana ndugu zangu. Tumechoka na magumashi ya linchi hili.
Narudia: ACHENI KUCHEKA CHEKA NA MAJIZI YA MALI ZA UMMA !!
- Kaveli -