Jaji Mkuu: Mabilioni ya rais Magufuli yanaboresha Mahakama

AKILI TATU

JF-Expert Member
Feb 10, 2016
1,808
2,000
JAJI Mkuu wa Tanzania, Mohamed Chande Othman amesema kuwa Sh bilioni 12.3 alizitoa Rais John Magufuli kwa ajili ya ujenzi na ukarabati wa majengo ya mahakama nchini zinaendelea kutumika kujenga majengo ya kisasa ya mahakama katika wilaya 10.

Jaji Mkuu Othman alibainisha hayo kwa nyakati tofauti wakati alipokutana na Mkuu wa Mkoa wa Rukwa, Zelothe Steven na baadae alipokuwa akizungumza na watumishi wa mahakama kutoka katika mikoa ya Katavi na Rukwa mjini Sumbawanga leo akiwa katika ziara ya siku moja mkoani humo.

Alisema ujenzi wa majengo ya mahakama hizo ambao uko katika hatua za mwisho yamejengwa kwa bei nafuu yakiwa imara, yenye hadhi ambayo ujenzi wake hadi kukamilika kwake utachukua miezi mitatu.

Aidha alizipongeza mahakama zilizopo katika Kanda ya Sumbawanga kwa kuweza kumaliza kero ya utoaji wa nakala za hukumu na mwenendo wa mashauri kwa wakati.

Alisisitiza kuwa msimamo uliotolewa Siku ya Sheria Duniani iliyofanyika Februari 4 mwaka huu ulisisitiza nakala hizo zitolewe ndani ya siku 21.

“Utoaji wa nakala za hukumu mwenendo wa kesi ni tatizo kubwa nchini, lakini kwa mkoa wa Rukwa sio tatizo tena niwapongeze sana kwa kuongoza nchini changamoto kwenu ni kuhakikisha muweze kutoa nakala hizo ndani ya siku saba au vizuri zaidi ili muoneshe kweli mnaongoza mzitoe siku hiyo hiyo iliyotolewa hukumu,” alieleza Jaji Mkuu Othman.

Alisema hata alipokutana na Mkuu wa Mkoa, Zelothe alimweleza kuwa hadi sasa amepokea malalamiko ya ucheleweshaji wa utoaji wa nakala za hukumu kutoka kwa mlalamikaji mmoja tu.
 

mwasu

JF-Expert Member
Jul 13, 2011
10,203
2,000
Eeeeh, yamesaidia pia kunyima uhuru wa mahakama na kubadili sheria zitumike kwa matakwa ya watawala badala ya kufuata katiba, hongera waongeze na nyingine.
 

jogi

JF-Expert Member
Sep 25, 2010
25,646
2,000
Mabilioni hayo yameinunua mahakama, maana siku hizi dhamana imekuwa haki ya serikali
 

Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Top Bottom