Jaji Mkuu(CJ) chunguza Mahakama kuu kitengo cha mashauri ya kazi

nyundo2017

JF-Expert Member
Sep 7, 2017
1,439
858
Habari Jaji Mkuu,
Kwa heshima na taadhima napenda kuchukua hatua hii kukujulisha kuwa kitengo cha mashauri ya kazi mahakama kuu inachelewesha mashauri sana,sana hasa ukizingatia kuna kesi nyingi naza muda mrefu hazijatolewa maamuzi/ hukumu pasipo sababau za msingi.

Kuna shida gani hasa ukizingatia mashauri ya watumishi dhidi ya serikali ndiyo yanachukua muda mrefu sana kuliko mashauri ya watumishi dhidi ya sekta binafsi.

Ucheleweshwaji huu hupelekea serikali kuja kuwalipa watumishi wake pesa nyingi zaidi pale inaposhindwa kesi pasipo sababu za msingi na kwa upande mwingine huwajengea hofu watumishi waliokazini kuwa serikali inawatumia wanapokuwa kazi ila wakionewa na viongozi wa ngazi za juu na baadae kufukuzwa kazi serikali hiyohiyo huwanyanyasa sana.

Kama kesi za albino zilisikilizwa mfululizo basi hata mashauri ya kazi nayo yasikilizwe mfululizo ili kuwatendea haki watumishi walioonewa hasa wa serikali.

Kesi ya madai inachukua miaka 5 kwa ajili ya marejeo tu siyo kwamba usikilizwaji unaanza upya,jamani?

AG saidia hili kwa kupitia upya mashauri yote dhidi ya serikali kuangalia yasiyo na mashiko yaondolewe na kufanya mazungumzo kwa pande zote mbili hii pia itapunguza msongamano wa mashauri ya madai dhidi ya serikali na gharama zisizo za msingi kwa serikali.

Nawasilisha.

"HAKI INAYOCHELEWESHWA NDIYO
INAYOPOTEA"
 
0 Reactions
Reply
Back
Top Bottom