Jaji Mkuu awataka Mawakili kuacha dhuluma.........................

Rutashubanyuma

JF-Expert Member
Sep 24, 2010
219,470
911,173
Mawakili watakiwa kuacha dhuluma
Saturday, 18 December 2010 08:33

James Magai

JAJI Mkuu wa Tanzania, Agustino Ramadhani, amewataka mawakili kuacha dhuluma, tamaa ya kujikusanyia mapato na badala yake, watoe kipaumbe katika kuwahudumia wanyonge kwa kuzingatia kuwa kazi hiyo ni wito.

Jaji Ramadhani aliyasema hayo jana jijini Dar es Salaam, alipokuwa aizungumza katika sherehe za kuwasajili mawakili wapya 337 wa kujitegemea.
Sherehe hizo zilifanyika katika Viwanja vya Karimjee.

Kiongozi huyo wa mahakama anayetarajiwa kustaafu rasmi Desemba 28 mwaka huu, alisema katika kipindi cha miaka mitatu na nusu ambacho amekuwa madarakani, ameshuhudia dhuluma nyingi, zikiwemo zinazofanywa na mawakili.

“Mtindo huu katu ninyi mawakili wapya msiufuate. Nawasihi mfuate miiko ya kazi. Kipato kamwe msikipe kipaumbele. Mawazo yenu yote na nguvu zenu zielekezwe katika kuwatetea wanyonge. Uwakili kwa hakika siyo biashara bali ni wito,”alisema Jaji Ramadhani.

Aliwataka mawakili hao wafuate kile alichokiita kuwa ni kielezo alichowapa, kwa jinsi alivyojitoa na kuwasaili hata kwa muda wake wa ziada na hatimaye kuwathibitisha kwamba ni wanasheria wanaofaa.

“Ninyi wenyewe mmeona jinsi nilivyojitoa ili kuwasaili na kuwathibitisha kuwa mnafaa kusajiliwa kuwa mawakili. Nimefanya kazi hiyo Jumamosi na hata Jumapili,"alisema.


Mkongwe huyo wa sheria aliongeza kuwa "nimekaa ofisini mwangu wakati mwingine hata saa kumi na moja na hata saa kumi na moja na nusu jioni nikiwahudumia. Hii ni kwa sababu nimeona uchungu kuwaacha hadi mwezi Juni mwakani 2011.”

Kwa upande wake, Rais wa Chama cha Wanasheria Tanganyika, Felix Kibodya aliwataka mawakili hao watambue kuwa wao ni kioo cha jamii.

Aliwataka wawe waungwana katika kutoa huduma za msaada wa kisheria kwa wananchi huku wakizingatuia kuwa Watanzanai wengi, hawana uwezo wa kulipia gharama za huduma za uwakili.

Kibodya pia aliwataka mawakili hao kuzingatia maadili ya kazi na kujifunza kutunza fedha za wateja wao, ili kuepuka kuitia doa fani yao.

Mwanasheria Mkuu wa Serikali, Jaji Fredrick Werema, katika hotuba yake iliyosomwa na Naibu Mwanasheria Mkuu wa Serikali, Geoge Masaju, aliwataka mawakili hao kuishi kwa misingi ya kanuni za taaluma yao.

Alisema wao kama maofisa wa mahakama, kila mmoja ana wajibu wa kuhakikisha kuwa mwenendo wake na uendeshaji wa shughuli zake mahakamani, vinakidhi malengo ya haki na kudumisha uadili wa mfumo wa mahakama.
 
Rutashubanyuma JAJI Mkuu wa Tanzania said:
Mbona mahakama ndio inaongoza kwa kudhulumu wananchi?
1. Kesi ya mgombea binafsi
2. Kuchelewa kuhudumia kesi mahakamani
3. Kuchelewa kutoa maamuzi/hukumu

Charity should begin at home
 
Dhuluma kubwa alifanya yeye siku hiyo kwa kutowaapisha mawakili kufuatia pingamizi la chuki la AG asubuhi hiyohiyo licha ya kuwa wamelipa ada,kuhakikishiwa na kustahihili.Aibu sana Brig.Gen.CJ
 
Mbona mahakama ndio inaongoza kwa kudhulumu wananchi?
1. Kesi ya mgombea binafsi
2. Kuchelewa kuhudumia kesi mahakamani
3. Kuchelewa kutoa maamuzi/hukumu

Charity should begin at home

Spot on man.........................It is equivocation................
 
Dhuluma kubwa alifanya yeye siku hiyo kwa kutowaapisha mawakili kufuatia pingamizi la chuki la AG asubuhi hiyohiyo licha ya kuwa wamelipa ada,kuhakikishiwa na kustahihili.Aibu sana Brig.Gen.CJ

Pia tukumbuke mgombea binafsi jinsi ambavyo alituburuta visivyo na kinyume cha sheria...................
 
Pia tukumbuke mgombea binafsi jinsi ambavyo alituburuta visivyo na kinyume cha sheria...................

Kweli kabisa, CJ, Agustino Ramadhan, ataondoka ameacha doa kubwa sana katika taaluma ya Sheria kuhusu Mgombea Binafsi!
 
A Ramadhani CJ, alichemka katika shauri la Mgombea binafsi. Mpaka leo hukumu ya kisheria haijatoka.
 
Back
Top Bottom