Jaji Mkuu awaita wastaafu Afrika Mashariki

kilimasera

JF-Expert Member
Dec 2, 2009
3,068
268
WASTAAFU wa iliyokuwa Jumuiya ya Afrika Mashariki (EAC) wamesema kuwa wamepewa barua inayowataka kufika mahakama ya rufaa kesho kwa ajili ya kusomewa mapitio ya kesi yao ambayo Jaji Mkuu, Augustine Ramadhani aliamua kuitisha jalada lake na kuipitia. Jaji Mkuu alitoa barua ya kupitia jalada la wastaafu hao mwezi uliopita ikiwa ni siku chache baada ya wastaafu hao kuzua kizaazaa nje ya viwanja vya Mahakama Kuu jijini Dar es Salaam.

Madai ya wastaafu hao ni malipo ya Sh2 trilioni zikiwa ni mafao yao baada ya kuvunjika kwa jumuiya hiyo mwaka 1977 iliyoshirikisha nchi za Tanzania, Uganda na Kenya lakini Mahakama iliishinisha walipwe Sh 117 bilioni. Wastaafu hao hivi karibuni walifunga Barabara ya Kivukoni Front kwa kulala katikati ya barabara kwa takriban saa saba wakipinga uamuzi wa kujitoa kwenye kesi hiyo wa Jaji Njengafibili Mwaikugile wa Mahakama Kuu aliyekuwa akisikiliza shauri lao.

Kabla ya tafrani hiyo, wastaafu hao walifika mahakamani hapo kwa kile walichokiita kuwa ni kupewa hati ya malipo, lakini kinyume na matarajio yao Jaji Mwaikugile alitangaza kujitoa.

Akizungumza na Mwananchi mweka hazina wa Jumuiya hiyo, Ramadhani Makingi, alisema kuwa wamepewa barua hiyo tangu Desemba 10, mwaka huu ambayo inawataka kufika Mahakama hapo Desemba 15 saa 3 asubuhi kwa ajili ya kusomewa mapitio ya kesi yao.

Kwa mujibu wa barua ya Jaji Mkuu yenye kumbukumbu Na DA/111/196/01/5,aliyoandika mwishoni mwa mwezi Novemba na kusainiwa na katibu wa jaji huyo, Ruwaichi Meela ilisema : “Jaji Mkuu anakusudia kulifanyia mapitio jalada la kesi husika (ya wastaafu wa EAC) ili kujiridhisha kuwa Mhe Jaji wa Mahakama Kuu aliyesikiliza kesi hii, alizingatia mwenendo wa shauri na ushahidi wa kesi uliokuwa mbele yake na pia alizingatia sheria husika.” “... Shughuli kama hiyo inataka utulivu wa akili na siyo shinikizo la maandamano.

Mhe Jaji Mkuu ana nia thabiti ya kuhakikisha suala hili kwa jinsi mahakama inavyohusika linamalizika kwa haraka iwezekanavyo,” inaeleza barua hiyo. Makingi alisema kitendo cha Jaji Mkuu kupitia upya jalada la kesi yao kinaonyesha jinsi anavyowajali wastaafu wa jumuiya hiyo na kusisitiza kuwa wana imani kubwa kuwa kesi hiyo itamalizika salama na wao kupatiwa fedha wanazodai.

“Barua hii tumeipata tangu Novemba 10 ambayo inatutaka tufike mahakama ya rufaa kwa ajili ya kusomewa mapitio ya kesi yetu, kwa hiyo tutakwenda kwa ajili ya kujua nini tutakachoelezwa, sidhani kama itakuwa tofauti, lakini tukielezwa kuwa hatuna cha kudai tutakaa na kujua nini la kufanya,” alisema Makingi. Hatahivyo,barua hiyo ilieleza kuwa kama wastaafu hawakuridhika na hukumu ya shauri lao iliyotolewa na Jaji John Utamwa wa Mahakama Kuu, wastaafu hao walitakiwa wakate rufaa au waombe mapitio ya kesi yao.
 
Back
Top Bottom