Jaji Mkuu awaapisha mawakili wapya166 awataka kuwajibika kwa mujibu wa Katiba ya nchi

beth

JF-Expert Member
Aug 19, 2012
3,877
6,326
Jaji Mkuu wa Tanzania Prof. Ibrahimu Juma amewataka mawakili 166 wapya walioapishwa leo kuziishi kanuni na maadili akiwataka kuwajibika kwa mujibu wa Katiba ya nchi ambayo ndiyo sheria mama akiwataka kutojihusisha na vitendo vya ujanja ujanja.

Jaji Mkuu ametoa rai hiyo katika hafla ya kuwapokea mawakili wapya 166 ambapo amewataka kusimamia misingi ya haki ili kuisaidia mahakama kufikia maamuzi ya kesi mbalimbali za wateja wao kwa wakati.

''Kwa sasa changamoto ya ajira ni kubwa katika dunia ya ushindani duniani unakuwa kwa kasi teknojia ukichukua nafasi hivyo mawakili hawana budi kupambana na changamoto hii''. Prof Ibrahimu Juma

Aidha amewaonya Mawakili ambao wamekuwa wakitumia Lugha zisizofaa katika mitandao ya kijamii kwa kutumia majina halisi na wengine majina yasiyo halisi ambao wamekuwa wakikosoa kanuni na sheria zilizowekwa
 
Jaji Mkuu wa Tanzania Prof. Ibrahimu Juma amewataka mawakili 166 wapya walioapishwa leo kuziishi kanuni na maadili akiwataka kuwajibika kwa mujibu wa Katiba ya nchi ambayo ndiyo sheria mama akiwataka kutojihusisha na vitendo vya ujanja ujanja.

Jaji Mkuu ametoa rai hiyo katika hafla ya kuwapokea mawakili wapya 166 ambapo amewataka kusimamia misingi ya haki ili kuisaidia mahakama kufikia maamuzi ya kesi mbalimbali za wateja wao kwa wakati.

''Kwa sasa changamoto ya ajira ni kubwa katika dunia ya ushindani duniani unakuwa kwa kasi teknojia ukichukua nafasi hivyo mawakili hawana budi kupambana na changamoto hii''. Prof Ibrahimu Juma

Aidha amewaonya Mawakili ambao wamekuwa wakifanya vitendo vya uchochezi katika mitandao ya kijamii kwa kutumia majina halisi na wengine majina yasiyo halisi ambao wamekuwa wakikosoa kanuni na sheria zilizowekwa
Kukosoa sheria na kanuni zilizowekwa!
 
hahah yani jaji mkuu hataki watu wakosoe kanuni mbovu????
Vitendo vya ujanja ujanja ndiyo vitendo gani? Kinyume chake ni vitendo vya ujinga ujinga. Nani anataka kuwa mjinga mjinga. Mimi nadhani Tanzania tungechagua maneno mengine ya kuelezea vitendo vya ''ujanja ujanja'' kwani kama unamnyima mtu kufanya vitendo vya ujanja ujanja ataonekana kama mjinga mjinga.
 
Back
Top Bottom