Jaji Mkuu awaagiza Mawakili kuhakikisha wanawasaidia wananchi kupata huduma za kisheria

Kurzweil

JF-Expert Member
May 25, 2011
6,622
8,410
Jaji Mkuu awaagiza Mawakili kuhakikisha wanawasaidia wananchi kupata huduma za kisheria hasa wale wasiokuwa na uwezo.
jaji%20chande.jpg



Baada ya Bunge kupitisha sheria ya uanzishwaji wa Divisheni ya Rushwa na uhujumu uchumi Jaji Mkuu Othumani Chande amesema Jumatatu ijayo mkandarasi aliyepewa jukumu la kujenga jengo kwa ajili ya mahahakama hiyo anatarajiwa kukabidhi tayari kwa kuanza kazi wakati Rais akisubiriwa kuweka saini sheria hiyo.

Mh chande ameyasema hayo alipokuwa akiwaapisha mawakili zaidi ya 600 ambapo amesema taratibu zote zimeshakamilika na tarehe kumi mwezi huu majaji waliopoangwa katika mahakama hiyo watakuwa na mkutano wa utendaji.

Naye Jaji kiongozi Mh. Ferdinard Wambali amewataka mawakili hao wapya kwenda kufuata kanuni na sheria za kiwakili na wahakikishe wanawasaidia wananchi kupata huduma za kisheria hasa wale wasiokuwa na uwezo.

Wakizungumza baada ya kula kiapo hicho baadhia ya mawakili wamesema wanatambua jukumu lilipo mbele yao na watahakaisha wanakwenda kusimamia sheria katika kuwasaidia wananchi kuweza kupata haki zao.
 
angeenda Pemba , Mkuu wa Polisi Msangi wa huko amesema atawsakamata mawakili wanao tetea watuhumiwa.....Jaji mkuu ni wa Tanzania Tunge furahi kupata neno lake kulaaani ujinga huu
Msangi alikuwa anaongea kichama, jaji anaongea kisheria.
 
Kwa Mawakili kusaidia wananchi wasio na uwezo bure hilo aisee halipo kabisaa.
Yaania naona alikuwa anafurahisha ukumbi tu,maana hao lengo ni kuapishwa tu kisha waje mtaani kupiga issue,maana Mawakili wapo teleeee,wapo Wajanja kibaoooo kwenye fani hiyo,na wapo wale Makini sana kwenye Kazi hii.
Na ndio maana unaweza kukuta mtu anaanza kesi na wakili fulani,baada ya muda akinusa jamaa amekula dili sehem ya pili anampiga chini nakutafuta wakili mwingine.
 
angeenda Pemba , Mkuu wa Polisi Msangi wa huko amesema atawsakamata mawakili wanao tetea watuhumiwa.....Jaji mkuu ni wa Tanzania Tunge furahi kupata neno lake kulaaani ujinga huu
Hawezi kulaani sababu ni zao la la Watawala actually utashangaa kesho akimuunga mkono.Kwa sasa hakuna Mahakama wala Bunge kuna Polisi ,Jeshi na serikali tu
 
Back
Top Bottom