MWANASHERIA
Member
- Aug 20, 2010
- 84
- 11
Jana, nimeona nakala ya barua ya Jaji mkuu akisema anakusudia kulipitia faili la wazee wa EAC. angalizo, (ANAKUSUDIA), sio kwamba analipitia. Nilipoisoma barua niligundua ilikua na nia ya kuwanyamazisha Wazee wa watu, ile leo wasifanye maandamano yao ya Amani, na ndio maana CJ akapeleka copy ya barua Polisi, ili polisi wawazuie. Nalazimika kuamini kwamba CJ katumwa, na kwa sasa matukio yanaonyesha kabisa anafanya kazi kama Executive (yaani, Serikali) badala ya JUDICIAL officer. (Officer wa mahakama) na hivyo kuua mhimili mmoja muhimu wa Dola (Mahakama). Kama kulipitia file ni kwa nia ya kuwasaidia hawa wazee wapate haki stahiki za kwao, ni vizuri, lakini kama CJ ametumwa na anafanya hivyo ili kuwakandamiza wazee, basi anavuna Dhambi katika hili.