JAJI MKUU, ANaVUNA DHAMBI KWA WAZEE WA E.A COMMUNITY

MWANASHERIA

Member
Aug 20, 2010
84
11
Jana, nimeona nakala ya barua ya Jaji mkuu akisema anakusudia kulipitia faili la wazee wa EAC. angalizo, (ANAKUSUDIA), sio kwamba analipitia. Nilipoisoma barua niligundua ilikua na nia ya kuwanyamazisha Wazee wa watu, ile leo wasifanye maandamano yao ya Amani, na ndio maana CJ akapeleka copy ya barua Polisi, ili polisi wawazuie. Nalazimika kuamini kwamba CJ katumwa, na kwa sasa matukio yanaonyesha kabisa anafanya kazi kama Executive (yaani, Serikali) badala ya JUDICIAL officer. (Officer wa mahakama) na hivyo kuua mhimili mmoja muhimu wa Dola (Mahakama). Kama kulipitia file ni kwa nia ya kuwasaidia hawa wazee wapate haki stahiki za kwao, ni vizuri, lakini kama CJ ametumwa na anafanya hivyo ili kuwakandamiza wazee, basi anavuna Dhambi katika hili.
 
ASIPOKUA MAKINI ATATUFKISHA MAHALI WATANZANIA KUTAFUTA NJIA MPYA YA KUPAMBANA NA UNYONYWAJI NA UNYANYASWAJI NDANI YA NCHI YETU WENYEWE!

WAKATI WA KUOMBA KURA WAZEE NDO WANAOMBWA KUISAIDIA SERIKALI NA WAKISHAINGIA MADARAKANI HATA HAIWAKUMBUKI....HII NI LAANA KWA KWELI

eh! KWELI SERIKALI IONE AIBU SASA!!!!!!!!!!!!!!
 
CJ,ameitisha file kwa lengo la kulipitia,hii ni mamlaka aliyonayo kisheria ya kuita kesi yoyote yenye mwenyewe(suo motu) kwa hili kama we mwenzangu ni mwanasheria wa ukweli utakuwa unalielewa.Tujitahidi kuongea vitu with actual proof.
 
CJ,ameitisha file kwa lengo la kulipitia,hii ni mamlaka aliyonayo kisheria ya kuita kesi yoyote yenye mwenyewe(suo motu) kwa hili kama we mwenzangu ni mwanasheria wa ukweli utakuwa unalielewa.Tujitahidi kuongea vitu with actual proof.

Kwanini iwe sasa hivi na sio zamani???...ukweli utajulikana kama sio leo basi kesho!
 
CJ,ameitisha file kwa lengo la kulipitia,hii ni mamlaka aliyonayo kisheria ya kuita kesi yoyote yenye mwenyewe(suo motu) kwa hili kama we mwenzangu ni mwanasheria wa ukweli utakuwa unalielewa.Tujitahidi kuongea vitu with actual proof.

Sijabisha kuhusu mamlaka, suala ni kwanini leo, sio siku zote, kwanini awaagize na kuwataarifu polisi wasitishe maandamano ya amani? Kwani asingeweza kulipitia file huku wakiwa wanaandamana?
I am questioning MENS REA na sio ACTUS REUS? Anaintend nini kuliita file? je anataka kuwasaidia wazee, au haki itendeke? Au anataka kutumia sheria kuwakandamiza wazee wa watu? au katumwa. kama alivyosema hapo juu, tutajua ukweli soon or later.
 
Hili hata mimi linanitia wasiwasi sana, inaonekana kua dhambi kabisa, maana ianakuwa kama wameambiwa chelewesha chelewesha miaka mingine mitano watakuwa wamepungua. Hivi ni kiasi gani wanadai hawa wazee wetu muda mrefu namna hiyo? Kinachosikitisha ni mwakati familia ya kigogo inapewa stendi ya mabasi kujitafunia tu. \Wala serikali haijataka kufanya tathimini ya kiasi cha hasara ili waagizwe warejeshe. Yaani vitu vinasahaulika kirahisi tuu. Tanzania wacha ni nchi ya aina yake, waliosema shamba la bibi, sipati jina bora zaidi!
 
Hebu acha bana usinitoe machozi, nasikitika sina jinsi ya kuwasaidia ony that I can pray for them!!!
 
kweli inauma sana hao wazee wamekosa nini kwa mungu, hata kama hawastahili serikali ione aibu ifanye kama inawasaidia kama ilivyosaidia makampuni ya jamaa zao ikisingizia kuimarisha uchumi kutokana na mtikisiko wa dunia, rais inawezekana kuwakandamiza wazee hawa lakini kumbuka mungu naye yupo walau muogopeni yeye. cj haki iliyochelewa ni sawa na haki iliyonyimwa nilikuwa nina imani sana na wewe mzee lakini katika hili nimepoteza imani. hawa ni wazee wetu ikishindikana itisheni harambee tuwachangie kuliko kuwapiga na mabomu na maji ya kuwasha, mabomu na maji ya kuwasha wanastahili mafisadi mnaogonganisha nao glasi, kagoda 40b, mramba na wenzake 11b, liyumba 122b, hebu oneni aibu walipeni wazee haki yao. inaumiza na kusikitisha sana
 
. cj haki iliyochelewa ni sawa na haki iliyonyimwa nilikuwa nina imani sana na wewe mzee lakini katika hili nimepoteza imani.

Pole sana ndugu tumpale, sisi tulipoteza imani na cj siku nyingi hasa kuanzia kwa ile hukumu ya mgombea binafsi. Alishajionyesha wazi kuwa yeye ni mtu wa serikali na si mhimili unaojitegemea. Pole sana kwa kuchelewa kumuelewa!
 
Back
Top Bottom