Jaji Mkuu akosoa utendaji wa criminal justice system Tanzania

bagamoyo

JF-Expert Member
Jan 14, 2010
21,285
24,161
July 19, 2019

Jaji Mkuu wa Tanzania Prof. Ibrahim Hamis Juma, ameelezea ziara yao ndefu ya kikazi mikoa ya kanda ya ziwa iliyoanza mapema Julai 4, 2019. Mahakama imebaini aina ya adhabu zinazotolewa, kasi ya upelelezi na adhabu zinazotolewa.

Kutokana na hayo, Mh. Jaji Mkuu amekosoa mtindo wa wapelelezi na ofisi ya Mwendesha Mashitaka kufikisha kortini kesi wakati upelelezi haujakamilika.

Pia Jaji Mkuu ana maoni kuwa dhamana iwe ni haki kwa watuhumiwa wote na masharti ya dhamana yapunguzwe. Akaongeza kwa makosa madogo, hata kitambulisho cha uraia kiweze kutumika watuhumiwa wapate dhamana na kupunguza msongamano wa mahabusu.

Jaji Mkuu akatoa mfano wa hulka iliyojengeka ya 'kamata na sukuma ndani' ambayo inapelekea mahabusu na magereza kujaa watuhumiwa kupita kiasi.

Mh. Jaji Mkuu anashangaa hata kesi za madai / civil case kama za kandarasi pia amri hutolewa kuwa mkandarasi atupwe mahabusu wakati kuna taratibu na kanuni ya jinsi ya kushughulikia madai hayo kortini.

Jaji Mkuu Ibrahim Hamisi Juma ametoa mapendekezo kuwa, mamlaka zinazohusika na kutunga sheria za adhabu kutokushikilia kutunga sheria za adhabu kali, bali kuangalia kutunga sheria zinazoendana na uzito wa kosa husika.
Source : millard ayo

 
Hahaha aliambiwa mahakama haziko huru, kuna hukumu za kisiasa akakataa.

Mtu anakamatwa kwanza anatupwa mahabusu bila dhamana, kisha ndio wanaanza kufikiria kesi ya kumpa.

Hii yote ni ccm kukomoa watu, halafu mwisho wa siku mtuhumiwa anaachiwa eti serikali haioni haja ya kuendelea na kesi hiyo.

Watu hawaendi mahakamani kushitaki kwasababu mahakama ni mali ya ccm, jaji huyo akiambiwa mahakama hazitendi haki anang'aka lakini leo anapiga siasa.

Juzi anamuaga jaji Pande kasema mfumo wa mahakama uko vizuri hakuna anayeonewa, leo anaongea tofauti, hahaha siasa za ccm kila kona unafiki tupu.

Tuliisha sema humu, na tuliisha uliza sana. Kwanini mtu akae mahabusu, kwa miaka 7-10 eti upelelezi haujakamilika. Sasa kwanini wasipeleleze kwanza kasha wakiisha pata ushahidi wa crime huyo mtu ashitakiwe.

Lakini unapomkamata mtu, unamuhukumu kwa kumuweka mahabusu muda mrefu, halafu kesi inaanza kusikilizwa kila siku inahairishwa kwa sababu eti ushahidi/upelelezi haujakamilika, huo ni uonevu na siho haki hata kidogo.

Siku ya sharia alisema mahakama iko huru, Juzi wana muaga jaji kiongozi akasema mahakama hiingiliwi na kushauri watu waende mahakamani kupata haki. Leo anasema tunayosema sisi na tunaambiwa tunaihujumu serikali.
 
Hahaha aliambiwa mahakama haziko huru, kuna hukumu za kisiasa akakataa.
Mtu anakamatwa kwanza anatupwa mahabusu bila dhamana, kisha ndio wanaanza kufikiria kesi ya kumpa. Hii yote ni ccm kukomoa watu, halafu mwisho wa siku mtuhumiwa anaachiwa eti serikali haioni haja ya kuendelea na kesi hiyo.
Watu hawaendi mahakamani kushitaki kwasababu mahakama ni mali ya ccm, jaji huyo akiambiwa mahakama hazitendi haki anang'aka lakini leo anapiga siasa. Juzi anamuaga jaji Pande kasema mfumo wa mahakama uko vizuri hakuna anayeonewa, leo anaongea tofauti, hahaha siasa za ccm kila kona unafiki tupu.
Huyo ndiye Ibrahim Juma , CJ
 
‘Only in Tanzania’ achilia dhamana tu head of justice anakumbuka baada ya ziara ya rais kuwa hakuna time limit katika sheria zetu zinazowataka polisi kumaliza upelelezi wao au kumwachia mtu huru.

Wakati makosa mengi madogo time frame ni 48 hours tu duniani huna ushahidi mwache mtu huru

Mambo mengine yanawezekana Tanzania tu. Sitoshangaa nikisikia watu maskini wanaenda mahakamani bila ya uwakilishi na watu wanakaona sawa tu.
 
Mihimili Mitatu ina viongozi, lakin huyu anafanya vema nimewapa marks kwamba wote wana share 100% ila nimezigawa hivi
Jaji Mkuu 45%
Rais 39%
Spika 16%
 
27 June 2021

TUNATAKA DPP ONGEA NA WANANCHI, KUWE NA UWAZI" KATIBU MKUU WIZARA YA KATIBA NA SHERIA


Katibu Mkuu Wizara ya katiba na Sheria Prof Sifuni Mchome amewataka leo mwezi June 2021 makatibu wakuu na wakuu wa Taasisi kuangalia ni vitu gani ambavyo vitakuwa na manufaa katika kuandaa Sera ya Taifa ya mashtaka kwa manufaa ya Nchi . Katibu Mkuu huyo amesema hayo wakati wa Mkutano uliowakutanisha Makatibu wakuu pamoja na wakuu wa Taasisi za kusimamia haki jinai ili kujadili mapendekezo ya kuandaa Sera ya Taifa ya mashtaka.

Source : millard ayo
 
Back
Top Bottom