Jaji mkuu akamilisha jengo la mahakama kwa fedha alizotengewa yeye!

p0123.jpg

Pinda kwenye ufunguzi. Hii kazi ya mikasi lakini siyo yake imekuwaje aichukue?
 
mmmh swali langu hizo za kurekebisha nyumba yake atazipataje tena???
bongo hakishindikani kitu! hizo hela alipewa ili afanye kama alivyofanya ila 'siasa' tu akasema eti zilikuwa za nyumba yake etc!

BTW: Wacha1 mbona umeweka picha kuuuubwa! punguza size yake, unajua mpaka inaboa kuiangalia!
 
mmmh swali langu hizo za kurekebisha nyumba yake atazipataje tena???

Kama nyumba ipo katika hali nzuri ya nn uanze kutumbua fedha kwa vile zipo?
Hongera sana Jaji kwa kumwonyesha mfano waziri mkuu Pinda anae pigia kelele mashangingi lakini kwenye msafara wake utakuta yapo zaidi ya 20 na yeye akiwa amelipanda.
 
Huwa najua kuwa ni ya PATEL au ROSTAM kumbe wakurugenzi ni Gilabhadi Pindolia na Jianesh Mandwama. reference ktaba wa ujenzi wa jengo la UVCCM.

Msemo wa Nyerere "Mkiwapa hawa watu nguvu ya kututawala watatutawala tu lazima tuangalie haya mambo watanzania"

Sasa hapo "UVCCM" Just angalieni ni kwanini au mwataka kutuambia hakuna Makapuni ya watanzania native ambao wanaweza hizi kazi au ndio kudhihakiana sie ngozi nyeusi au ndio mwataka kuutukuza msemo usemao BLACK IS BLACK hat iweje? jamani imefika mahari hii hali tusiiendekeze.

Majuzi nilikuta na mtu katokea India akaniambi hata kama umefanikiwa fungua kiwanda India usitegemee utaajiri watu weusi huko kutoka nchi za afrika sahau ilo kule ni utaajiri wa hindi pure no compromising kwa hilo. sasa nchi hii watu weupe ndio wanaongoz a kwa tenda zote
 
MiTanzania bwana!!!
Kuna post moja nilisoma hapa kwamba huyu mheshimiwa ata-staafu mwishoni mwa mwaka huu 2010... kama ni za kweli basi sina hata sababu ya kumsifia... ila tunamshukuru, kwa ku-score vizuri kwenye kujua vipaumbele... kwa sababu tofauti hapa nijengo lip lianze kujengewa... lakini eventually yote yatajengwaa....

Angezipeleka kwenye hiyo nyumba angeishi humo kwa muda gani?

Alafu acheni siasa bwana... nyumba ya jaji mkuu ni nyumba ya jaji mkuu sio ya Augustino Ramadhan... padashi
 
 
mahzf.jpg

 Mama Elizabeth Said, akiangalia Sanamu ya Mumewe iliyoandaliwa kumkumbuka
 
mah6.jpg

Waziri Mkuu Mhe. Mizengo Pinda (Wa kwanza kushoto) akifuatiwa na Mke wa hayati Jaji Mkuu wa kwanza wa Mahakama ya Rufaa mhe. Augustine Said Bibi Elizabeth Said wakiwa kwenye picha ya pamoja na Majaji wakuu wastaafu akifuatiwa na Barnabas Samatta (wa tatu kulia) na Lewis Makame( wa pili kulia) na nyuma ni Sanamu ya hayati Augustine Said
 
mah2.jpg

 Jaji Mkuu Msaafu Mhe.Barnabas Samatta (wa kwanza kushoto) na wa pili kushoto ni Jaji Mkuu wa Mahakama Mhe. Augustino Ramadhani wakizungumza na Waziri Mkuu Mhe. Mizengo Pinda kwenye Ofisi ya Mahakama ya Rufaa
 
mah3.jpg

 
 Jaji Mkuu Mhe. Augustino Ramadhani akizungumza na Waziri Mkuu Mhe Mizengo Pinda kwenye Ofisi ya Mahakama ya Rufaa kabla hajazindua Mahakama hiyo

Picha: Hisani ya Michuzi blog
 
Watu kama hawa ndio wanatakiwa tatizo viongozi wetu wana ubinafsi sana kuliko uzalendo hawajali kabisa walau Jaji Mkuu kaonyesha wazi na kaalika viongozi kuhudhuria, Huu ni mfano wa kuigwa kabisa.
 
Tunaposema VIPAUMBELE ni lazima tumaanishe hivyo.

Ukisikia waziri anajibu bungeni kwamba ...oooh serikali haina fedha za mradi huu wala ule lakini kabla hajamaliza usemi utasikia serikali imeagiza magari ya kifahari kwa viongozi wake waandamizi.....

Jaji mkuu ana maanisha anachofikiria na anachokisema tofauti na jaji werema na wanasiansa wenzake kule bungeni
 
mah5.jpg


Waziri Mkuu Mhe. Mizengo Pinda (Alievaa suti) na Jaji Mkuu( wa kwanza kushoto) Mhe. Augustino Ramadhani na (wa pili kshoto) ni mke wa hayati Augustine Said wakiwa kwenye picha ya pamoja na Majaji wa Mahakama kuu wakati wa sherehe za uzinduzi wa mahakama ya Rufaa jijini Dar
 
mah1.jpg

 
Mke wa hayati Augustine Said Bibi Elizabeth Said (Wa tatu shoto) pamoja na familia yake na wageni waalikwa wakisikiliza hotuba ya Waziri Mkuu Mhe. Mizengo pinda leo jijini Dar

 
mah4r.jpg


Mke wa hayati Augustine Said Bibi Elizabeth Said (Wa kwanza Kushoto) pamoja na familia yake wakisikiliza hotuba ya Waziri Mkuu Mhe. Mizengo pinda leo jijini Dar es Salaa

Picha: Hisani ya Michuzi blog
 
Twampongeza Jaji kwa alilolifanya....la ukarabati.

.....ila la Kujenga SANAMU hilo limeongeza gharama isiyo ya lazima...Ujenzi wa sanamu ile ungeweza saidia akina mama wengi tu hospitali...!!!

Kila atakaeingia madarakani akitaka achongewe sanamu lake tutakuwa na masanamu mangapi jamani...?
 
Hongera sana muheshimiwa jaji angalau umeweza kuonyesha njia lakini tatizo ni kwa hao viongozi wetu je wataweza kuuchukua huo kama mfano wa kuigwa ama wataendelea kuwa na mioyo migumu na kuendelea kujineemesha nafsi zao na familia zao bila kujali watoto yatima mitaani wanazagaazagaa. Ahsante muheshimiwa jaji.
 
Namfahamu Jaji Augustino Ramadhani tangu akiwa kijana. Anatoka kwenye a very humble family of late Mwalimu M. Ramadhani aliyekuwa miongoni mwa waalimu waafrika wa Tabora School miaka ya 1960s. Bahati mbaya, miaka hiyo hiyo ya 1960s sikumbuki mwaka, alipokuwa Uingereza kujiendeleza kimasomo akafariki dunia kwa ajali ya treni na kuwaacha akina Augustino wakingali vijana wadogo. Wamelelewa na mama yao very humbly na ni wacha Mungu sana. Kwa hiyo, sishangai kabisa kwa Augustino kufanya hiyo noble gesture ya kutumia fedha alizotengewa yeye na kuzitoa zitumike kwa ajili ya kumbukumbu ya aliyekuwa Jaji Mkuu wa Kwanza wa nchi yetu baada ya nchi kupata Uhuru.

Si hilo tu ambalo judge Ramadhani ameweza ku-sacrifice kwa ajili ya wengine, yapo mengine mengi na amefanya hivyo bila motive yoyote binafsi ama kisiasa. Moja ninaloweza kulieleza hapa ni kwamba anayo nyumba Mbagala ambayo aliamua kumwachia Askofu mmoja wa Kanisa la Anglican aishi bure kabisa kwa kuwa Mzee yule alipostaafu alikuwa hana nyumba Dar es Salaam na familia yake ilibidi iishi Dar kwa sababu mbalimbali. Askofu yule aliishi ndani ya nyumba ile kwa miaka zaidi ya 10 bila kutakiwa kumlipa Jaji Augustino chochote hadi Mzee huyo Askofu alipofariki dunia mwaka jana.

Kasheshe, Pape et al,
Nyie mwaweza kuyafanya hayo?
 
Kasheshe, Pape et al,
Nyie mwaweza kuyafanya hayo?

Bibi Ntilie,

Hata mimi nafahamu angalau kwa kidogo kwamba kama kuna watumishi watatu WASAFI nchini basi jaji AR. atakuwepo ... ninalokataa ni hili hapa.

1. Hilo jengo liliokuwa linajendwa ni la Jaji Mkuu wa Tanzania sio la Jaji Augustino Ramadhani.
2. Waliokadiria (budget) kwamba majengo hayo mawili la Jaji na la Mahakama ni hao hao.
3. Jaji mkuu anastaafu karibuni kwa tetesi za hapa jamvini... mwaka huu kama sikosei... hivyo hakuna masilahi kwake kujenga helo hekalu.
----> kilichofanyika ni changes of priority lakini majengo yote mawili yatajengwa... nothing special to me.
 
Bibi Ntilie,

Hata mimi nafahamu angalau kwa kidogo kwamba kama kuna watumishi watatu WASAFI nchini basi jaji AR. atakuwepo ... ninalokataa ni hili hapa.

1. Hilo jengo liliokuwa linajendwa ni la Jaji Mkuu wa Tanzania sio la Jaji Augustino Ramadhani.
2. Waliokadiria (budget) kwamba majengo hayo mawili la Jaji na la Mahakama ni hao hao.
3. Jaji mkuu anastaafu karibuni kwa tetesi za hapa jamvini... mwaka huu kama sikosei... hivyo hakuna masilahi kwake kujenga helo hekalu.
----> kilichofanyika ni changes of priority lakini majengo yote mawili yatajengwa... nothing special to me.

kama mambo yangekuwa hivyo basi hata Mkapa +Mramba wasingenunua Presidential Jet ambayo kwa sasa kila kona ya dunia IMESHATEMBELEA, Jaji mkuu hana tamaa hata kidogo na amekuwa akipigania saana uborweshaji wa mahakama zetu, kumbuka ni majuzi tu alilalamika kwama budget anayopewa ni ndogo ukilinganisha na budget ya msajili wa vyama vya siasa.Upo hapo BONGO NI SIASA KWANZA
 
Eti gharama za sanamu zingeenda kusaidia wanawake hospitali.. Come on, you people sometimes..hehehe
 
kumbuka ni majuzi tu alilalamika kwama budget anayopewa ni ndogo ukilinganisha na budget ya msajili wa vyama vya siasa.Upo hapo BONGO NI SIASA KWANZA

Tuko pamoja! kwa sababu kwa Tanzania SIASA KWANZA. i love my country.

Lakini majengo yote yatajengwa... kwa sasa limetangulia la mahakama then la jaji mkuu... okay!
 
Bibi Ntilie,

Hata mimi nafahamu angalau kwa kidogo kwamba kama kuna watumishi watatu WASAFI nchini basi jaji AR. atakuwepo ... ninalokataa ni hili hapa.

1. Hilo jengo liliokuwa linajendwa ni la Jaji Mkuu wa Tanzania sio la Jaji Augustino Ramadhani.
2. Waliokadiria (budget) kwamba majengo hayo mawili la Jaji na la Mahakama ni hao hao.
3. Jaji mkuu anastaafu karibuni kwa tetesi za hapa jamvini... mwaka huu kama sikosei... hivyo hakuna masilahi kwake kujenga helo hekalu.
----> kilichofanyika ni changes of priority lakini majengo yote mawili yatajengwa... nothing special to me.

Kasheshe,
Unaweza ukawa sahihi - majengo hayo yatajengwa.

Lakini, tukubaliane kwamba kutokana na uadilifu wa Jaji Augustino Ramadhani hata kama angelikuwa hastaafu mwaka huu, angeliweza sana kuamua kama alivyoamua sasa. Sitaki kukubali kwamba aliamua kwa sababu aliona kuwa hakuna maslahi kwake kwa kuwa anastaafu.

Kuhusu 'changes of priority' kama ulivyobainisha, sitaki pia kuamini kwamba ujenzi wa hekalu la judge na jengo la Mahakama ni priorities zinazozidi vifo vya akina mama na watoto vinavyotokea kila siku kutokana na huduma duni za jamii katika hospitali zetu, kwa sababu fedha ambazo zingeliweza kutengwa kwa ajili yao zinakwenda kwenye ujenzi wa mahekalu ya afisa mmoja mmoja wa ngazi ya juu Serikalini na ununuzi wa vitu vingine vya gharama kubwa, vya anasa na visivyo vya lazima.

Majumba na ofisi walizoacha wakoloni ziliweza kutumika miaka nenda rudi na zingine hadi leo zinatumika bila kuwa na ukarabati/ujenzi unaotumia fedha nyingi zinazoweza kujenga nyumba nyingine za kawaida hata tatu. Ama zinaweza kutumika kwa mambo mengine yenye manufaa kwa wananchi wengi zaidi. Ni muhimu tuchunguze 'priorities' zetu.

Tunachompongeza Jaji Ramadhani ni kwamba angalau ameonyesha uzalendo katika uamuzi wake huo katikati ya ubadhilifu wa fedha za umma tunaoushuhudia hivi leo nchini mwetu.

Hivi majuzi nilishuhudia msafara wa kiongozi nikabaki mdomo wazi! Magari makubwa makubwa meusi ya bei mbaya na mwisho wa convoy kuna karandinga la FFU - Kiongozi huyo alikuwa anakwenda msibani hapahapa mjini!

Kasheshe, Priorities.
 
Back
Top Bottom