Jaji mkuu akamilisha jengo la mahakama kwa fedha alizotengewa yeye!

hata kama ni mwanasiasa, lakini kitendo cha yeye kubana matumizi au kuzuia matumizi kwa mambo yasiyo na tija anapaswa kupongezwa.
kwanini aishi maisha yenye kufuru katika lindi na umasikini kama huu, heri kaamua kufanya jambo lingine kwa faida ya UMMA.
wangapi wanaweza kukubali kuishi maisha ya kawaida ili kuinufaisha jamii yao ? wachache sana.
nafikiri mawazo yako yamejaa kutu, sioni mantinki ya wewe kutoona mantinki ya Jaji Mkuu.
Ndugu yangu Nguvumali.....akistaafishwa kutoka madarakani say mwaka kesho, successor wake atanyimwa pesa nyingine ya kukarabati jengo atakalorithi?
Ndugu yangu hii yote ni sarakasi tu ambapo aumiaye mwisho wa siku ni walipa kodi (wewe, yule na mimi).
 
Ndugu yangu hilo ni kweli, ila si kwa wote, JM ameonyesha kuwa yupo kwa ajili ya watanzania sio kwa ajili ya familia yake
 
Aibu! Aibu!, Aibu kwa Serikali. Mahakama ni miongoni mwa vyombo muhimu vilivyosahaulika na Serikali za awamu zote 4. Wengi wetu tunatoka vijijini, angalia Mahakama za Mwanzo kule, ni zile alizoacha mkoloni, majengo yake yameshikwa na nguzo dhaifu, kuna ukumbi mdogo uliozungukwa na msingi wa simenti kama viti vya kukalia (mfano ni mahakama ya mwanzo Temeke)ambao unatumika kusikilizia kesi. Chumba cha Mahabusu ni kidogo sana ambacho hakina choo, watuhumiwa hujisaidia kwenye ndoo nakulala na uchafu huo hadi kesho watakapobeba kwenda kumwaga hii ni aibu na ukiukwaji wa haki za binadamu. Sasa Mhe. CJ anaona Idara yake imesahaulika, kwa vile anauchungu na anaona Serikali haina mpango wa kujenga majengo ya Mahakama zaidi ya kuwafurahisha Magavana wa BOT, mawaziri, Makatibu wakuu na wakurugenzi, sasa ameamua kuikumbusha Serikali kwamba Ahadi aliyoiahidi JK siku chache kuhusu kuboresha huduma na kujenga majengo ya kisasa ya mahakama haionyeshi kutekelezwa, bora apalilie njia yeye mwenyewe. Mfano huu ni wakiigwa na watanzania wote wanaoitakia nchi yao mema. Walaaniwe wanaonemesha matumbo yao tu kwa kuhujuma kodi za walala hoi
 
Jaji Mkuu siyo mwanasiasa; ni mwanajeshi (nadhani ni Brig. Generali).. hajawahi kugombea urais wala uenyejikiti wa kijiji..
 
Ndugu yangu Nguvumali.....akistaafishwa kutoka madarakani say mwaka kesho, successor wake atanyimwa pesa nyingine ya kukarabati jengo atakalorithi?
Ndugu yangu hii yote ni sarakasi tu ambapo aumiaye mwisho wa siku ni walipa kodi (wewe, yule na mimi).

We uko dunia gani ndugu yetu????? Pinda mwenyewe kachemsha lakini kamkubali Mh Jaji.Huoni wewe hata mafisadi wanweza kukushangaa kwa maneno yako

Swali kwako MbabeJe kafanya kosa kuzidivert hizo hizo hela kwend kujenga jengo la mahakama ?.
Kama ni sarakasi unavyotaka tuamini basi hizi ni sarakasi za kichina ambazo kila mtu anafurahi kuziangalia. Kuzoea kwako sarakasi za kibongo kusikufanye uone sarakasi nyingine sio bora.

Ifuatayo ni just an amaizing Coincidence.

Yeye na Agustino Ramadhani, wanafafana kwa mengi.
1. Majina yao ya kwanza wote ni jina la Agustino.
2. Majina yao ya kwanza wote ni ya Kikristo
3. Majina yao ya pili wote ni ya Kiislamu, mmoja akiitwa Saidi, mwingine akiitwa Ramadhani.
4, Wote ni Wakristo wachaMungu, Agustino Saidi akihudumu St. Peters na familia yake yote, Agustino Ramadhani akihudumu na mpaka kupiga piano St. Albans.
5. Wote ni majaji Wakuu wa Tanzania wakihudumu chini ya maraisi wenye majina ya JK,
Jaji Saidi chini ya Julius Kambarage, Jaji Ramadhani chini ya Jakaya Kikwete.
Pathetic
 
Hivi Jaji Mkuu wa Tanzania na Gavana wa Benki Kuu nani anaonesha kuijali nchi yake zaidi?

Huu ni uhuni mtupu... Hongera Jaji Ramadhani, kumbe nyumba ya Jaji bado inakalika na haogopi kutekwa kama somebody i know..

Jaji Mkuu ndie anaye jari nchi yake zaidi huyu Ramadhani ni mtu poa sana ila tu ni unakuta mtu swafi yuko kwenye utawala wa viongozi mafisadi unadhani anataongea sana ila vitendo mtaviona tuuu ndio huyo Jaji Mkuu

Hapo Gavana Ndullu alitaka kumwingiza mwenzie kingi akashtuka anajua kuwa siku mkono wa sheria ukipita na wakiwa bado wako hai watajikuta kwa kiti cha hukumu na kuambiwa matumizi mabaya ya fwedha na madaraka Ramadhani kasoma alama za nyakati na kuwataka viongozi wenye nyazifa kama Jaji Mkuu na wengine watambue nini maana ya vyeo vyao na nyazifa walizo nazo katika jamii na watoe mifano hai na sio kusubili wakati wa kampeni ndio wajitutumue.

Safi JAJI RAMADHANI

Nitajaribu kutafuta picha za jengo moja la mahakama za mwanzo na pia kuna swali la muhimu la kujiuliza hapa ni kwamba, kama jengo hili tunajenga kwa gharama hii je huko mikoani itakuaje??

njoo piga picha mahakama ya kawe aibu
kila nkitaka piga nahsi harufu ya segadance
 
nilimwangalia pinda jana akitoa pongezi nikashikwa na hasira
nkasema yaan nchi hii mtu anajinyima na kuipa serikali pesa.n ambapo serikali ilipaswa kusaidia katka hili.

aibu kweli !
 
Hili issue ya Jaji inaibua maswali mengi juu ya utendaji na maamuzi ya baadhi ya watendaji katika utayarishaji na uandaji wa BAJETI

Ni vigezo gani maafisa bajeti, sera ,nk wanatumia kutoa priority na kugawa hela kwenye idara na kazi mbali mbali kweye wizara au tasisi
 
Mfano Mahakama ya Mkoa wa Mwanza Toka nimezaliwa pale na kukua kwangu mpaka umri huu lile jengo Sijui lilipigwa rangi mara ngapi au hata kuboresha vitendea kazi ndani ya hizo Court rooms jamani sijui kama vyaboreshwa? Mahakama zetu nazo ziwe za kuonyesha kweli pale ni mahakama ya mkoa.

Mfano mwingine ni pale shinyanga nimeona kuna Jengo "laenda juu gorofa tatu au nne" ukitokea stand ya mabasi ya mikoani kuelekea njia ya hospitali kuu ya mkoa liko upande wa kushoto, ni jengo la mahakama nadhani kwa ajiri ya Tabora shinyanga na kigoma kitu kama hicho na sidhani kama hilo jengo limeisha na sijui kama litawekewa vitendea kazi vya kisasa kwa ajiri ya shughuri za mahakama?
 
Hili issue ya Jaji inaibua maswali mengi juu ya utendaji na maamuzi ya baadhi ya watendaji katika utayarishaji na uandaji wa BAJETI

Ni vigezo gani maafisa bajeti, sera ,nk wanatumia kutoa priority na kugawa hela kwenye idara na kazi mbali mbali kweye wizara au tasisi

Viongozi wengi wanaenda bungeni just i think for funny kweli kabisa haya yote huwa wanakuwa wapi kuyasemea bungeniii??? kazi ni kupitisha kila bajeti. ivi walisha wahi kutuambia wizara furani bageti yao ilibakisha pesa?

Wabunge wengine wakiwa serious ndani ya huo mjengo wan CCM wanaanza yao majungu sasa nashinda pata picha je huwa kuna mtuu ndie anaye waambia mtu akigeuka CCM basi tumtizame kwa jicho baya?? kuwa yeye ni msaritiiii? CCM imeingia madarakani kufanya biasharaaa IKULU au?

Bunge na wabunge nao wabadirike sasa waende kimaslahi ya nchii na sio maslahi ya vyama vyao au mtu na mtu

We uko dunia gani ndugu yetu????? Pinda mwenyewe kachemsha lakini kamkubali Mh Jaji.Huoni wewe hata mafisadi wanweza kukushangaa kwa maneno yako

Swali kwako MbabeJe kafanya kosa kuzidivert hizo hizo hela kwend kujenga jengo la mahakama ?.
Kama ni sarakasi unavyotaka tuamini basi hizi ni sarakasi za kichina ambazo kila mtu anafurahi kuziangalia. Kuzoea kwako sarakasi za kibongo kusikufanye uone sarakasi nyingine sio bora.

Huyu jaji kaonyesha uadilifu wake katika utumishi wa uma, ni wengi sana na narudia kusema kuwa ni maafisa wengi sana wa serikali hii hupewa fedha kwa namna hiyo na wao huishia kutumia kidogo na the rest... kona kubwa., ni kama hongo fulani hivi isiyorasmi,

Hii inanikumbusha kibosile mmoja mjeshi aliyepewa kitita cha kutengeneza nyumba yake na sasa hivi ukiiona ni kichekesho na pesa imeeisha, kwangu mie nafikiri jaji kaamua kupeleka salaam zake za mwisho kwamba viongozi wetu wanapaswa kuweka kando nafsi zao kwanza na kuangalia vipambele muhimu

Jaji mkuu aaelekea kustaafu nani atavaa viatu vyake? je ni wale wa jana? ambao wengine walitunyima haki mahakamaani?? au walee Yeboyebo walioshiriki kweenye Deep Green au EPA? au wale makanjanja waliosaidia kufunguua kagoda? au ni yule wakilii aliyekuwa anakula huku na kule?

Tukubali tusikubali Mahakama tu ndio nguzo iliyobaki nje ya mikono ya mafisadi (si Bunge wala Serikali) lakini kuna ubunifu mkubwa ambao unafanyika ili nayo iwe mikononi mwao na baada ya hapo mchezo ni kuuma meno,
 
Ingawa hatuwezi kujua nia ya Jaji augustino, lakini alichofanya ni kitendo cha hekima na heshima kubwa. Hongera sana Jaji Augustino. Cha kujiuliza wa TZ ni kuwa;
  1. Kwanini Jaji alipewa pesa nyingi kiasi hicho ingawa ni wazi kuwa hakuwa anazihitaji?
  2. Kwa nini Pinda hakushangazwa na mgao huo mbovu wa pesa ya umma, licha ya kushiriki ufunguzi wa jengo la mahakama?
  3. Ni nani aliyefanya huu mgawanyo wa pesa maana ingefaa aeleze ni kwa nini alimpatia Jaji pesa yote hiyo ikiwa haikuwa inahitajika?
  4. Je kuna uwezekano kuwa hii pesa ilikuwa na nia ya kumhonga/kumrubuni Jaji Augustine kwenye maamuzi atakayofanya?
  5. Ni nani mwenye uwezo wa kuiuliza serikali haya maswali? Wabunge? Vyama vya upinzani? Magazeti? Wanasubiri nini wasidadisi?
  6. Je sio vema kufanya uchunguzi wa hii miradi tata ya ukarabati ambayo kumbe mingi haihitajiki na iko kila idara kuliko tunavyohabarishwa?
  7. Ni lini serikali yetu/Bunge letu vitaweza kuchunguza na kutoa adhabu kwa wale wanaoihujumu nchi yetu?
 
Angalau Jaji Agustino Saidi (RIP) amekumbukwa. Huyu alipostaafu, alikwenda kuishi kwenye nyumba yake ya kawaida, Msasani Mikoroshini, nyuma ya flats za Drive -In with his Peogeot 404!.

Agustino Saidi ndie alikuwa Advocate wa kwanza mzawa Tanzania huru, kabla ya hapo walikuwa ni wazungu tuu.

He was totally Nyerere type mpaka kifo kilipomuita.

Ifuatayo ni just an amaizing Coincidence.

Yeye na Agustino Ramadhani, wanafafana kwa mengi.
1. Majina yao ya kwanza wote ni jina la Agustino.
2. Majina yao ya kwanza wote ni ya Kikristo
3. Majina yao ya pili wote ni ya Kiislamu, mmoja akiitwa Saidi, mwingine akiitwa Ramadhani.
4, Wote ni Wakristo wachaMungu, Agustino Saidi akihudumu St. Peters na familia yake yote, Agustino Ramadhani akihudumu na mpaka kupiga piano St. Albans.
5. Wote ni majaji Wakuu wa Tanzania wakihudumu chini ya maraisi wenye majina ya JK,
Jaji Saidi chini ya Julius Kambarage, Jaji Ramadhani chini ya Jakaya Kikwete.

Waaw!
Inatia moyo angalau kidogo kuona tz kuna anaejali japo kiduuchu!
 
Huyu Jaji hana makuu wala majivuno, ni mtu wa watu kwa hiyo hana tamaa ya utajiri. Alipo teuliwa kuwa Jaji wa Mahakama ya Rufaa, wakati ule Mahakama ilikuwa haina nyumba yeye na familia yake wakawa wanaishi katika Hoteli ya Kilimanjaro kwa muda.

Alipoambiwa kuwa kuna nyumba ya Mahakama inakaliwa na ofisa wa Mahakama na maeneo ya Oysterbay na wameamua kumhamisha ofisa yule ili nyumba ikarabatiwe kwa ajili yake na familia yake Jaji Augustine alikataa kitendo hicho ndipo alipoomba nyumba Jeshi la Wananchi kwa sababu wakati ule Alikuwa Brigadia Jenerali na kwa wadhifa wake jeshi likampatia nyumba, na yule ofisa akaendelea kuishi katika nyumba ile.

Watu kama hawa katika Uongozi wangepatikana kama 10 nchi ingekuwa mbali katika maendeleo.
 
Wengi kumbe hamumjui huyu Jaji Mkuu. Huyu ni mwanasiasa. Hapa anacheza politics kwa sababu ana malengo yake ya kisiasa baada ya kustaafu mwisho wa mwaka. Sintashangaa mweiz Aprili akitoa hukumu ya kuruhusu wagombea binafsi. He is from Zanzibar. One time in the past aliwahi kugombea Urais kama sikosei.

Acha porojo siyo lazima kila anyefanya jema basi ana malengo ya kisiasa!!
 
Ingawa hatuwezi kujua nia ya Jaji augustino, lakini alichofanya ni kitendo cha hekima na heshima kubwa. Hongera sana Jaji Augustino. Cha kujiuliza wa TZ ni kuwa;
  1. Kwanini Jaji alipewa pesa nyingi kiasi hicho ingawa ni wazi kuwa hakuwa anazihitaji?
  2. Kwa nini Pinda hakushangazwa na mgao huo mbovu wa pesa ya umma, licha ya kushiriki ufunguzi wa jengo la mahakama?
  3. Ni nani aliyefanya huu mgawanyo wa pesa maana ingefaa aeleze ni kwa nini alimpatia Jaji pesa yote hiyo ikiwa haikuwa inahitajika?
  4. Je kuna uwezekano kuwa hii pesa ilikuwa na nia ya kumhonga/kumrubuni Jaji Augustine kwenye maamuzi atakayofanya?
  5. Ni nani mwenye uwezo wa kuiuliza serikali haya maswali? Wabunge? Vyama vya upinzani? Magazeti? Wanasubiri nini wasidadisi?
  6. Je sio vema kufanya uchunguzi wa hii miradi tata ya ukarabati ambayo kumbe mingi haihitajiki na iko kila idara kuliko tunavyohabarishwa?
  7. Ni lini serikali yetu/Bunge letu vitaweza kuchunguza na kutoa adhabu kwa wale wanaoihujumu nchi yetu?

mbona haya maswali hukumuuliza Prof. Beno ndulu?
 
Back
Top Bottom