Jaji Mkuu agoma kujitoa kesi ya samaki 'wa Magufuli'

Rutashubanyuma

JF-Expert Member
Sep 24, 2010
215,419
2,000
Jaji Mkuu agoma kujitoa kesi ya samaki 'wa Magufuli' Thursday, 16 December 2010 20:39

James Magai
JAJI Mkuu wa Tanzaia, Agustino Ramadhan, amepuuza maombi ya Serikali ya kumtaka ajiondoe katika jopo la majaji wanaosikiliza maombi ya dhamana ya washtakiwa katika kesi ya uvuvi haramu, katika Ukanda wa Bahari Kuu wa Tanzania.

Jaji Ramadhan, alitoa msimamo huo jana wakati kesi hiyo inayowakabili raia wa mataifa matano ya nje, ilipofikishwa mahakamani kwa ajili ya kusikilizwa rufaa ya kupinga masharti ya dhamana ya washtakiwa hao.
Rufaa hiyo ya kupinga masharti ya dhamana kwa washtakiwa,ilifunguliwa Desemba 8 mwaka huu na jopo la mawakili wa washtakiwa hao, linaloongozwa na wakili Kapteni Ibrahimu Bendera, akisaidiwa na John Mapinduzi.

Katika maombi yao, mawakili hao wanaiomba mahakama hiyo, itangue uamuzi uliotolewa na Jaji Njengafibili Mwaikugile, kuhusu masharti ya dhamana.
Masharti hayo ni pamoja na kuwataka washtakiwa watoe mahakamani kiasi cha Sh1.37bilioni kila mmoja na kuwa na wadhamini wawili.

Kabla ya kuanza kusikilizwa kwa rufaa hiyo iliyofikishwa mbele ya jopo la majaji watatu wa Mahakama ya Rufani, lililoongozwa na Jaji Mkuu akisaidiwa na majaji Mbarouk Mbarouk na Othman Chande, upande wa serikali ulitoa hoja ya awali ya kumtaka Jaji Agustino ajiondoe katika kesi hiyo.

Wakili Mkuu wa Serikali Boniface Stanslaus, alisema hawana imani na Jaji Mkuu kwa kuwa aliwahi kutoa kauli iliyoonyesha kuwa ana maslahi katika kesi hiyo na kwamba kwa msingi huo, hatatenda haki.
Stanslaus alikuwa akirejea hotuba ya Jaji Mkuu ya Mei 25 mwaka huu kwa Waziri wa Katika na Katiba, Mathias Chikawe, wakati wa ufunguzi wa semina ya majaji mjini Arusha.

Katika hotuba hiyo, Jaji Mkuu aliwatetea washtakiwa hao kuwa kisheria hawakupaswa kushtakiwa wote bali nahodha wa meli yao waliyokuwa wakifanyia shughuli za uvuvi na kwamba wameshtakiwa kimakosa.
Pia Jaji Mkuu alizungumzia uamuzi wa Mahakama Kuu ya Tanzania, kuhusu masharti ya dhamana kuwa haikuwa haki.
Hata hivyo Jaji Mkuu alipuuza hoja hizo za serikali za kumtaka ajitoe katika kesi hiyo na kwamba hawezi kujiondoa kwa kuwa hoja za serikali hazina msingi.

Kabla ya kutoa msimamo wake huo, Jaji Ramadhan alimtaka Wakili Stanslaus asome mwongozo wa uendeshaji wa shughuli za mahakama.
Mwongozo huo unabainisha kuwa Jaji Mkuu anaruhusiwa kutoa mwongozo au maelekezo kwa maofisa wake katika kutekeleza majukumu yake.
Kwa mantiki ya mwongozo huo Jaji Mkuu alisema kuwa alichokifanya alikuwa akikifanya kama jaji mkuu ambaye ni kiongozi wa mhimili huo wa kusimimia utoaji wa haki.
Alimuliza wakili Boniface iwapo tangu atoe hotuba hiyo miezi saba iliyopita kuna athari zozote katika mwenendo wa kesi hiyo naye akajibu kuwa hakuna.

Akitoa uamuzi wake baada ya mjadala huo baina yake na mawakili hao wa serikali, Jaji Mkuu alisema kwa hoja hizo tu, hawezi kujitoa na kwamba sababu zaidi za kutokujitoa katika kesi hiyo atazitoa mwisho wa usikilizwaji wa rufaa hiyo kwenye hukumu yake.

Katika hatua nyingine upande wa serikali ulikiri kuwa Mahakama Kuu ilikosea katika hukumu yake kwa kuwaamuru washtakiwa hao kila mmoja atoe pesa taslimu Sh1.37 kwa ajili ya dhamana.
Baada ya kuigomea serikali kujiondoa katika kesi hiyo Jaji Ramadhan aliendelea na usikilizwaji wa rufaa hiyo hadi mwisho.

Katika hoja zao, mawakili wa upande wa utetezi walipinga masharti hayo na kuitaka mahakama
kutengua uamuzi wa masharti uliotolewa na Mahakama Kuu ya Tanzania.

Mawakili hao Kapteni Bendera na Mapinduzi walitoa maombi hayo mbele ya mahakama hiyo kwa madai kuwa kwa sasa meli iliyokamatwa ikidaiwa kutumiwa na watuhumiwa hao tayari iko mikononi mwa serikali na kwamba tayari samaki waliokamatwa katika meli hiyo walishagawiwa kwa wananchi.

Pia walisema kuwa hati ya mashtaka ya washtakiwa hao ilishabadilishwa na kwamba hati ya sasa haineshi kiwango cha pesa au hasara iliyosabibishwa.

Baada ya kusikilizwa kwa hoja za pande zote Jaji Mkuu aliahirisha kesi hiyo.
 

Rutashubanyuma

JF-Expert Member
Sep 24, 2010
215,419
2,000
Kabla ya kutoa msimamo wake huo, Jaji Ramadhan alimtaka Wakili Stanslaus asome mwongozo wa uendeshaji wa shughuli za mahakama.
Mwongozo huo unabainisha kuwa Jaji Mkuu anaruhusiwa kutoa mwongozo au maelekezo kwa maofisa wake katika kutekeleza majukumu yake.
Kwa mantiki ya mwongozo huo Jaji Mkuu alisema kuwa alichokifanya alikuwa akikifanya kama jaji mkuu ambaye ni kiongozi wa mhimili huo wa kusimimia utoaji wa haki.
Alimuliza wakili Boniface iwapo tangu atoe hotuba hiyo miezi saba iliyopita kuna athari zozote katika mwenendo wa kesi hiyo naye akajibu kuwa hakuna.

Hoja hizi za jaji Mkuu zina mapungufu kwa sababu utoaji wa miongozi kwa mahakama zizilopo chini hakumaanishi ya kuwa hiyo mionogozo aweza kutiota kwa Waziri wa katiba........................miongozo hiyo huwa ni katika magazeti ya serikali au maagizo ya kimaandishi kwa wananahaki lakini siyo kujadili haki za wadai kwa wanasiasa.......................kwa kufanya hivyo Jaji Mkuu alikuwa anamlalamikia Wazri wa Sheria ambaye hana mchango wowote wa moja kwa moja katika uendeshaji wa kesi...................
 

TIMING

JF-Expert Member
Apr 12, 2008
22,613
2,000
Jaji mkuu hapo labda ana maslahi binafsi

sijui atapungukiwa na nini akitoka

keshavuruga kanisa la Anglican zanzibar, sasa anataka kuvuruga hadi kesi ya samaki... dhambi inaambukiza na kuenea kama saratani
 

Rutashubanyuma

JF-Expert Member
Sep 24, 2010
215,419
2,000
Mwalusako: Niombeni radhi


*Atoa siku saba, vinginevyo...

Na Elizabeth Mayemba
SAKATA la ufujaji wa fedha za usajili sh.milioni 100, zilizotolewa na mdhamini Mkuu wa klabu ya Yanga, Yusuf Manji, limezidi kuchukua sura mpya, baada ya Katibu Mkuu wa klabu hiyo Lawrence Mwalusako kutaka aombwe radhi ndani ya
siku saba.

Kauli kama hiyo ilikuwa ikitolewa na Mwenyekiti wa Chama cha Tanzania Labour Party, Augustino Mrema wakati akiwa Waziri wa Mambo ya Ndani miaka ya 90.

Hivi karibuni kuna habari zilizoenea kwamba, uongozi wa Yanga kupitia kwa Katibu Mkuu, Mwalusako, ulichukua sh. milioni 100, kutoka kwa Manji, kwa ajili ya usajili wa dirisha dogo, hali inayodaiwa kuwa, zimetumika vibaya, na hivyo zitolewe ufafanuzi wa matumizi yake.

Akizungumza Dar es Salaam jana, Katibu Mkuu wa klabu hiyo, Mwalusako alisema habari hizo zimelenga kumchafua mbele ya wana-Yanga wote, jamaa zake na familia yake, hivyo ametaka aombwe radhi ndani ya siku saba, vinginevyo ataenda mahakamani na kudai fidia ya sh.milioni 150.

"Hata siku moja siwezi kutumia fedha za klabu yangu kwa matumizi yangu binafsi, na taarifa za kusema kwamba, nimefuja fedha hizo, zimenidhalilisha sana, nataka kuombwa radhi ndani ya siku saba, vinginevyo naenda mahakamani," alisema Mwalusako.

Akitoa ufafanuzi wa fedha hizo, Mwalusako alisema ni kweli alipokea hundi ya sh.milioni 100, kutoka kwa mdhamini wao kwa ajili ya usajili, ambapo mahesabu yao yalikuwa ni kusajili wachezaji watatu.Alisema katika fedha hizo, sh.milioni 25 walitumia kusajili wachezaji wao wawili, Mzambia Davies Mwape na Juma Seif 'Kijiko' wa JKT Ruvu.

Mwalusako alizidi kufafanua kwamba, kuna hundi ya sh.milioni 40 ambayo aliionesha kwa waandishi wa habari kwamba, haijatumika na sh.milioni 35 zipo katika akaunti ya klabu yao.

Alisema huo ndio ufafanuzi wa kiasi hicho cha fedha na kuwataka wanachama wote ambao nao walitaka kujua matumizi hayo, kujua ufafanuzi huo alioutoa ili kuondoa msemo wa kwamba, fedha hizo amezitafuna.
 

Rutashubanyuma

JF-Expert Member
Sep 24, 2010
215,419
2,000
Jaji mkuu hapo labda ana maslahi binafsi

sijui atapungukiwa na nini akitoka

keshavuruga kanisa la Anglican zanzibar, sasa anataka kuvuruga hadi kesi ya samaki... dhambi inaambukiza na kuenea kama saratani

Hoja hizi ni za kimsingi.......................Jaji Mkuu nastaafu tarehe 27th December 2010.................Sasa hizi kesi ni za nini.....................nilifikiria huu ni wakati wa kutuaga badala ya kuendekeza malumbano yasiyo na tija kwake mwenyewe na kwa taifa................

Kesi ya mgombea binafsi ndiyo ilimtoa kwenye chati kabisa na kamwe hata afanyaje hawezi kuwa kiongozi atakayekumbukwa hapa nchini.....................
 

Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Top Bottom