Jaji Mkuu aeleza sababu za 'kujitoa' kesi ya Lema

Kitwange

Member
Apr 10, 2011
47
125
Jaji Mkuu: Siku ya kesi ya Lema nitakuwa nje ya nchi, sijajitoa

JAJI Mkuu, Mohamed Chande Othman ameeleza sababu za kutokuwa kwenye jopo la majaji waliopangwa kusikiliza kesi ya aliyekuwa mbunge wa Chadema mkoani Arusha, Godbless Lema.

Jaji mkuu, alitoa maelezo haya jana alipozungumza na gazeti hili katika mahojiano maalumu kwenye mahafali ya 12 ya Chuo cha Uongozi wa Mahakama Lushoto (IJA).

"Ngoja nitolee ufafanuzi suala hilo ili jamii itambue utaratibu wa uendeshaji wa Mahakama ya Rufani, ambayo ina majaji 16 nchini," alisema Jaji Othman.

Jaji Othman alisema kimsingi hajajitoa kushughulikia kesi hiyo, ila siku ambayo kesi hiyo inatajwa, atakuwa nchini India kuhudhuria Mkutano Mkuu wa 13 wa Majaji Wakuu Duniani.

Maelezo hayo ya Jaji Chande yamekuja siku tatu baada ya gazeti hili kuripoti kuwa, mkuu huyo wa mhimili wa Mahakama nchini amejitoa kusikiliza kesi hiyo na nafasi yake imechukuliwa na Jaji Bernard Luanda.

"Kwanza ifahamike kwamba, jaji wa Mahakama ya rufani hana ubia na kesi yoyote kwa mujibu wa utaratibu. Jaji yeyote kati ya majaji 16 wa mahakama ya rufani nchini ana mamlaka ya kusikiliza kesi yoyote ya rufani," alieleza Jaji Othman.

Jaji Othman alifafanua kuwa, rufani ya Lema ni miongoni mwa kesi tatu za uchaguzi zilizobaki ambazo kwa mujibu wa taratibu za kisheria, huanza kusikilizwa baada ya muda wa mwaka mmoja na hukumu yake ni lazima itolewe ndani ya mwaka mmoja tangu kuanza kwake.

"Hivyo basi, kwa vile Jaji yeyote wa Mahakama ya Rufaa anaweza kuisikiliza kesi hiyo, hakukuwa na sababu inisubiri mimi," alisema.

Jaji Othman alitaja kesi nyingine za uchaguzi zitakazoanza kufanyiwa vikao vya rufani na jopo la majaji wa Mahakama ya Rufani kuwa, ni ile ya Jimbo la Ubungo kati ya Hawa Ng'umbi na John Mnyika ambayo itakuwa chini ya jopo la majaji watatu; Jaji Nathalia Kimaro, Jaji Salum, Salum Masati na Jaji Katherine Oriyo.

Nyingine ni ya Jimbo la Ilemela ya Yusuph Yussuph Masengela Lupilya na wenzake wawili dhidi ya Highness Kiwia na wenzake wawili, ambayo itakuwa chini ya jopo la Majaji Januari Msofe, Jaji Beard Luanda na Jaji Salum Massati.

Alisema rufani ya Lema haijaanza kusikilizwa kwa jaji yeyote, hivyo yeye asingeweza kujitoa kwa kuwa hajapangiwa.

"Kinachotatiza hapa ni kwamba, watu wanaifungamanisha rufani hii na ile ya Arusha ambayo mimi nilikuwa miongoni mwa jopo la majaji kama mwenyekiti.

Source: Mwananchi

 

pembe

JF-Expert Member
Nov 4, 2010
2,091
2,000
Mazito haya. Huu mhimili utoe haki mapema kwani kila kitu kiko wazi.. vuta vuta ya nini? haki huwa haibadiliki!
 

CHUAKACHARA

JF-Expert Member
Jun 3, 2011
12,366
2,000
Kitwange Fine, haki nadhani imebaki CA! huko uwezekano wa kutoa hukumu ya haki ni over 99%.
 
Last edited by a moderator:

Crashwise

JF-Expert Member
Oct 23, 2007
22,230
2,000
Mazito haya. Huu mhimili utoe haki mapema kwani kila kitu kiko wazi.. vuta vuta ya nini? haki huwa haibadiliki!

Kweli kabisa tena wanataka kusema mwaka mmoja ipite ndiyo watoe maamuzi kweli???!!!
 

Crashwise

JF-Expert Member
Oct 23, 2007
22,230
2,000
Ameogopa shinikizo la JK!

Haki ya Lema ipo sema wanaichelewesha tuu jk anaweza kufundisha mahakama ndogo kazi lakini siyo mahakama ya rufani hata wakimvua ubunge Lema anaruhusiwa kugombania tena na kwa wana wa Arusha atashinda tena kwa kura nyingi kuliko zile za mwanzo maana utukufu wa mwisho ni mkubwa sana kuliko utukufu wa mwanzo
 

Ndallo

JF-Expert Member
Oct 1, 2010
7,623
2,000
Jaji Othman alifafanua kuwa, rufani ya Lema ni miongoni mwa kesi tatu za uchaguzi zilizobaki ambazo kwa mujibu wa taratibu za kisheria, huanza kusikilizwa baada ya muda wa mwaka mmoja na hukumu yake ni lazima itolewe ndani ya mwaka mmoja tangu kuanza kwake.

Na kwanini iwe ndani ya mwaka mmoja? Katiba mpya ijayo iangalie hili swala!
 

Mwita Maranya

JF-Expert Member
Jul 1, 2008
10,565
2,000
Naona Jaji Salum Masati amepangwa kuwa katika majopo yote matatu ya rufaa. Rufaa ya Hawa Ngh'umbi Vs Jonh Mnyika (Ubungo), Rufaa ya Yusuph Yusuph Vs Haines Kiwia (Ilemela) na Rufaa ya Godbless Lema Vs Musa Mkanga na wenzake.
Kuna nini cha ziada hadi aonekane lulu kiasi hiki?
Personally ninamkubali Jaji Masati lakini kitendo cha kuteuliwa kuwa katika majopo ya rufaa zote tatu za uchaguzi linaleta aina fulani ya mvuto kama si kuzua tashwishwi ya kutaka kujua siri ya hizi teuzi!
 

Lambardi

JF-Expert Member
Feb 7, 2008
12,814
2,000
Ni kweli nami nimeshangaa kama kuna majaji 16 ila mmoja ametokea kesi zote 3 tena kwa muda mfupi mfupi inaonekana kuna mushkeri sehemu fulani katika labda kurekebisha mambo kwa matakwa ya mtu fulani!!kwa nini Jaji Masati awemo mara zote?labda hii nalo alitolee ufafanuzi!ingawa mhimili wa mahakama umetingishwa sana na wameshindwa kujitetea wananchi hatuwaelewi kabisa kuna madudu mengi sana pale!
 

Bobuk

JF-Expert Member
Oct 8, 2010
5,870
1,500
Nashangaa waandishi/wanahabari wa Bongo kwanini hawawi wachokonozi? (inquisitive)
  1. Kwanini kwanza hawakumchokonoa/kuuliza kuhudsu kudanganya umri wake?
  2. Kwanini pia hawajamuuliza kama majudge wa mahakama ya rufani wako 16 kwanini Judge Salum Masati atokee kwenye jopo la kesi zote tatu?

Hivi tutawafundisha kazi hadi lini? No wonder Mkapa aliwaita MAKANJANJA!
 

Mwanaweja

JF-Expert Member
Feb 8, 2011
3,575
1,195
huyu kaongopa kuaibika maana siku lema akishinda majaji wa kwanza watadharaulika sana
 

Arafat

JF-Expert Member
Nov 17, 2009
2,582
2,000
Hakuna kitu kinaitwa Muhimili wa Mahakama hapa Tanzania wala hakuna haja ya kuwepo hicho kitu kabisa.
Eti Rais anamteuwa Jaji?! Uwiano wa hiyo mihimili upo wapi? Mbona hatuoni Jaji Mkuu akipewa stahili sawa kama Rais iwapo wote ni viongozi wa mihimili iliyo sawa? Mbona Jaji Mkuu hatokani na Wananchni kama hii Mihimili ipo sawa? Ukweli ni kuwa kuna Muhimili ulio juu ya mingine nayo ni ile inayo ongozwa na Rais, ipo juu ya huo fake wa Mahakama na ule uliosinzia wa Bunge.
 

KV LONDON

JF-Expert Member
Jul 18, 2012
903
225
Lakini akiulizwa baada ya hukumu siatasema hakuhusika? Chande acha kutuchezea akili zetu'
 

JIULIZE KWANZA

JF-Expert Member
Nov 6, 2010
2,569
0
Hawana weledi na elimu zap za kuunga unga wana mu interview mtu Hana ata quesioner note. Hawajiamini as if sio mwandishi ndio maana mkapa akawaita makanjanja wanatema na kumeza maneno kisa Bahasha na ukiona ivi ujue mwandishi ndio aliitwa aje kujenga mazingira their all fake dude


Nashangaa waandishi/wanahabari wa Bongo kwanini hawawi wachokonozi? (inquisitive)
  1. Kwanini kwanza hawakumchokonoa/kuuliza kuhudsu kudanganya umri wake?
  2. Kwanini pia hawajamuuliza kama majudge wa mahakama ya rufani wako 16 kwanini Judge Salum Masati atokee kwenye jopo la kesi zote tatu?

Hivi tutawafundisha kazi hadi lini? No wonder Mkapa aliwaita MAKANJANJA!
 

JIULIZE KWANZA

JF-Expert Member
Nov 6, 2010
2,569
0
Inatakiwa ktk kesi zote 3 basi 1 atende haki na 2 apindishe haki ili mkihoji Kulikoni nae ahoji Kulikoni. Atapima upepo kupindisha au kunyoosha hukumu aone hasira zenu au awapumbaze ili msihoji amini nakwambia ndicho walichoambiwa na Mkuu. Uwepo wa majaji 16 na ikawa yeye anasimamia kesi 3 tena za kisiasa kuna maswali mengi ya kujiuliza.

Ni mtazamo tuu MkuuNaona Jaji Salum Masati amepangwa kuwa katika majopo yote matatu ya rufaa. Rufaa ya Hawa Ngh'umbi Vs Jonh Mnyika (Ubungo), Rufaa ya Yusuph Yusuph Vs Haines Kiwia (Ilemela) na Rufaa ya Godbless Lema Vs Musa Mkanga na wenzake.
Kuna nini cha ziada hadi aonekane lulu kiasi hiki?
Personally ninamkubali Jaji Masati lakini kitendo cha kuteuliwa kuwa katika majopo ya rufaa zote tatu za uchaguzi linaleta aina fulani ya mvuto kama si kuzua tashwishwi ya kutaka kujua siri ya hizi teuzi!
 

hoyce

JF-Expert Member
Oct 26, 2010
1,117
1,195
Nashangaa
waandishi/wanahabari wa Bongo kwanini hawawi wachokonozi? (inquisitive)
  1. Kwanini kwanza hawakumchokonoa/kuuliza kuhudsu kudanganya umri wake?
  2. Kwanini pia hawajamuuliza kama majudge wa mahakama ya rufani wako 16
    kwanini Judge Salum Masati atokee kwenye jopo la kesi zote tatu?

Hivi tutawafundisha kazi hadi lini? No wonder Mkapa aliwaita
MAKANJANJA!
Kwani hayo waliyouliza uliwatuma wewe? Jiulize kama wewe uko kamili katika eneo lako, usiishie kukosoa maeneo ya wengine
 

hoyce

JF-Expert Member
Oct 26, 2010
1,117
1,195
mbona wewe hujajiuliza, hayo yote waliyokuletea huo weledi wamepata wapi. Jiulize, mbona kwenye research zenu mnakwenda na dodoso na bado mnapika results na conclusion
Hawana weledi na
elimu zap za kuunga unga wana mu interview mtu Hana ata quesioner note.
Hawajiamini as if sio mwandishi ndio maana mkapa akawaita makanjanja
wanatema na kumeza maneno kisa Bahasha na ukiona ivi ujue mwandishi ndio
aliitwa aje kujenga mazingira their all fake dude
 

Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Top Bottom