Maoni kama haya kutoka kwa watu wanaoheshimika katika jamii yanasaidia kuondoa wasiwasi kwa wananchi juu ya upinzani kama inavyo chakanuliwa na mafisadi wenye wivu wa kuona wenzao wana elimika na kupata ufahamu juu ya ukweli wa mambo yanavyotakiwa kuwa.
Inawezekana Serikali kutoa huduma za afya bure- Jaji Mfalila
· Ashangaa wanasiasa wanaodai haiwezekani
Na Charles Lucas
22 September 2010
JAJI mstaafu wa Mahakama Kuu ya Tanzania, Lameck Mfalila amesema inawezekana serikali kutoa huduma za afya bure endapo wanasiasa watakuwa na dhamira ya kweli kutekeleza jambo hilo.
Akizungumza wakati wa uzinduzi wa Tamko la Wanaharakati Wasio wa Kiserikali kuhusu Uchaguzi Mkuu, jijini Dar es Salaam jana Jaji Mfalila aliwaponda baadhi ya wanasiasa wanaowabeza wenzao kwa maelezo kwamba haiwezekani serikali kutoa huduma za afya bila malipo na kuwataka kuacha kupinga jambo hilo.
Alisema Tanzania ina rasilimali za kutosha yakiwemo madini ya kila aina na mengine hayapatikani sehemu yoyote duniani hivyo ni wajibu wa serikali kuyatumia vizuri ili yagharamie huduma zingine.
"Nimesikia sikia mgombea mmoja wa chama kimoja cha siasa ametamka kuwa atatoa huduma za afya bure kwa Watanzania, asibezwe hilo linawezekana ikiwa maadili ya matumizi ya rasilimali za taifa yatazingatia," alisema Jaji Mfalila na kuongeza; "Wanakojeli kauli hizo wana mapungufu ya uongozi au hawana ufahamu," alisema Jaji Mfalila huku akishangiliwa kwa mguvu na washiriki wa mkutano huo.
"Kama zipo ahadi nyingi zinazotolewa na zinatekelezeka kwanini hii moja ya kutoa huduma bure isitekelezeke?" Alihoji.
Alisema inasikitisha kwamba baadhi ya viongozi wanaopinga jambo hilo alisoma nao kuanzia hadi chuo kikuu na walipewa huduma zote bure kuanzia matibabu hadi elimu lakini leo wanapinga jambo hilo kuwa haliwezekani.
Aliendelea kusema Tanzania haistahili kuwa na njaa kutokana na rasilimali kubwa ya mabonde ya kilimo yenye rutuba yanayoweza kuzalisha chakula cha kutosha kwa wananchi wake.
"Mfano Japan ina ardhi ndogo inayofaa kwa kilimo ukilinganisha na Tanzania, ni aibu kwenda kuomba chakula wakati tuna mabonde yenye rutuba ya kuweza kuzalisha vyakula kama Rufiji."
Jaji Mfalila alisema kiongozi hatakiwi kuhamasisha wananchi kwamba misaada ndio majibu ya matatizo yao bali anapaswa kutengeneza mipango na kuwahamasisha kujenga mazingira ya kuwafanywa wajione wana wajibu wa kuwajibika kwa maendeleo ya taifa lao.
"Kitendo cha kuweka mawazo kwenye misaada kinaondoa fikra za kujiamini kwamba sisi wenyewe tunaweza kujitegemea bila kuomba," alisema.
Alisema uchumi wa nchi hauwezi kukua kama hakuna hazina ya kutosha ya madini ndani ya Benki Kuu na kulaumu mtindo wa serikali kupokea mrahaba wa asilimia tatu jambo linaloonesha wazi kunyonywa na wawekezaji.
"Kuna wakati, Bw. Mrema (Augustino) alipokuwa Waziri wa Mambo ya Ndani na Naibu Waziri Mkuu, alichukua jukumu la kununua dhahabu na kuipeleka Benki Kuu, alikusanya kilo 16. Nashangaa kwanini serikali iliondoa utaratibu huo. Ingekuwa afadhali kama katika kila kilo 100 anazochimba mwekezaji serikali ipate walau kilo moja."
Alifafanua kuwa nchi inapokuwa na akiba ya dhahabu, uchumi wake unakuwa mzuri lakini inasikitisha kwamba pamoja na madini hayo hatuna akiba ya kutosha na tunaishia kupata mrahaba wa asilimia tatu ambao si chochote.
Alisema kitendo hicho kimewapa nafasi baadhi ya wawekezaji ambao si waaminifu wanaotumia udhaifu wa mikataba iliyopo kujinufaisha wenyewe na kunukuu kauli ya Mwalimu Nyerere kuonya kupokea ushauri usio na maana.
"Mwalimu alisema mtu mjinga akikushauri jambo la kijinga na wewe ukalikubali wewe utakuwa mjinga zaidi," alisema Jaji Mfalila na kuwataka viongozi wawe makini wanapopewa ushauri.
Akizungumzia Uchaguzi Mkuu alisema unatoa nafasi adhimu kwa wapiga kura na wagombea kukumbuka malengo ya misingi ya mfumo wa uchaguzi ni kuweka mbele na kulinda maslahi ya taifa.
Alisema kunatakiwa kuwepo mchakato wa uchaguzi wenye uwazi haki na amani unaopinga aina zote za vitisho, rushwa, mizengwe au hila za kupindisha ushindi utokanao na kura halali za wananchi na uzingatia misingi ya kidemokrasia.
Alisema Tanzania inayotakiwa kuwa taifa lenye amani na maendeleo ambalo linaheshimu haki za wananchi wake bila kujali jinsia, hadhi, dini, kabila, imani ya kundi fulani na uwezo kimwili ama kiuchumi.
"Tunataka Tanzania ambayo licha ya kutokuwa na wala rushwa inaendeshwa na viongozi wenye uvumilivu na uadilifu wenye kutumia ipasavyo maliasili na rasilimali hususani watu.
"Tunataka Tanzania inayojitosheleza kwa chakula miundombinu bora yenye misingi ya kiteknolojia na yenye kutafsiri maendeleo ya kitaifa kwa kuangalia afya, elimu, na ustawi wa jamii. Tunaomba wananchi wayasimamie haya na kuyafautilia kwa sababu Tanzania tunayoitaka inawezekana," alisema Jaji Mfalila.