Jaji Mfalila: Chagueni upinzani ASEMA MGOMBEA ATAYETOA ELIMU, AFYA BURE NDIYE ANAFAA | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Jaji Mfalila: Chagueni upinzani ASEMA MGOMBEA ATAYETOA ELIMU, AFYA BURE NDIYE ANAFAA

Discussion in 'Uchaguzi Tanzania' started by MziziMkavu, Sep 22, 2010.

 1. MziziMkavu

  MziziMkavu JF-Expert Member

  #1
  Sep 22, 2010
  Joined: Feb 3, 2009
  Messages: 39,620
  Likes Received: 4,616
  Trophy Points: 280
  [​IMG]
  JAJI mstaafu wa Mahakama ya Rufaa nchini, Lameck Mfalila

  Patricia Kimelemeta

  JAJI mstaafu wa Mahakama ya Rufaa nchini, Lameck Mfalila, amewataka Watanzania kuchagua mgombea aliyethubutu kusema; "atasomesha wanafunzi na kutoa huduma ya afya bure." Akitetea msimamo huo, Jaji Mfalila alisema:"Huyu ni shujaa, sio ghilba bali amethubutu kusema anaweza kufanya mabadiliko hayo, mchagueni."

  Katika mkutano wa wanaharakati kuhusiana na Uchaguzi Mkuu jijini Dar es Salaam jana, Jaji Mfalila alitoa sifa kwa mgombea mmojawapo wa urais kutoka kambi ya upinzani ambaye ameweka wazi kwamba akiingia Ikulu, elimu na afya zitatolewa bure.


  "Kuna mgombea mmoja kutoka kwenye vyama vya upinzani, naona anaitia changamoto serikali, yeye alithubutu kusema ikiwa atachaguliwa kuingia Ikulu, atasomesha wanafunzi na kutoa huduma ya afya bure, huyu ni shujaa, sio ghilba bali amethubutu kusema anaweza kufanya mabadiliko hayo, mchagueni," alisisitiza.


  Kwa mujibu wa Jaji Mfalila, ikiwa wananchi watafanya mabadiliko hayo wataweza kupata kiongozi bora atayesimamia mali asili za nchi yake vizuri.


  Ingawa hakumtaja mgombea huyo, lakini wagombea urais kwa tiketi ya Chadema, Dk Willibrod Slaa na wa CUF, Prof Ibrahim Lipumba ndiyo ambao wamekuwa wakitoa ahadi hiyo ya kutoa elimu na afya bure kama wakishinda uchaguzi.


  Kwa upande wa Dk Slaa, amekuwa akisema iwapo Chadema itapewa ridhaa ya kuongoza nchi, fedha zilizoporwa kifisadi zitarejeshwa na kuwa mwanzo wa kutoa elimu na afya bure kwa wananchi.


  Ahadi yake hiyo ilimsababishia Dk Slaa kuingia katika mgogoro na Spika wa Bunge aliyemaliza muda wake, Samuel Sitta, aliyepinga sera ya wapinzani ya kutoa elimu bure akisema kuwa haiwezekani.


  Naye Prof Lipumba mara kadhaa amenukuliwa akisema kama akichaguliwa kuwa rais katika Uchaguzi Mkuu wa mwaka huu, Serikali yake itaondoa gharama za elimu katika ngazi zote.

  Lipumba alitoa kauli hiyo hivi karibuni wakati akijinadi katika mikutano tofauti ya kampeni iliyofanyika mkoani Lindi na Mtwara.

  Lipumba alisema CUF imeazimia kuweka suala la elimu ya bure katika vipaumbele vyake, kwa vile sekta hiyo ni mkombozi wa umaskini uliokithiri kwa wananchi wengi.


  Katika mkutano huo wa jana, Jaji Mfalila alisema Tanzania ina kampuni kubwa ambazo zinafanya shughuli za kuzalisha madini yakiwamo ya dhahabu na almasi, jambo ambalo lingeweza kuingiza kiasi kikubwa cha fedha, lakini kutokana na ujanja uliopo makampuni hayo yanalipa kiasi kidogo cha kodi huku yakiwanufaisha wachache.


  Jaji Mfalila ambaye alitumia zaidi ya saa moja kuitafakari serikali, ilipotoka, ilipo sasa na inapokwenda, alisema kuwa rasilimali zilizopo zinatumika kiujanja ujanja jambo ambalo limesababisha nchi kutegemea misaada kutoka kwa wahisani na nchi marafiki.


  Alisema kutokana na hali hiyo, wananchi wanapaswa kufanya mabadiliko ya kumchagua kiongozi atakayeweza kuleta maendeleo kwenye taifa lake, hasa katika nafasi ya rais ambayo ndio injini ya maendeleo.


  "Tanzania bila ya misaada inawezekana, tuna rasilimali za kutosha ambazo zikitumika vizuri zinaweza kuleta mabadiliko ya kimaendeleo. Wananchi wanapaswa kufanya mabadiliko ya kumchagua kiongozi anayeweza kuthubutu kuleta maendeleo hayo, chagueni upinzani kwa ajili ya maendeleo," alisema Jaji Mfalila.


  Jaji Mfalila alisema nchi nyingi duniani zilizopiga hatua kimaendeleo zilitumia rasilimali zake vizuri bila ya kuingiza ujanja ujanja.


  Akizungumzia kilimo, Jaji Mfalila alisema kwamba inashangaza kilimo cha Tanzania mpaka sasa kinategemea mvua za misimu na pale ambapo mvua hizo hazinyeshi, viongozi wanaitana Ikulu kutafuta nchi ya kuomba msaada wa chakula wakati ardhi yenye rutuba ipo.


  "Hii ni aibu ya kutosha kuona tunaomba msaada wa chakula wakati tuna ardhi bora kwa ajili ya shughuli za kilimo, lakini bado tunasubiri mvua ya miezi mitatu ambapo isiponyesha viongozi wanaitana Ikulu kwa ajili ya kutafuta nchi ya kuomba msaada wa chakula, kweli tunahitaji mabadiliko," alisema.


  Akizungumzia enzi za uongozi wa Mwalimu Julius Nyerere, Jaji Mfalila alisema wanafunzi wa chuo kikuu waliweza kupatiwa mahitaji yote muhimu ili wasome kwa umakini zaidi, lakini siku hizi fedha za matibabu, chakula na kulipia gharama za ada zimekuwa tatizo kwao.

  "Nasikia tu wanafunzi wamegoma kwa ajili ya kukosa fedha za ada, chakula na matibabu wakati enzi zetu tulikuwa tunakabidhiwa hundi ya malipo kabla ya kufika shuleni,"alisema.

  Naye Profesa Chris Peter Maina, wa Shule ya Sheria ya Chuo Kikuu cha Dar es Salaam na Mwenyekiti wa Kituo cha Huduma ya Sheria Zanzibar, aliunga mkono kauli iliyotolewa na Jaji Mfalila akisisitiza kuwa elimu yaweza kutolewa bure.


  "Nimesoma bure kuanzia darasa la kwanza hadi nilipopata shahada yangu ya uzamili. Sharti kuu lililokuwapo ni kwamba nilihitajika kujaza fomu kuazimia kuwa nitalitumikia taifa langu baada ya kuhitimu masomo yangu," alisema Profesa huyo.Aliongeza: "Kama nisingepata elimu ya bure, leo hii ningelikuwa nachunga ng'ombe kijijini kwetu."


  Profesa Maina alisema tatizo kubwa linaloikabili Tanzania ni kwamba viongozi wamevigeuza vipaumbele juu chini kwa kuwapa wakaguzi wa elimu wanaotumia magari ya Sh 150milioni yaliyo na viyoyozi kazi ya kukagua madarasa yasiyo na madawati na yenye wanafunzi wanaoketi chini.


  "Sielewi ni kwanini mpaka leo miaka 50 baada ya uhuru wanafunzi wa Tanzania bado wanaketi chini kwenye madarasa yao?" alishangaa Profesa huyo wa sheria.


  Chanzo: Jaji Mfalila: Chagueni upinzani ASEMA MGOMBEA ATAYETOA ELIMU, AFYA BURE NDIYE ANAFAA KUWA RAIS

  Umesema kweli Mkuu Jaji mgombea anaweza kutowa elimu na afya bure anafaa kuwa Rais wetu nakupa hongera mkuu jaji Bravo.
   
 2. u

  urasa JF-Expert Member

  #2
  Sep 22, 2010
  Joined: Aug 12, 2010
  Messages: 435
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 0
  Safi sana mzee wetu kwa kuwa wazi na kuweka maslahi ya taifa mbele,wasomi wengine igene mfano wa jaji wetu,jitokezeni na mtoe kauli za kulikomboa taifa letu
   
 3. Saharavoice

  Saharavoice JF-Expert Member

  #3
  Sep 22, 2010
  Joined: Aug 30, 2007
  Messages: 2,644
  Likes Received: 131
  Trophy Points: 160
  Hii habari Chadema wanaweza kuitumia kama mtaji. zinunuliwe nakala nyingi za mwananchi zisambazwe kwenye mikutano ya kampeni zote za Chadema kuanzia udiwani hadi urais
   
 4. The Finest

  The Finest JF-Expert Member

  #4
  Sep 22, 2010
  Joined: Jul 14, 2010
  Messages: 21,709
  Likes Received: 43
  Trophy Points: 145
  Well said Jaji Mstaafu
   
 5. PhD

  PhD JF-Expert Member

  #5
  Sep 22, 2010
  Joined: Jul 15, 2009
  Messages: 3,819
  Likes Received: 818
  Trophy Points: 280
  karibu ndugu kinana ukanushe habari hii, au pia unaweza kuwaagiza vijana wako MS na TANDALE ONE kukanusha.
   
 6. Njowepo

  Njowepo JF-Expert Member

  #6
  Sep 22, 2010
  Joined: Feb 26, 2008
  Messages: 9,296
  Likes Received: 381
  Trophy Points: 180
  Jaji chonde chonde wasije wakakumaliza kwa shinikizo la damu na kisukali.
  Kwa tamkao ilo naomba uwe makini,mafisadi can do anything
   
 7. Mr. Zero

  Mr. Zero JF-Expert Member

  #7
  Sep 22, 2010
  Joined: Jun 5, 2007
  Messages: 9,504
  Likes Received: 2,744
  Trophy Points: 280
  Hawa ndiyo wazee makini tunaowahitaji. Siyo akina JM, PM, nk. Akina Warioba kama kweki bado wanaipenda nchi yao nao wajitokeze wazungumze.
   
 8. Smarter

  Smarter JF-Expert Member

  #8
  Sep 22, 2010
  Joined: Nov 10, 2008
  Messages: 455
  Likes Received: 5
  Trophy Points: 35
  Ukijua Kusoma halafu Usisome, Unatofauti gani na Asiyejua Kusoma?

  Wengi tu Wanajua na Wanakubali kwamba yanawezekana, Pole kwa wanaojua na kutunza tumboni, Pamoja Tutafika, Sema hapana kwa wapinga UKWELI.
  :playball:
   
 9. M

  Mdondoaji JF-Expert Member

  #9
  Sep 22, 2010
  Joined: Mar 17, 2009
  Messages: 5,106
  Likes Received: 45
  Trophy Points: 145
  Niliisoma hii habari asubuhi nikasisimuka na kuanza kujiuliza maswali mengi kwanza kilichonisisimua ni kwamba Jaji mstaafu wa mahakama ya rufaa ni mtu very influential katika serikali akatoa tamko la kuipigilia msumari serikali inayomlipa marupurupu ya pensheni ni ujasiri wa hali yajuu. Unlike others kama CJ Augustino wanaweka mbele maslahi ya matumbo halafu maslahi ya taifa baadae huu ni uzalendo wa hali ya juu. Pili ni jinsi professa maina alivyomalizia haingii akilini mie nisomeshwe bure na serikali halafu nikiingia serikali nifute ili misingi au system iliyonilea haingii akilini kabisa. Kama ina walakini kwanini usiiboreshe na sio kuiharibu kabisa. Leo hii kuanzia chekechekea mpaka form six ada ya shule ya mtoto katika shule makini inaweza kufika mpaka milioni na kitu sasa unadhani mtanzania wa kawaida atapata elimu bora kweli. Shule ya serikali tulizosoma utasikia elimu bure lakini michango ni lukuki, sekondari unasikia ada 70,000 mkulima atazitoa wapi? Nimefurahishwa sana na uzalendo wa hawa watu angalau wanatoa matumaini kwa watanzania.
   
 10. Mpambalyoto

  Mpambalyoto JF-Expert Member

  #10
  Sep 22, 2010
  Joined: Mar 26, 2010
  Messages: 752
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 0
  Mkuu naona akina MS, Tandale One and the company LTD nao wamechoka kupiga kelele hapa. Kasi inapungua kila kukicha, sijajua ni malipo au wamegundua kila wanachosema hakionekani kuleta mabadiliko labda tuseme wanajipanga upya kumalizia ngwe iliyobaki
   
 11. Gobret

  Gobret JF-Expert Member

  #11
  Sep 22, 2010
  Joined: Jun 11, 2010
  Messages: 320
  Likes Received: 10
  Trophy Points: 35
  Mwenyezi mungu akubariki sana. Akuongezee wingi wa rehema zake. Ili utuongoze utuonyeshe kweli yake tu. Naamini umesema kweli tu. Hata kama itv leo usiku watatoa majibu yasiyoendana na ukweli huu, huo utakuwa masimamo wa itv tu na wafanyakazi wake tu. Sisi watz tunaamini elimu na huduma ya afya inaweza kutolewa bure kama tutapata viongozi wenye hofu ya mungu. Tumchague dr slaa. Ashindwe mwenyewe kutimiza ahadi yake. Asante mzee wetu jaji mfalila. May god bless you.
   
 12. Jatropha

  Jatropha JF-Expert Member

  #12
  Sep 22, 2010
  Joined: Apr 9, 2009
  Messages: 1,152
  Likes Received: 144
  Trophy Points: 160


  kwa heshima ya waee hawa wawili waliomaua kuweka unafiki pembeni na kusema ukweli kwa mujibu wa Katiba yetu. Nawaomba watanzania

  wote waliosoma Shule za Msingi, Middle School, Secondary Schools na Vyuo Vikuu vya hapa nyumbani na nje ya nchi buree katika utwala wa Mwalimu Nyerere watupatie taarifa kidogo hali ilikuwaje wakati huo? Natambua Mwalimu Nyerer alikuwa akiheshimu sna Katiba ya Nchi, na Haki ya Kupata Elimu Katina inatamka

  Katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania ya mwaka 1977, Sehemu ya Tatu ya Kifungu ya cha 11 kinasema kuwa "serikali itafanya jitihada kuhakikisha kwamba watu wote wanapata fursa sawa na za kutosha kuwawezesha kupata elimu na mafunzo ya ufundi katika ngazi zote za shule na vyuo vinginevyo vya mafunzo".

  Naomba mtueleze yafuaatyao:-
  a) Mazingira ya shule, vyuo yalikuwaje?
  b) Mlikuwa mkisafiri kwa gharama za nani kutoka majumbani hadi mashuleni, vyuoni n.k?
  c) Mazingira ya mabweni, chakula katika hizo shule na vyuo vilikuwaje?

  Taarifa za aina hii zitachangia kuwapatia picha halisi vijana wetu walioko mashuleni na vyuoni kwa sasa, na hivyo kuwasaidia kupima kwa makini kama wanapata Haki zao za Kikatiba za Elimu hivi sasa.

  Hii ni muhimu sana, kwani CCM imewafanya watanzania wengi kuamini kuwa elimu duni inayotolewa hapa nchini tena katika mazingira duni sana ni hisani kutoka viongozi wa CCM na chama hicho na sio haki ya msingi ya Mtanzania kwa mujibu wa Katiba.
   
 13. Mantissa

  Mantissa JF-Expert Member

  #13
  Sep 22, 2010
  Joined: Jul 24, 2010
  Messages: 870
  Likes Received: 27
  Trophy Points: 45
  Hongera sana mzee Mfalila. Wewe ni msomi pekee na uliyelelewa ktk kipindi cha CCM miaka mingi iliyopita, amabaye umeona hiki kitu kizuri.

  Sasa Makamba, kinana , sitta au Kikwete mkanushe hili. Aibu zimewajaa tu, hamna lolote zaidi ya ufisadi.

  Watu fisadi ndo mtakaoichagua CCM ili muendelee na huo ufisadi wenu. Ila mwaka huu, hapatoshi kwenu mafisadi wahujumu nchi.
   
 14. k

  kanda2 JF-Expert Member

  #14
  Sep 22, 2010
  Joined: Apr 22, 2007
  Messages: 1,318
  Likes Received: 36
  Trophy Points: 145
  Mfalilla kafulia
   
 15. Saint Ivuga

  Saint Ivuga JF-Expert Member

  #15
  Sep 22, 2010
  Joined: Aug 21, 2008
  Messages: 39,469
  Likes Received: 19,854
  Trophy Points: 280
  itakuwa ni jambo la kushangaza kama kuna mtu ambaye hatampigia slaa kwenye ngazi ya urais. Jamani bahati haiji mara mbili this is our chance now. Hiviv jamani watu ambao wanataabika tuseme watanzania ambao % kumbwa ni maskini hawataki elimu bure?????in maana watu watampigia JK kura ili walipe ada za shule?? And then utapata faida gani baada ya kumpigia?? JK mda wake ushiasha hANA JiPYAAAA. Au kuna watu labda wanapenda kutaabika. JK ni mtanzania na DR Slaa ni mtanzania vilevile sasa kwa nn tusimpe slaa?? Amkeni nyie .
   
 16. dkims

  dkims Senior Member

  #16
  Sep 22, 2010
  Joined: Mar 25, 2010
  Messages: 148
  Likes Received: 3
  Trophy Points: 35
  Profesa Maina alisema tatizo kubwa linaloikabili Tanzania ni kwamba viongozi wamevigeuza vipaumbele juu chini kwa kuwapa wakaguzi wa elimu wanaotumia magari ya Sh 150milioni yaliyo na viyoyozi kazi ya kukagua madarasa yasiyo na madawati na yenye wanafunzi wanaoketi chini.

  hayo maneno yana maana sana,big up
   
 17. b

  bagamoyo JF-Expert Member

  #17
  Sep 22, 2010
  Joined: Jan 14, 2010
  Messages: 4,531
  Likes Received: 2,113
  Trophy Points: 280
  Haya sasa tunaona waliofaidika na sera ya elimu iliyo bure kwa wote kama Jaji L. Mfalila , Prof. Chris Maina Peter, Prof. Lipumba, Dakta Slaa wote wanaona 'ndiyo inawezekana elimu bure kwa wote'.

  Swali:
  1. Kwa nini mgombea Urais kwa CCM Mh. Dakta Jakaya Mrisho Kikwete anaona haiwezekani?
  2. Pia kwa Nini wagombea ubunge wa CCM waliosomeshwa buree kama Mustafa Mkulo, Basil Mramba, Bernard Membe, Dr. Nagu, Dr. Buriani, Dr. Mwakyembe, Prof. Mwandosya na wengine wote wa CCM wanasema haiwezekani ?
  3. Wagombea Udiwani wa CCM kwa nini wanaona elimu na huduma za afya haziwezi kuwa bure kwa wote?
   
 18. Henge

  Henge JF-Expert Member

  #18
  Sep 22, 2010
  Joined: May 14, 2009
  Messages: 6,765
  Likes Received: 78
  Trophy Points: 145
  Ongea kweli jaji ongea ujualo
   
 19. R

  Rugemeleza Verified User

  #19
  Sep 22, 2010
  Joined: Oct 26, 2009
  Messages: 668
  Likes Received: 5
  Trophy Points: 35
  Napongeza kauli hii ya Jaji Mfalila. Nafurahi kuona Mwenyezi Mungu amemrudishia afya kwani mwaka juzi alipata kiharusi na alikuwa na hali mbaya. Sasa hivi anaonekana yu mkakamavu na akili zake ni timamu na zilizojaa busara. Ninapenda kusema tena elimu na huduma ya afya bure ni haki ya kila mtu anayeishi nchini mwetu. Suala ambalo tunatakiwa kulijadili ni jinsi gani huduma hizo zitatolewa katika ubora wa hali ya juu na kuhakikisha hakuna ufujaji. Hivyo wale wanaosema haiwezekani ni watu wenye mtima gubi au mtima gutitu (roho mbaya) na wanatakiwa kubezwa na kusahauliwa kwani ni watu wanaowachukia wenzao. Raha yao ni kuona wengi wanateseka na kutopea katika lindi la umaskini, Waingereza huwaita watu hawa kuwa ni sadists.
   
 20. MwanaHaki

  MwanaHaki R I P

  #20
  Sep 22, 2010
  Joined: Oct 17, 2006
  Messages: 2,403
  Likes Received: 122
  Trophy Points: 145
  Watu wengi wanadhani kwamba mabadiliko yanaletwa na Upinzani. Hapana. Mabadiliko yanaletwa na wapiga kura, wananchi wenyewe.

  Uchaguzi Mkuu sio wa vyama. Ni uchaguzi unaofanywa na wananchi, walio au wasio wanachama wa vyama vya siasa.

  Binafsi nimependezwa na ushauri wa Jaji Mfalila kupendekeza CHADEMA ipigiwe kura kwa kuwa imetamka wazi kuwasomesha Watanzania bure. Huo ni mfano wa sera inayopaswa kuwekwa kwenye Ilani ya Uchaguzi. CCM hawawezi kufanya hivyo kwa kuwa HAWANA NIA hata kidogo. Wanatambua kwamba Watanzania wakisoma wataachana na umaskini, kwani elimu ni ufunguo wa maisha. CCM iko madarakani kwa kutegemea KUCHUMIA TUMBO kwa maskini. Maskini ndio mtaji wa CCM, wakiondoka, CCM kazi kwisha!

  Asante Jaji Mfalila kwa kuonesha njia. Wasipokusikiliza wewe, sijui watamsikiliza nani tena?

  -> Mwana wa Haki
   
Loading...