Jaji Mstaafu Mark Bomani akataa Tanzania kuitwa Tanzania Bara, ataka iitwe Tanganyika

Safi sana Jaji Boman, tunapenda viongozi wasiokuwa wanafiki kama wewe, eti serikali mbili za nini sasa! tuwe na serikali tatu, na Tanganyika yetu ijulikane hivyo
 
nyie mlikua mnawashwawashwa kuuchokonoa muungano hatimaye umekwisha vinjika! sasa mnaleta majina ya kinafiki eti "bara" ! hapa kuna Tanganyika na Zanzibar...sitaki unafiki wenu. CCM imeharibu mambo mengi sana katika kudhibiti CDM. Makubwa yaliyo wazi ni Umoja aliouacha Nyerere, na Udini ambao hata nani aje hatotatua! ......Labada Oman wawe circular state.
 
IBARA YA 1 YA RASIMU YA KATIBA YENYEWE
1.-(1) Jamhuri ya Muungano wa Tanzania ni Shirikisho lenye
mamlaka kamili ambayo imetokana na Muungano wa nchi mbili za
Jamhuri ya Tanganyika na Jamhuri ya Watu wa Zanzibar ambazo kabla
ya Hati za Makubaliano ya Muungano ya mwaka 1964 zilikuwa nchi
huru.



Hivyo ndivyo inavyosomeka rasimu yenyewe. Kama jina la Zanzibar limebaki, na kama nchi zote bado ni huru, kwanini jina la Tanganyika life?

senkiyuu veri machi !!!!!
 
Sijui kwa nini wanang'ang'ania kuliua jina letu zuri TANGANYIKA. Sijui wanataka kuipeleka wapi Mafia kwa kuharibu jina! Tanganyika is real name.
 
Kwani Bara maana yake nini....huu muungano ni kama haupo siku nyingi tu ila kuna watu wanaogopa kudondokewa na historia ya kuuvunja muungano...Tanganyika ni nchi yetu hata ikikataliwa sasa wataikubali baadae....nashangaa chama tena kamati yake kutoa tamko hawakubali serikali tatu nchi hii yenu wenyewe? acheni upumba..%^&*
 
Hiyo rasimu ina mapungufu kibao
1. Hiyo nchi ya Tanzania Bara haijawahi kutokea duniani na hakuna nchi imewahi kupata uhuru inaitwa hivyo
2. Hii rasimu inasema ikipitishwa na wananchi itakuwa katiba, haisemi isipopitishwa itakuwaje?
3. Kuna section inaongelea haki za raia na nyongine inaongelea haki za wanawake. Kwani wanawake sio raia? kama ni hivyo basi either wanfeweka na haki za wanaume au hiyo section isingekuwepo kabisa ili kuwepo na haki za raia tu. Wote wanawake na wanaume ni raia.
4. Hii ni rasimu yakatiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na ikipitishwa itakuwa katiba ya JMT yenye washirika wawili i.e. Tanganyika na Zanzibar. Itawezekana vipi kuwa na nchi isiyo na katiba (Tanganyika )ndani ya muungano ambapo JMT na Zanzibar zina katiba zao?
5. Rasimu inajichanganya yenyewe kwa kutumia jina TANGANYIKA kwenye kurasa za mwanzo na kule ndani nchi hiyo haitajwi bali inaonekana TANZANIA BARA
6. Hayo ni baadhi tu ya mapungufu mengi yaliyopo kwenye hii rasimu
 
Tupeni ghrama (figures) za serikali 2 na tatu kisha tuchambue na kupembua. Naona neno "mzigo/ghrama" linapigiwa upatu sana. Kwangu mimi kama ndio gharama ya kulipa ili tuwe na amani na maendeleo I will happily pay. Kumbuka "cheap is always more costly/expensive"
Mimi kwangu serikali mbili tosha ili mradi kero za kweli zirekebishwe kwa katiba. Wanaoratibu madai ya serikali 3 zenj hawana nia njema. Wanataka serikali ya tanganyika kama hatua ya kuvunja muungano. Sasa kwa nini tupoteze tena muda badala ya kutafuta maendeleo kwa kupigiwa kelele za kero ya muungano wakati wazenj wanawasikiliza wenye nia ya kuuvunja. Suluhisho la kweli ni kua na serikali moja au mbili vinginevyo muungano uvunjwe sasa.
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom