Jaji Mstaafu Mark Bomani akataa Tanzania kuitwa Tanzania Bara, ataka iitwe Tanganyika

BONGOLALA

JF-Expert Member
Sep 14, 2009
16,509
11,881
Jaji Mstaafu Mark Bomani amesema anaunga mkono rasimu ya Katiba kwa Serikali tatu ila amepinga kuiita Tanganyika kwa jina la Tanzania Bara,amesema mbona Zanzibar waitwa hivyo? Na sisi Tanzania visiwani?

Amehoji ni Kwanini Baadhi ya Watu wanaona Aibu kutumia Jina Tanganyika Badala ya Tanzania Bara.

Amesema kuwa Muundo wa Muungano wa Serikali tatu ndo Moarobaini Pekee kwa Kero Zote za Muungano.

Chanzo: ITV
 
Wana JF, Amani iwe nanyi.

Akiisifu Rasimu ya Katiba Mypa Kipengele cha Muungano wa Serikali tatu.
Mwanasheria Nguli Nchini na aliyewahi kuwa Mwanasheria Mkuu wa Serikali , Jaji Mstaafu Mark Bomani amesmea kuwa Halipendi Jina Tanzania Bara.
Amehoji ni Kwanini Baadhi ya Watu wanaona Aibu kutumia Jina Tanganyika Badala ya Tanzania Bara.
Amesema kuwa Muundo wa Muungano wa Serikali tatu ndo Moarobaini Pekee kwa Kero Zote za Muungano.

Source ITV Habari

My Take

Huu ni Muendelezo wa Wazee wetu wenye Heshima zilizotukuka kutuonesha kuwa, CCM ni janga la Kitaifa.
CCM Wako Tayari kuiuza Tanganyika kwa Zanzibar for the sake ya Kupinga Muundo wa Serikali Tatu.
Vynazo Kutoka Ndani ya CCM ambavyo vinachukizwa na Ubinafsi wa Viongozi wa Ngazi za juu ndani ya CCM.
Vinasema kuwa, CCM wamjeipanga kwenda Zanzibar ku Lobe Wanzaznibar wapinge Mfumo wa Serikali Tatu.
CCM Wameonesha kuwa wako Tayari kuteleza Matakwa yote ya Akina Jussa na Maalimu Seif katika Kutafuta Unngwaji Mkono Kwenye Kupinga Muundo wa Serkali Tatu.

Wa Tanganyika, Tushirikiane Kuitokomeza CCM
 
Safi kabisa Mr Jaji, tunawataka pia watu wengine wenye heshima kwenye jamii ya kitanganyika nao wawe wazi, siyo wanajificha nyuma ya ccm wanaojifanya eti wanataka serikali 2.
 
One of the best brains in the legal fraternity has called serikali tatu cause the best option is federal Republic which the zanzibari and ccm do not want.Chadema want majimbousm
 
duh,serekali 3 mzıgo bana

Tupeni ghrama (figures) za serikali 2 na tatu kisha tuchambue na kupembua. Naona neno "mzigo/ghrama" linapigiwa upatu sana. Kwangu mimi kama ndio gharama ya kulipa ili tuwe na amani na maendeleo I will happily pay. Kumbuka "cheap is always more costly/expensive"
 
duh,serekali 3 mzıgo bana
Hizi mbili zenyewe mzigo! Sasa hivi penyewe tuna Marais watano (5) ambapo waNNE (4) ni Wazanzibari.

  1. Rais wa Jamhuri wa Muungano
  2. Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano - (Zanzibar)
  3. Rais wa Zanzibar - (Zanzibar)
  4. Makamu wa Kwanza wa Rais - (Zanzibar)
  5. Makamu wa Pili wa Rais - (Zanzibar)
Haya Ongeza na Waziri Mkuu, Maspika wawili (Zanzibar & Muungano) + wengine wengi
.
 
Ndiyo tujiite watanganyika lakini hapana serikali tatu bwana mi binafsi pia naona mzigo tu serilikali tatu zote hizo za nini?
 
Hongera Mheshimiwa Mark, hayo ndiyo maoni ya wananchi.

Ila navyojua Mimi wananzibari wanataka Serikali Mbili Na Shirikisho (Muungano Wa Mkataba) Au vinginevyo Muungano uvunjike.

Wazanzibari wako sahihi. Muungano ni sawa na ndoa huwezi ukalazimisha ndoa hata Kama mke au mme unampenda kiasi gani. Ndoa haitadumu au Siku zote itakuwa na mgogoro!

Watanganyika wapeni uhuru wanzenu Wazanzibari wapumue
 
Ndiyo tujiite watanganyika lakini hapana serikali tatu bwana mi binafsi pia naona mzigo tu serilikali tatu zote hizo za nini?

Mzigo kivipi? Kuna rasilimali za kutosha kabisa. I want our Tanganyika back.

Sent from my BlackBerry 9860 using JamiiForums
 
Jaji Mstaafu Mark Bomani amesema anaunga mkono rasimu ya Katiba kwa serikali tatu ila amepinga kuiita Tanganyika kwa jina la tanzania bara,amesema mbona Zanzibar waitwa hivyo?na siii tanzania visiwani?source ITV
Kama visiwa ni kigezo Mbona huku kuna visiwa vya mafia ukerewe nk huku paitwa Tanzania na kule paitwa Zanzibar kwani baba wa muungano ni Bara na endapo mungano utakufa jina la Tanzania litabaki kwa baba
 
Tanganyika kwanza ihuishwe then ziwe saba, 10, au 50 haijalishi, cha msingi tuwe na tanganyika yetu mengine tutajadili!
 
IBARA YA 1 YA RASIMU YA KATIBA YENYEWE
1.-(1) Jamhuri ya Muungano wa Tanzania ni Shirikisho lenye
mamlaka kamili ambayo imetokana na Muungano wa nchi mbili za
Jamhuri ya Tanganyika na Jamhuri ya Watu wa Zanzibar ambazo kabla
ya Hati za Makubaliano ya Muungano ya mwaka 1964 zilikuwa nchi
huru.

Hivyo ndivyo inavyosomeka rasimu yenyewe. Kama jina la Zanzibar limebaki, na kama nchi zote bado ni huru, kwanini jina la Tanganyika life?

ANGALIA IBARA YA 3, IBARA NDOGO YA PILI.
(2) Siku Kuu za Kitaifa zitakuwa ni:
(a)Siku ya Uhuru wa Tanganyika, itakayoadhimishwa tarehe 9
Disemba;
(b)Siku ya Mapinduzi ya Zanzibar, itakayoadhimishwa tarehe 12
Januari;
(c)Siku ya Muungano wa Tanganyika na Zanzibar,
itakayoadhimishwa tarehe 26 Aprili;

Kama tunaita Tanzania bara itakuwa na maana ya kuikiuka Katiba kabla hata haijapitishwa kwa 7bu Ibara ya 3(2)a ni sawa na kuadhimisha cku ya taifa lililokwisha kufa!

Na kwa mujibu wa Ibara ya 3(2)c haioneshi kuwa kuna SHIRIKISHO LA TANZANIA BARA NA ZANZIBAR bali Tanganyika na Zanzibar.

Je, Mh Jaji Warioba anataka kututengenezea nchi ya 3? i.e Tanganyika, Zanzibar na Tanzania Bara

TUNAITAKA TURUDISHIWE TANGANYIKA YETU.
 
kizuri gharama. Serikali 3 ndio mpango!

Mie nawashangaa Watanzania, pia najishangaa mwenyewe.
Tumeacha kubishania mambo ya msingi, kama vile haki za binadamu, miliki ya rasilimali, tunabishana idadi ya serikali..!!!!!!!!!!

Hii ni aibu.
Ningekuwa Rais, ningeahirisha mchakato wote hadi tutakapokuwa tumejiandaa vyema kuitafuta hiyo katiba.
 
IBARA YA 1 YA RASIMU YA KATIBA YENYEWE
1.-(1) Jamhuri ya Muungano wa Tanzania ni Shirikisho lenye
mamlaka kamili ambayo imetokana na Muungano wa nchi mbili za
Jamhuri ya Tanganyika na Jamhuri ya Watu wa Zanzibar ambazo kabla
ya Hati za Makubaliano ya Muungano ya mwaka 1964 zilikuwa nchi
huru.

Hivyo ndivyo inavyosomeka rasimu yenyewe. Kama jina la Zanzibar limebaki, na kama nchi zote bado ni huru, kwanini jina la Tanganyika life?

ANGALIA IBARA YA 3, IBARA NDOGO YA PILI.
(2) Siku Kuu za Kitaifa zitakuwa ni:
(a)Siku ya Uhuru wa Tanganyika, itakayoadhimishwa tarehe 9
Disemba;
(b)Siku ya Mapinduzi ya Zanzibar, itakayoadhimishwa tarehe 12
Januari;
(c)Siku ya Muungano wa Tanganyika na Zanzibar,
itakayoadhimishwa tarehe 26 Aprili;

Kama tunaita Tanzania bara itakuwa na maana ya kuikiuka Katiba kabla hata haijapitishwa kwa 7bu Ibara ya 3(2)a ni sawa na kuadhimisha cku ya taifa lililokwisha kufa!

Na kwa mujibu wa Ibara ya 3(2)c haioneshi kuwa kuna SHIRIKISHO LA TANZANIA BARA NA ZANZIBAR bali Tanganyika na Zanzibar.

Je, Mh Jaji Warioba anataka kututengenezea nchi ya 3? i.e Tanganyika, Zanzibar na Tanzania Bara

TUNAITAKA TURUDISHIWE TANGANYIKA YETU.
 
Fanyeni mfanyavyo,jiiteni mpendavyo,bila ya mamlaka kamili ya z'br hapatoshi,zanzbr kwanza.
 
Fanyeni mfanyavyo,jiiteni mpendavyo,bila ya mamlaka kamili ya z'br hapatoshi,zanzbr kwanza.

Rukarukeni mpaka mchoke...lakini siku mkifanikisha kujitenga na JMT mjue wenzenu huko huko Zanzibar ambao kwa sasa wako kimya watakirudisha kisiwa kilicho na Ikulu ya Zanzibar kwenye Jamhuri ya Watu wa Tanzania.
 
Similar Discussions

0 Reactions
Reply
Back
Top Bottom