Jaji Mark Bomani: Silipendi jina Tanzania Bara

Bramo

JF-Expert Member
Oct 21, 2009
11,215
2,000
Wana JF, Amani iwe nanyi.

Akiisifu Rasimu ya Katiba Mypa Kipengele cha Muungano wa Serikali tatu.
Mwanasheria Nguli Nchini na aliyewahi kuwa Mwanasheria Mkuu wa Serikali , Jaji Mstaafu Mark Bomani amesmea kuwa Halipendi Jina Tanzania Bara.
Amehoji ni Kwanini Baadhi ya Watu wanaona Aibu kutumia Jina Tanganyika Badala ya Tanzania Bara.
Amesema kuwa Muundo wa Muungano wa Serikali tatu ndo Moarobaini Pekee kwa Kero Zote za Muungano.

Source ITV Habari

My Take

Huu ni Muendelezo wa Wazee wetu wenye Heshima zilizotukuka kutuonesha kuwa, CCM ni janga la Kitaifa.
CCM Wako Tayari kuiuza Tanganyika kwa Zanzibar for the sake ya Kupinga Muundo wa Serikali Tatu.
Vynazo Kutoka Ndani ya CCM ambavyo vinachukizwa na Ubinafsi wa Viongozi wa Ngazi za juu ndani ya CCM.
Vinasema kuwa, CCM wamjeipanga kwenda Zanzibar ku Lobe Wanzaznibar wapinge Mfumo wa Serikali Tatu.
CCM Wameonesha kuwa wako Tayari kuteleza Matakwa yote ya Akina Jussa na Maalimu Seif katika Kutafuta Unngwaji Mkono Kwenye Kupinga Muundo wa Serkali Tatu.

Wa Tanganyika, Tushirikiane Kuitokomeza CCM
 

Ronal Reagan

JF-Expert Member
Nov 4, 2010
4,843
2,000
duh,serekali 3 mzıgo bana
Tupeni ghrama (figures) za serikali 2 na tatu kisha tuchambue na kupembua. Naona neno "mzigo/ghrama" linapigiwa upatu sana. Kwangu mimi kama ndio gharama ya kulipa ili tuwe na amani na maendeleo I will happily pay. Kumbuka "cheap is always more costly/expensive"
 

Dotworld

JF-Expert Member
Aug 10, 2011
3,946
2,000
duh,serekali 3 mzıgo bana
Hizi mbili zenyewe mzigo! Sasa hivi penyewe tuna Marais watano (5) ambapo waNNE (4) ni Wazanzibari.

  1. Rais wa Jamhuri wa Muungano
  2. Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano - (Zanzibar)
  3. Rais wa Zanzibar - (Zanzibar)
  4. Makamu wa Kwanza wa Rais - (Zanzibar)
  5. Makamu wa Pili wa Rais - (Zanzibar)
Haya Ongeza na Waziri Mkuu, Maspika wawili (Zanzibar & Muungano) + wengine wengi
.
 

Aggrey86

JF-Expert Member
Jun 26, 2011
855
195
Ndiyo tujiite watanganyika lakini hapana serikali tatu bwana mi binafsi pia naona mzigo tu serilikali tatu zote hizo za nini?
 

blueray

JF-Expert Member
Sep 15, 2012
2,218
0
Hongera Mheshimiwa Mark, hayo ndiyo maoni ya wananchi.

Ila navyojua Mimi wananzibari wanataka Serikali Mbili Na Shirikisho (Muungano Wa Mkataba) Au vinginevyo Muungano uvunjike.

Wazanzibari wako sahihi. Muungano ni sawa na ndoa huwezi ukalazimisha ndoa hata Kama mke au mme unampenda kiasi gani. Ndoa haitadumu au Siku zote itakuwa na mgogoro!

Watanganyika wapeni uhuru wanzenu Wazanzibari wapumue
 

kinauche

JF-Expert Member
Oct 17, 2012
7,685
2,000
Ndiyo tujiite watanganyika lakini hapana serikali tatu bwana mi binafsi pia naona mzigo tu serilikali tatu zote hizo za nini?
Mzigo kivipi? Kuna rasilimali za kutosha kabisa. I want our Tanganyika back.

Sent from my BlackBerry 9860 using JamiiForums
 

Songoro

JF-Expert Member
May 27, 2009
4,127
0
Tanganyika kwanza ihuishwe then ziwe saba, 10, au 50 haijalishi, cha msingi tuwe na tanganyika yetu mengine tutajadili!
 

bernardp

JF-Expert Member
Mar 23, 2009
619
1,000
kizuri gharama. Serikali 3 ndio mpango!
Mie nawashangaa Watanzania, pia najishangaa mwenyewe.
Tumeacha kubishania mambo ya msingi, kama vile haki za binadamu, miliki ya rasilimali, tunabishana idadi ya serikali..!!!!!!!!!!

Hii ni aibu.
Ningekuwa Rais, ningeahirisha mchakato wote hadi tutakapokuwa tumejiandaa vyema kuitafuta hiyo katiba.
 

Bahati furaha

JF-Expert Member
Jul 11, 2012
2,943
2,000
IBARA YA 1 YA RASIMU YA KATIBA YENYEWE
1.-(1) Jamhuri ya Muungano wa Tanzania ni Shirikisho lenye
mamlaka kamili ambayo imetokana na Muungano wa nchi mbili za
Jamhuri ya Tanganyika na Jamhuri ya Watu wa Zanzibar ambazo kabla
ya Hati za Makubaliano ya Muungano ya mwaka 1964 zilikuwa nchi
huru.Hivyo ndivyo inavyosomeka rasimu yenyewe. Kama jina la Zanzibar limebaki, na kama nchi zote bado ni huru, kwanini jina la Tanganyika life?

ANGALIA IBARA YA 3, IBARA NDOGO YA PILI.
(2) Siku Kuu za Kitaifa zitakuwa ni:
(a)Siku ya Uhuru wa Tanganyika, itakayoadhimishwa tarehe 9
Disemba;
(b)Siku ya Mapinduzi ya Zanzibar, itakayoadhimishwa tarehe 12
Januari;
(c)Siku ya Muungano wa Tanganyika na Zanzibar,
itakayoadhimishwa tarehe 26 Aprili;


Kama tunaita Tanzania bara itakuwa na maana ya kuikiuka Katiba kabla hata haijapitishwa kwa 7bu Ibara ya 3(2)a ni sawa na kuadhimisha cku ya taifa lililokwisha kufa!

Na kwa mujibu wa Ibara ya 3(2)c haioneshi kuwa kuna SHIRIKISHO LA TANZANIA BARA NA ZANZIBAR bali Tanganyika na Zanzibar.

Je, Mh Jaji Warioba anataka kututengenezea nchi ya 3? i.e Tanganyika, Zanzibar na Tanzania Bara

TUNAITAKA TURUDISHIWE TANGANYIKA YETU.
 

Bobwe

JF-Expert Member
May 21, 2013
1,239
0
Fanyeni mfanyavyo,jiiteni mpendavyo,bila ya mamlaka kamili ya z'br hapatoshi,zanzbr kwanza.
 

TUJITEGEMEE

JF-Expert Member
Nov 6, 2010
15,222
2,000
Fanyeni mfanyavyo,jiiteni mpendavyo,bila ya mamlaka kamili ya z'br hapatoshi,zanzbr kwanza.
Rukarukeni mpaka mchoke...lakini siku mkifanikisha kujitenga na JMT mjue wenzenu huko huko Zanzibar ambao kwa sasa wako kimya watakirudisha kisiwa kilicho na Ikulu ya Zanzibar kwenye Jamhuri ya Watu wa Tanzania.
 

Ng'wanambula

Senior Member
Oct 2, 2011
197
195
Hiyo rasimu ina mapungufu kibao
1. Hiyo nchi ya Tanzania Bara haijawahi kutokea duniani na hakuna nchi imewahi kupata uhuru inaitwa hivyo
2. Hii rasimu inasema ikipitishwa na wananchi itakuwa katiba, haisemi isipopitishwa itakuwaje?
3. Kuna section inaongelea haki za raia na nyongine inaongelea haki za wanawake. Kwani wanawake sio raia? kama ni hivyo basi either wanfeweka na haki za wanaume au hiyo section isingekuwepo kabisa ili kuwepo na haki za raia tu. Wote wanawake na wanaume ni raia.
4. Hii ni rasimu yakatiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na ikipitishwa itakuwa katiba ya JMT yenye washirika wawili i.e. Tanganyika na Zanzibar. Itawezekana vipi kuwa na nchi isiyo na katiba (Tanganyika )ndani ya muungano ambapo JMT na Zanzibar zina katiba zao?
5. Rasimu inajichanganya yenyewe kwa kutumia jina TANGANYIKA kwenye kurasa za mwanzo na kule ndani nchi hiyo haitajwi bali inaonekana TANZANIA BARA
6. Hayo ni baadhi tu ya mapungufu mengi yaliyopo kwenye hii rasimu
 

kmbwembwe

JF-Expert Member
Aug 16, 2012
7,017
2,000
Tupeni ghrama (figures) za serikali 2 na tatu kisha tuchambue na kupembua. Naona neno "mzigo/ghrama" linapigiwa upatu sana. Kwangu mimi kama ndio gharama ya kulipa ili tuwe na amani na maendeleo I will happily pay. Kumbuka "cheap is always more costly/expensive"
Mimi kwangu serikali mbili tosha ili mradi kero za kweli zirekebishwe kwa katiba. Wanaoratibu madai ya serikali 3 zenj hawana nia njema. Wanataka serikali ya tanganyika kama hatua ya kuvunja muungano. Sasa kwa nini tupoteze tena muda badala ya kutafuta maendeleo kwa kupigiwa kelele za kero ya muungano wakati wazenj wanawasikiliza wenye nia ya kuuvunja. Suluhisho la kweli ni kua na serikali moja au mbili vinginevyo muungano uvunjwe sasa.
 
Top Bottom