mito
JF-Expert Member
- Jun 20, 2011
- 10,513
- 10,404
Kwa nini viongozi wetu wanakuwa hawataki kusikia wananchi wakiomba kupewa kura ya maoni (Referendum) ili kujiamulia mstakabali wa muungano kama uendelee kuwepo au uwekwe kwenye kopo taka (dustbin).
Tumeishi na manung'unguniko hasa kutoka Zanzibar kwa miaka zaidi ya miaka 34 na katika hiyo, mpaka Rais Aboud Jumbe alishinikizwa kuachia madaraka kwa sababu ya swala hili la Muungano na sidhani kama inafaa tuendelee kuishi tena na malalamiko wakati nafasi ya kufanya mabadiliko imetokea. We are just horsing around with a RARE opportunity.
Huu ni muda wa kuwapa wananchi sauti itakayowafanya watoe maamuzi muhimu na hata likitokea jambo baya mbeleni, hakutakuwa na mtu au taasisi ya kubeba lawama zaidi ya wananchi wenyewe.
It's time for REFERENDUM. The time is NOW kama nilivyosema few days ago kwenye hii Thread,
https://www.jamiiforums.com/katiba-...-moja-mbili-au-tatu-tupiganie-referendum.html
Mkuu hapo kwa red jibu ni hili, kwa sababu wanajua wakitoa nafasi hiyo (ya referendum) wanasiasa watawarubuni wananchi kuvunja muungano kwa maslahi yao (wanasiasa)