Jaji Mark Bomani awashukia polisi

abdulahsaf

JF-Expert Member
Aug 31, 2010
858
130
KUJIRUDIA kwa matukio ya polisi kutumia silaha za moto dhidi ya raia, kumepokewa kwa hisia tofauti, huku Mwanasheria Mkuu wa Kwanza wa Serikali, Jaji Mark Bomani akilitaka jeshi hilo kuacha kutumia nguvu wanapokuwa katika operesheni zao.

1.JPG

Jaji Mark Bomani

Wakizungumza jana kwa nyakati tofauti kuhusu tukio la hivi karibuni la kupigwa risasi mwandishi wa habari wa gazeti la Tanzania Daima, watu wa kada mbalimbali walisema, kitendo cha polisi kutumia nguvu sio busara.

Jaji Bomani kitendo cha polisi kutumia nguvu badala ya busara katika operesheni zao kinaweza kuleta uhasama kati ya wananchi na jeshi hilo.

Kwa ujumla matumizi ya nguvu kwa polisi si mazuri na nadhani tunatakiwa kubadilika katika hilo. alisema Jaji Bomani.

Bomani alieleza kuwa kwa ujumla polisi wanatumia vibaya silaha zao ingawa bado hajapata uhakika wa jinsi tukio la kujeruhiwa kwa Matutu lilivyokuwa .

Alisema tukio la Mwangosi lilikuwa baya zaidi lakini picha anayoiona na kuihusisha na tukio la juzi, ni kuwa kuna matumizi mabaya ya mashambulizi ya polisi kwa raia.

Hata hivyo wakati Jaji Bomani akieleza hayo Mwenyekiti wa Tume ya Haki za Binadamu na Utawala Bora, Jaji mstaafu Amiri Ramadhan Manento alisema kila tukio linalofanywa na polisi linatakiwa kufanyiwa uchunguzi kabla ya kuanza kulizungumzia.

Jaji Manento alisema akiwa ni mwanasheria hawezi kutoa hitimisho ya tukio la kujeruhiwa kwa Matutu kabla ya uchunguzi wa kisheria kufanyika.

Tunahitaji kujua mambo mengi, ya michakato ya makosa ya jinai, (criminal procedure) kwa mfano polisi walipoingia walifanya nini, walipotoka, ni maneno gani walimuuliza mtu wa kwanza waliyekutana naye.

Tunahitaji kujua iwapo walitumia kizuizi cha usalama(safe cage) katika silaha zao au la alisema Jaji Manento

Alisema kulingana na taarifa zilizopo katika magazeti bado unahitajika uchunguzi wa kujua ni namna gani polisi waliingia ndani ya nyumba hiyo.

Aidha Jaji huyo mstaafu alisema hawezi kuwahukumu polisi moja kwa moja kwani hakuna ushahidi kuwa walikuwa wakimwinda mwandishi, bali inawezekana waligundua kuwa ni mwandishi baada ya kumjeruhi.

Chanzo Mwananchi
 
....Hata hivyo wakati Jaji Bomani akieleza hayo Mwenyekiti wa Tume ya Haki za Binadamu na Utawala Bora, Jaji mstaafu Amiri Ramadhan Manento alisema kila tukio linalofanywa na polisi linatakiwa kufanyiwa uchunguzi kabla ya kuanza kulizungumzia.

Jaji Manento alisema akiwa ni mwanasheria hawezi kutoa hitimisho ya tukio la kujeruhiwa kwa Matutu kabla ya uchunguzi wa kisheria kufanyika. .....Aidha Jaji huyo mstaafu alisema hawezi kuwahukumu polisi moja kwa moja kwani hakuna ushahidi kuwa walikuwa wakimwinda mwandishi, bali inawezekana waligundua kuwa ni mwandishi baada ya kumjeruhi.
Halafu atakuja kusema kwamba wao Tume ya haki za binadamu hawawezi kufanya huo uchunguzi hadi mtu alete mashtaka ama malalamiko.

Kuna majibu huwa yanakera kweli.

KITAIFA

Na Waandishi Wetu

Posted Ijumaa,Decemba7 2012 saa 8:17 AM

KWA UFUPI

ASEMA WANATUMIA ZAIDINGUVU KULIKO MAARIFA

KUJIRUDIA kwa matukio ya polisi kutumia silaha za moto dhidi ya raia, kumepokewa kwa hisia tofauti, huku Mwanasheria Mkuu wa Kwanza wa Serikali, Jaji Mark Bomani akilitaka jeshi hilo kuacha kutumia nguvu wanapokuwa katika operesheni zao.

Wakizungumza jana kwa nyakati tofauti kuhusu tukio la hivi karibuni la kupigwa risasi mwandishi wa habari wa gazeti la Tanzania Daima, watu wa kada mbalimbali walisema, kitendo cha polisi kutumia nguvu sio busara.

Jaji Bomani kitendo cha polisi kutumia nguvu badala ya busara katika operesheni zao kinaweza kuleta uhasama kati ya wananchi na jeshi hilo.

"Kwa ujumla matumizi ya nguvu kwa polisi si mazuri na nadhani tunatakiwa kubadilika katika hilo." alisema Jaji Bomani.

Bomani alieleza kuwa kwa ujumla polisi wanatumia vibaya silaha zao ingawa bado hajapata uhakika wa jinsi tukio la kujeruhiwa kwa Matutu lilivyokuwa .

Alisema tukio la Mwangosi lilikuwa baya zaidi lakini picha anayoiona na kuihusisha na tukio la juzi, ni kuwa kuna matumizi mabaya ya mashambulizi ya polisi kwa raia.

Hata hivyo wakati Jaji Bomani akieleza hayo Mwenyekiti wa Tume ya Haki za Binadamu na Utawala Bora, Jaji mstaafu Amiri Ramadhan Manento alisema kila tukio linalofanywa na polisi linatakiwa kufanyiwa uchunguzi kabla ya kuanza kulizungumzia.

Jaji Manento alisema akiwa ni mwanasheria hawezi kutoa hitimisho ya tukio la kujeruhiwa kwa Matutu kabla ya uchunguzi wa kisheria kufanyika.

"Tunahitaji kujua mambo mengi, ya michakato ya makosa ya jinai, (criminal procedure) kwa mfano polisi walipoingia walifanya nini, walipotoka, ni maneno gani walimuuliza mtu wa kwanza waliyekutana naye.

Tunahitaji kujua iwapo walitumia kizuizi cha usalama(safe cage) katika silaha zao au la" alisema Jaji Manento

Alisema kulingana na taarifa zilizopo katika magazeti bado unahitajika uchunguzi wa kujua ni namna gani polisi waliingia ndani ya nyumba hiyo.

Aidha Jaji huyo mstaafu alisema hawezi kuwahukumu polisi moja kwa moja kwani hakuna ushahidi kuwa walikuwa wakimwinda mwandishi, bali inawezekana waligundua kuwa ni mwandishi baada ya kumjeruhi.

Alisema hili ni tukio la tofauti na lile la kuuwa kwa Mwangosi kwani Mwangosi alikuwa kashika vifaa vyake vya kazi lakini hapa Matutu hakuwa na kitambulisho chochote kuwa ni Mwandishi.

"Unajua polisi wanafuata amri na sheria na wapo kwa ajili ya kulinda raia wake, hivyo hatuwezi kusema kuwa walikuwa wakimwinda mwandishi, kwa sababu hata polisi naye amejeruhiwa kwa panga katika tukio hilo," alisema Jaji Manento

Mhadhiri wa Chuo Kikuu cha Dar es salaam Dk Kitila Mkumbo alisema kuwa jeshi la Polisi limekuwa halifanyi kazi zake kwa kufuata weledi hali inayosababisha kuongezeka kwa matukio ya raia kupigwa risasi na Taasisi ya serikali yenye dhamana ya kuimarisha usalama wa raia hao.

"Matukio haya yanaweza kuathiri amani ya nchi kwa sababu wananchi wakikosa imani na serikali yao wanaweza kufanya jambo lolote bila kufuata sharia, matokeo yake amani inatoweka" alisema Dk Mkumbo.

Dk Mkumbo aliongeza kuwa ni vema IGP Saidi Mwema akatilia mkazo juu ya kufanya kazi kwa weledi ili kuimarisha utendaji kazi wa jeshi la polisi na kulipa taswira mpya katika jamii.

Mkuu wa Idara ya Fedha waskuli ya Biashara chuoni hapoDk Esther Ishengoma alisema kuwa jeshi la Polisi linadhamana ya kulinda usalama wa raia na mali zao, litaendelea kubeba dhamana hiyo, jambo la msingi ni kudhibiti nidhanu ya askari wanapokuwa wakitekeleza majukumu yao.

"Ukiangalia matukio yanayotokea utaona kuna baadhi ya askari polisi wanaolichafua jeshi kwa kufanya mambo kinyume cha sheria, ni vema suala la nidhamu likaimarishwa ili kuongeza ufanisi," alisema Dk Ishengoma.

Mkazi wa Mbagala Mtongani Solomon Isaiah alisema matendo yanayofanywa na polisi ya kujeruhi na kuua raia ndani ya kipindi kifupi ni dalili za kutokuwepo utawala bora nchini na usimamizi mzuri wa ngazi za juu ndani ya Polisi.

"Hawa polisi hawajitakii kufanya hivyo bali wanatekeleza amri za viongozi wao wa ngazi za juu, hivyo basi lawama, hatua za kisheria na mabadiliko yafanyike kwenye ngazi hizo za juu za polisi ndipo wahamie kwa polisi wenyewe" alisema Isaiah.

Matukio ya kuua na kujeruhi raia yanayotekelezwa na jeshi la polisi yamezidi kuongezeka siku hadi siku nchini licha ya wadau na wananchi kupigia kelele matendo hayo hali ambayo imezidi kugharimu maisha ya Watanzania wengi wasio na hatia kwa kuchukua sheria mkononi.

Hivi karibuni Kituo cha Sheria na Haki za Binadamu (LHRC) kiliazimia kuishtaki Serikali kwa Mahakama ya Kimataifa ya masuala yaUhalifu(ICC) ili ichukue hatua zaidi juu ya mfululizo wa matukio ya kutisha yanayofanywa na jeshi la polisi kwa Wananchi baada ya Serikali kushindwa kuchukua hatua stahiki.

Kauli hizo imekuja siku moja baada ya polisi kulizungumzia tukio hilo kwamba lilitokea wakati wakiwa wanajihami.

Kamanda wa Polisi mkoa wa Kinondoni Charles Kenyela akizungumzia tukio la mwandishi huyo kupigwa risasi alisema alijeruhiwa baada ya kuanza kumshambulia askari kwa Panga.

Hata hivyo ufafanuzi wa kamanda huyo unatofautiana na ule wa Matutu na mashuhuda wa tukio hilo, ambao walisema kuwa polisi walivamia nyumba ya mwandishi huyo iliyopo maeneo ya Kunduchi huku wakimtaka mwanamke mmoja waliyemtaja kwa jina la mama J.

Katika maelezo yake Matutu alisema polisi hao walifika nyumbani kwake wakimtaka mkewe baada ya kumfananisha na mtu mwingine, kwamba wakati akiwa katika harakati za kumtenganisha mke polisi hao baada ya kuhisi huenda wakawa majambazi ndipo polisi hao wakampiga risasi ya bega.

Habari hii imeandaliwa na Florence Majani, Peter Elias na Nuzulack Dausen

Serikali inayojiona kuwa INAANGUKA MADARAKANI last OPTION wanayotumia kubaki MADARAKANI ni NGUVU za DOLA

POLISI; MAHAKAMA; JESHI
 
Back
Top Bottom