Gosbertgoodluck
JF-Expert Member
- Mar 3, 2008
- 2,855
- 401
Wazee,
Kuna jamaa mmoja aliniambia kwamba majaji ni watu makini sana katika kufanya mambo yao. Katika nchi zote duniani hata zisizofuata demokrasia na haki za binadamu majaji ni miongoni mwa kundi la watu wanaoheshimiwa sana. Kwa ujumla, hata Tanzania hali ndivyo ilivyo. Sasa kwa muktadha huo, nimekuwa nikimtafakari sana Jaji Lewis Makame kwamba hivi anajisikiaje anaposikia wananchi, NGOs, viongozi wakongwe na wanaoheshimika hapa nchini, vyombo vya habari na wanaharakati kwa ujumla wakipiga kelele kutaka mabadiliko ya Tume???? Kwamba tume anayoingoza siyo huru na kwamba maamuzi yake hayawezi kupingwa mahakamani.
Bila chembe ya shaka lazima naye anajua fika kwamba kinachoongelewa na wananchi ni haki. Lakini yeye anajisikiaje?? Anafanyeje kazi katika mazingira hayo, kama ni jaji aliyeiva kwelikweli??? Je, moyoni mwake ana amani kweli??