Jaji Lubuva: Tukio la Arusha ni 'fujo tu zilizotokea katika mkutano wa CDM!'

Zak Malang

JF-Expert Member
Dec 30, 2008
5,404
233
Ndivyo alivyosema Mwenyekiti huyo wa NEC katika mahojiano na mtangazaji wa kipindi cha Nipashe asubuhi leo akitangaza kuahirisha uchaguzi katika kata nne za Arusha. Hakutaja kabisa mlipuko, bali fujo tu!
 
Mteule wa fastjet unadhani atasemaje? Kwani natofauti na savimbi? Wote ancestor wao ni mmoja
 
Mwigulu nchimbi verified killer

Sent from my BlackBerry 9300 using JamiiForums
 
Watu wameenda shule lakini inakuwa kama hawajaenda shule! Why not say or speak the truth? Ndiyo yale yale ya Yesu aliyesema kama nimesema ukweli kwa nini unanipiga? akauliwza ukweli ni kitu gani? Inaelekea serikali ya TZ haijui ukweli iku hizi?
 
Ndivyo alivyosema Mwenyekiti huyo wa NEC katika mahojiano na mtangazaji wa kipindi cha Nipashe asubuhi leo akitangaza kuahirisha uchaguzi ktk kata nne za Arusha. Hakutaja kabisa mlipuko, bali fujo tu!
Kuna watu wanatakiwa kupimwa akili kabla ya kuhojiwa. Hasa alcohol content kwenye damu. Msije mkawaonea tu.
 
Aitwe kwenye tume iliyoundwa aeleze vizuri fujo zilivyo kuwa na mwanzilishi nani nadhani huyo ni shahidi wa muhimu sana
 
Anaongea kulingana na Masharti ya Kazi aliyopewa.Aliyempa Kazi ndie anayempangia Majukumu ya kutekeleza.
 
Anayo sema ni kweli kabisa, nyie mmelikoroga wenyewe, sasa mnataka kuisingizia ccm na polisi.
 
Anayo sema ni kweli kabisa, nyie mmelikoroga wenyewe, sasa mnataka kuisingizia ccm na polisi.

Wamelikoroga nini?
-Walizidisha muda wa kampeni?
-Walirusha mawe kwa mtu
-Walitukana mtu?
Eleza walichokosea ili tuende pamoja.
 
Ndivyo alivyosema Mwenyekiti huyo wa NEC katika mahojiano na mtangazaji wa kipindi cha Nipashe asubuhi leo akitangaza kuahirisha uchaguzi katika kata nne za Arusha. Hakutaja kabisa mlipuko, bali fujo tu!

tena huyu ndiye mwenyekiti wa tume ya uchaguzi kama ikiwezekana chadema ishinikize ajiuzulu tukio la la kigaidi unaliita fujo kwa maana ya criminal act
 
Halafu tunategemea haki kitendeka chini ya mtu kama huyu. Hizii Ndiyo hasara za kuwapa watu wasiostahili zawadi za ujaji. Title ya Jaji imeshushwa hadhi sana Tz kutokana na watu kama hawa.
 
Kwani huyu ana shida gani,ana maisha mazuri kama peponi.Anapungukiwa nini,hata waliokufa kwake ni mizoga fulani,hata hivyo wakati ni ukifika kila kitu kitabaki na asili na uhalali wake.Nawahii chipoo na kopo moto rangi ya chai kwa mama nijazie
 
Huyu anajidhalilisha mbele ya Watanzania. Labda atuambie yeye alikuwepo Arusha? Na nini kilisababisha fujo hizo? Ilikuwa kati ya nani na nani? Kwanini wahusika hawakukamatwa mpaka leo na polisi walikuwepo? Huyu mzee hata kwenye vyombo vya habari hafuatilii?
 
Kama kweli tungekuwa tunataka kuujua ukweli huyu mzee alitakiwa kuhojiwa maana inawezekana anaujua ukweli. Matukio haya ni zaidi ya laana
 
IGP Mwema amesema tumpe ushirikiano katika kuwataja wahusika ama watu wenyetaarifa kamili. Ngoja nimwandikie sms kuwa amuhoji huyu Jaji feki ampe taarifa. Ila huyu kama ataachiwa kusimamia uchaguzi 2015, hakika damu zisizo na hatia zitamwagika.
 
Aishie zake huko,mpaka afe yeye ndio ajue kuwa ni bomu,mnafiki mkubwa na chama chake.AKAFIE MBALI HUKO.
 
Back
Top Bottom