Jaji kiongozi Fakh Jundu amjibu Lissu kuhusu tuhuma zilizotolewa dhidi ya Mahakama Bungeni

mkuu henge ndo umeshuka leo kutoka sayari ya mars nini? jaji wa mahakama ya rufaa ya tz aitwaye mbarouk salim mbarouk fr6 zenji kumbe ana diploma ya law ya ud na bachelor of arts. sasa hivi ndo anaitafuta LLB pale pa professor mbwete(open university)

mkuu kunahabari zingine sijui hata huwa zinanipitaje,
Imenisikitisha sana mkuu!
 
kwa hili sijaona hoja ya lissu kujibiwa....halafu kwa nini mtu aongezewe wakati tuna wasomi wengi wanazurula na vyeti mtaan......MTU AKISTAAFU AKAPUMZIKE JAMANI SIO KUSHIKILIA TU NA HUU UONGOZI WA NCHI HIIHABARI ZA KUPEANA VYEO KWA URAFIKI KAMA ANAOFANYA BABA MWANAASHA HATUWEZI KUFIKA NA NDIO MAANA NCHI INAYUMBA JAMANI
 
HANA JIPYA, HANA SIFA. SIJUI ni mwanasheria gani huyu? Aaaaaaaa nimekumbuka, siyo mwanasheria ndiyo maana analopoka. ETI HAKUJITETEA? MBONA hata mahakamani watu huwa utetezi wao unatupiliwa mbali, kwa hiyo wanakuwa hawajajitetea. BUNGE ni mahali pa siasa, pa kuzungungumzia, neno parliament limetokana na neno parlour yaani sebule mahali pa kuzungumza, siyo mahakamani ambapo ni mahali pa kutolea ushahidi ambao unaweza kupokelewa au kutupiliwa mbali: JUNDU hajui anachokisema, anajundua tu.

UBAYA wa CCM wanaamini kuwa RAIS ni MUNGU NA WATEULE WAKE, KAMA HAWA MAJAJI FEKI NI WANA WA MUNGU, HAWAKOSEI. Wapi na wapi, hakuna kitu kama hicho. WANAMSHAMBULIA LISSU bure, ye2 anatafiti wao wanalopoka tu ... JIREKEBISHENI
 
Kwa hiyo, mtu asiye na degree ya Sheria kapewa uajaji wa mahakama ya rufaa yenye uweze kutoa hukumu ya kifo kwa mtu ye yote na mtu mzima na degree yake kichwani anakaa JF anamtetea Kikwete siku nzima.


ukisema ujaji wa rufaa, hapa unaongelea nafasi ambayo bado ni kubwa mno, kwani kesi zote toka mahakama kuu zikikatiwa rufaa hupelekwa huko. na rufaa ikitupwa basi ndio ujue mtu hana bahati tena.....mahakama ya rufaa sio ndogo kama inavyodhaniwa.
 
Du! Huyu Lissu ni BONGE LA TUNDU. Pengine yafaa aitwe LITUNDU kwani tundu lake si lakawaida. Anamfanya Jaji mzima aweweseke na asijue chakujibu? Tundu kweli kiboko ya sheria Tanzania. Sidhani kama huyu jaji alijua alichokua akiongea kwani hajajibu hoja hata moja. In fact, amempandisha chati Tundu Lissu. Du! I admire Lissu jamani
 
Huyu jaji bwana kama angeongezewa mkataba angeongezewa kama jaji wa kawaida na siyo kuteuliwa katika wadhifa mkubwa wa jaji kiongozi. Kama Kikwete hakumwona anafaa kushika wadhifa mkubwa yungali ndani ya umri (miaka 60) iweje sasa ateuliwe akiwa na miaka 63 kama siyo kumwandalia marupurupu tu? Huyu Jaji hajajibu kabisa hoja za mh. Lissu akajipange upya na huyo aliyembeba.
 
Wakuu,
Jaji kiongozi wa mahakama ya Tanzania Fakh Jundu amejibu tuhuma zilizotolewa na msemaji wa wizara ya Sheria na katiba tundu Lissu, kuwa si kweli.

Ninamnukuu,
Akizungumza baada ya kumuapisha Naibu Msajili wa Mahakama hiyo, John Kahyoza, kushika wadhifa huo jana, Jaji Jundu alisema yuko katika nafasi hiyo kwa mujibu wa sheria.

Alisema Rais ana mamlaka ya kuwaongezea muda majaji baada ya wao wenyewe kukubali.

“Taarifa iliyotolewa bungeni kuhusu majaji, imenisikitisha sana. Kwa sababu hatuna nafasi ya kwenda kujitetea. Na kuhusu mimi kuendelea kuwa kwenye kiti hiki kwa mkataba bandia ni suala la uzushi, ambalo halina ukweli,” alisema Jaji Jundu na kuongeza:

“Vyombo vya habari vilivyoandika taarifa hiyo, waanike huo mkataba niliosaini kuendelea kuwa na wadhifa huu.”

My take; Jaji hakujibu hoja za tundu Lissu hata mmoja, kweli Lissu ni Kiboko.
Source Nipashe.



Habari kamili. Hii hapa.
Jaji Mkuu: Nimekasirishwa






Jaji Kiongozi, Fakihi Jundu, amesema amesikitishwa na kitendo cha majaji wa Mahakama Kuu ya Tanzania kutuhumiwa bungeni, kwa kuwa hawana nafasi ya kwenda kwenye chombo hicho kujitetea.

Miongoni mwa tuhuma zinazodaiwa kutolewa bungeni na Msemaji wa Kambi Rasmi ya Upinzani Bungeni wa Wizara ya Katiba na Sheria, Tundu Lissu, dhidi ya majaji hao, ni pamoja na iliyomhusu yeye mwenyewe (Jaji Jundu) ya kuendelea kuwa kwenye kiti hicho kwa kutumia mkataba bandia.

Lissu ambaye ni Mbunge wa Singida Mashariki (Chadema) na Mnadhimu Mkuu wa Kambi hiyo, alitoa tuhuma hizo wakati akiwasilisha maoni ya kambi hiyo kuhusu hotuba ya makadirio ya mapato na matumizi ya Wizara ya Katiba na Sheria iliyowasilishwa na Waziri wa wizara hiyo, Mathias Chikawe.

Akizungumza baada ya kumuapisha Naibu Msajili wa Mahakama hiyo, John Kahyoza, kushika wadhifa huo jana, Jaji Jundu alisema yuko katika nafasi hiyo kwa mujibu wa sheria.

Alisema Rais ana mamlaka ya kuwaongezea muda majaji baada ya wao wenyewe kukubali.

“Taarifa iliyotolewa bungeni kuhusu majaji, imenisikitisha sana. Kwa sababu hatuna nafasi ya kwenda kujitetea. Na kuhusu mimi kuendelea kuwa kwenye kiti hiki kwa mkataba bandia ni suala la uzushi, ambalo halina ukweli,” alisema Jaji Jundu na kuongeza:

“Vyombo vya habari vilivyoandika taarifa hiyo, waanike huo mkataba niliosaini kuendelea kuwa na wadhifa huu.”

Hata hivyo, alisema Mahakama ya Tanzania haiwezi kufanya mabishano ambayo hayana msingi kwa kuwa yote yaliyozungumzwa yamesikilizwa upande mmoja.

Tuhuma hizo zinazodaiwa kutolewa na Lissu dhidi ya majaji wanane wa Mahakama Kuu, mmoja wao akiwa ni Jaji wa Mahakama ya Rufaa ya Tanzania pamoja na Jaji Jundu.

Baadhi ya majaji wanatuhumiwa kuteuliwa wakiwa wamekaribia muda wao wa kustaafu kwingineko katika utumishi wa umma na wanapewa ‘zawadi’ ya ujaji ili kuwawezesha kupata mafao ya majaji wastaafu, ambayo yameboreshwa sana katika miaka ya karibuni.

Wengine wanatuhumiwa kuteuliwa huku wakiwa wagonjwa mahututi, ambapo inadaiwa kuwa hawakuwahi kuandika hukumu hata moja kabla ya mauti kuwafika.

Majaji wengine wanatuhumiwa kwa kutoandika hukumu na hivyo kuwa wacheleweshaji wakubwa wa kesi katika Mahakama Kuu na wengine kwa kupewa mkataba mpya baada ya kustaafu kama Jaji wa mahakama hiyo.

Majaji wengine wanatuhumiwa kwa “kushinikiza au kushawishi kushughulikia au kuamua kwa upendeleo mashauri yaliyowahusu jamaa au rafiki zao na kuwaandalia sababu za rufaa baadhi ya washitakiwa waliotiwa hatiani na mahakama za mahakimu.

Julai 13, 2012 Kambi Rasmi ya Upinzani Bungeni iliwasilisha maoni yake kuhusu Mpango na Makadirio ya Matumizi ya Wizara ya Katiba na Sheria kwa mwaka wa fedha 2012/2013. Pamoja na mambo mengine, yalihusu utaratibu wa uteuzi wa majaji wa Mahakama ya Tanzania.

Maoni ya Kambi yalizua mjadala mkubwa ndani na nje ya Bunge huku wachangiaji wengi wakimtuhumu Msemaji wa Kambi kwa “kuidhalilisha” Mahakama na “kuwadhalilisha majaji” (Gosbert Blandes-Karagwe CCM); “kuwavunjia heshima majaji” (Naibu Spika Job Ndugai); kuwatukana na kuwadhalilisha majaji (Murtaza Mangungu-Kilwa Kaskazini); “kuwa-offend, kuwadhalilisha na kuwanyanyasa majaji” (Assumpter Mshama-Nkenge CCM); “kufedhehesha Mahakama na majaji” (Mwanasheria Mkuu wa Serikali Frederick Werema).

Aidha, Msemaji wa Kambi ya Upinzani alishambuliwa kwa kudaiwa kuwa mfitini na asiye na akili timamu (Muhammad Chomboh- Magomeni CCM)); na “kujiamini kwamba yeye anajua zaidi kuliko watu wengine wote” (Mangungu).

Kwa upande wake, Waziri Chikawe alilihakikishia Bunge kwamba “... haijatokea hata siku moja katika nchi hii Rais akamteua Jaji wa Mahakama Kuu bila kuzingatia mapendekezo yaliyopelekwa kwake na Tume ya Uajiri wa Mahakama. Zaidi ya hayo labda Mheshimiwa Lissu anamjua Jaji angalau mmoja na anaweza akamtaja aseme Jaji huyu ametolewa tu mitaani na Mheshimiwa Rais, yupi hakuna… hawa majaji wote walioteuliwa wamepitia mchakato huu wa kikao kizito sana cha watu ambao ndiyo wenye sheria ya nchi hii.”

Baadaye Msemaji wa Kambi alitakiwa kufuta kauli yake kuhusu uteuzi wa majaji usiofuata utaratibu uliowekwa na Katiba.

Lissu alikataa kufuta kauli hiyo na Mwenyekiti wa kikao alielekeza Msemaji wa Kambi apelekwe kwenye Kamati ya Haki, Maadili na Madaraka ya Bunge kwa hatua zaidi.

Alichukua uamuzi huo ili masuala hayo yapatiwe ufafanuzi ili wananchi wapate picha kamili na ya kweli kuhusu jambo hilo.

Hata hivyo taarifa zilizovuja kutoka kwenye kamati hiyo zilieleza kile alichowasilisha Lissu kuwa ni kufafanua tuhuma moja baada ya nyingine na kuwataja majaji hao kwa majina na walivyoteuliwa au kushindwa kuwajibika kwa mujibu wa viapo vya kazi yao.

Katika maelezo yake kwa Kamati ya Haki, Maadili na Madaraka ya Bunge, Lissu alisema, “Nitajitahidi kwa kadri inavyowezekana kutoa ushahidi unaothibitisha kwamba siyo tu kwamba utaratibu wa kikatiba katika uteuzi wa majaji umekiukwa mara nyingi, bali pia majaji wengi walioteuliwa kwa utaratibu wa nje ya Katiba wamekuwa hawana ‘uwezo, ujuzi na kwa kila hali hawakufaa kukabidhiwa madaraka ya Jaji wa Mahakama Kuu.”

Ripoti ya kamati hiyo hajawekwa hadharani, ingawa kuna hisia kwamba utetezi wa Lissu siyo tu umefungua mambo mapya bali umewafanya waliokuwa wanamkejeli na kupuuza kuanza kuwaza mara mbili juu ya misimamo yao ya awali.




CHANZO: NIPASHE

Kama sikosei mwananchi yoyote anaweza kuwa summoned na kamati ya Bunge au kulalamika kuhusu yaliyosemwa ndani ya Bunge dhidi yake, je majaji wamekuwa-excluded?
 
Nimekumbuka mfano ni Kesi ya Bwana Mengi na Adam Malima ambayo ilishughulikiwa na Bunge, sasa yeye ni kitu gani kimemzuia?! Au ndio umbumbumbu?
 
kwa hili sijaona hoja ya lissu kujibiwa....halafu kwa nini mtu aongezewe wakati tuna wasomi wengi wanazurula na vyeti mtaan......MTU AKISTAAFU AKAPUMZIKE JAMANI SIO KUSHIKILIA TU NA HUU UONGOZI WA NCHI HIIHABARI ZA KUPEANA VYEO KWA URAFIKI KAMA ANAOFANYA BABA MWANAASHA HATUWEZI KUFIKA NA NDIO MAANA NCHI INAYUMBA JAMANI

Wanasheria wengi na mawakili wengi wamejazana ktk law firms hapa nchini wakilipwa mishahara kiduchu kwa sababu hamna kazi. Wengine anastaafu halafu anapewa kazi kisa uzoefu. Je, hawa wengine watapataje uzoefu?
Katiba mpya ni muhimu sana kuweka mambo mengi sawa.
 
Mimi nadhani Kikwete anajua anachokifanya. Ana ajenda ambayo madhara yake tutakuja kuyaona miaka mingi ijayo.
Ukishashusha hadhi ya mahakama kuu kwa kuweka watu ambao sio qualified kuwa mahakimu wa rufaa ni kwamba umeshaondoa nguvu za mhimili wa pili wa mamlaka katika dola. Kwenye usalama wa taifa hali ni hiyo hiyo.Dr. Slaa hakukosea aliposema kuwa Kikwete ni janga la taifa.
 
Duu!!!!!!
Ni bora umuite Jundu, lile la kwanza linasikika vibaya kwa kidhungu, naamini wewe ndiye.

Hawa huwa wanakuja kupotosha mjadala ukishamjibu ndo lengo lake limetimia. Mpotezee. Maana anatutoa kwenye hoja ya Aweda ya majaji feki
 
Kuhusu Jundu Lissu alisema hivi;

JAJI KIONGOZI FAKIH JUNDU


Jaji Kiongozi Fakih Jundu aliteuliwa kuwa Jaji wa Mahakama Kuu na Rais Mkapamwaka 2003. Julai 29, 2009, Jaji Jundu wakati huo akiwa Jaji Mfawidhi wa Kandaya Iringa, alitoa taarifa ya kustaafu kwa mujibu wa sheria. Hata hivyo, marabaada ya kutoa taarifa hiyo, Jaji Jundu siyo tu alipewa mkataba wa ujaji kwamiaka mitatu, bali pia alipandishwa cheo na kufanywa Jaji Kiongozi.


Kama hiyo haitoshi, inasemekana sasa kwamba Jaji Kiongozi Jundu ameongezewamkataba mwingine tena wa miaka miwili kuendelea kuwa Jaji Kiongozi kuanziaJulai 29, 2012! Huu ni ukiukaji wa Katiba. Kwanza, kwa mujibu wa Taarifa yaKikundi Kazi, “... umri wa kustaafu wa Jaji Kiongozi ni miaka sitini.... Hivyo,iwapo Rais atamuongezea Jaji Kiongozi muda wa kufanya kazi, hatamuongezea kamaJaji Kiongozi.”



Kwa maana nyingine, kama ilikuwa makosa kikatiba kumpa Jaji Jundu mkataba waajira kama Jaji wa kawaida, ilikuwa makosa makubwa zaidi kikatiba kumpandishacheo na kumfanya Jaji Kiongozi wakati alikwishafikisha umri wa kustaafu wa JajiKiongozi! Pili, kwa utamaduni uliozoeleka Tanzania, majaji wamekuwawanaongezewa kipindi kimoja cha miaka miwili ili wamalizie kesi walizokuwa nazohadi muda wao wa kustaafu unawadia. Kwa msimamo wa kikatiba ulioelezwa na Jajiwa Rufaa Luanda, Jaji Mkuu Ramadhani na Kikundi Kazi, siyo sahihi kwa JajiKiongozi Jundu kustaafu na kupewa mkataba wa kuendelea na wadhifa huokupindukia muda wake wa kustaafu kwa mujibu wa Katiba!



Nyongeza hii ya pili ya mkataba wa Jaji Kiongozi Jundu imewafanya watuwanaojiita ‘Watumishi wa Mhimili wa Mahakama’ kumwandikia Msajili wa Mahakamaya Rufani ya Tanzania kulalamikia jambo hilo. Kwa mujibu wa barua yao, ambayopia ilinakiliwa kwa Mwanasheria Mkuu na Jaji Mkuu, watu hao wamesema yafuatayokuhusu Jaji Kiongozi Jundu: “Sisi watumishi wa Mahakama tunafahamu udhaifumkubwa kiutendaji alionao Jaji Kiongozi wetu wa sasa. Kimsingi hamudu madarakahaya. Ipo mifano mingi ya udhaifu wa Jaji Jundu. Mfano alimhamisha hakimukutoka kituo chake cha kazi kama adhabu kwa vile hakimu huyo alitoa maamuziambayo yeye hakuyafurahiya kwenye ile kesi maarufu ya kibaragashia. Ni busaraza Jaji Mkuu, Mohamed Chande Othman, ndizo zilizomsaidia hakimu huyo.”

sasa hapo kajibu kitu gani?

Mwenye kumbukumbu sahihi ma akili timamu atajua nini kinaendelea na. hasa ikizingatiwa kuwa kesi ya kibaragashia ilitokea lini. Just time will tell.
 
HANA JIPYA, HANA SIFA. SIJUI ni mwanasheria gani huyu? Aaaaaaaa nimekumbuka, siyo mwanasheria ndiyo maana analopoka. ETI HAKUJITETEA? MBONA hata mahakamani watu huwa utetezi wao unatupiliwa mbali, kwa hiyo wanakuwa hawajajitetea. BUNGE ni mahali pa siasa, pa kuzungungumzia, neno parliament limetokana na neno parlour yaani sebule mahali pa kuzungumza, siyo mahakamani ambapo ni mahali pa kutolea ushahidi ambao unaweza kupokelewa au kutupiliwa mbali: JUNDU hajui anachokisema, anajundua tu.

UBAYA wa CCM wanaamini kuwa RAIS ni MUNGU NA WATEULE WAKE, KAMA HAWA MAJAJI FEKI NI WANA WA MUNGU, HAWAKOSEI. Wapi na wapi, hakuna kitu kama hicho. WANAMSHAMBULIA LISSU bure, ye2 anatafiti wao wanalopoka tu ... JIREKEBISHENI

Hapo kwenye red; nina uhakika 100% mkuu wa ule mhimili yuko kwenye usingizi wa pono kuhusu hiyo kitu. Teh teh teh teh! Burdani kweli kweli.
 
Huyu jaji kiongozi Fakhi Jundu nakumbuka uteuzi wake ulizua malumbano sana hapa JF back in a days. Hatimaye TL ametusaidia kukata mzizi wa fitna. Na katika kudhihirisha jinsi alivyo dhaifu kama walivyodai watumishi wa mahakama, majibu yake juu ya sakata hili yanamuelezea kinagaubaga.
 
[h=2][/h] Ijumaa, Agosti 31, 2012 06:30 Na Kulwa Mzee, Dar es Salaam

*Ashangazwa na tuhuma zinazoelekezwa kwake
*Asema viongozi wa aina hiyo ni hatari mno
JAJI Kiongozi, Fakhi Jundu amesema mjadala wa uteuzi wa majaji uliotokea hivi karibu ni dalili mbaya, inayoonyesha kuna watu fulani kama wakipewa nafasi ya kuongoza nchi, watawaangamiza wengine.

Licha ya kutotaja jina la kiongozi yeyote, kauli ya Jaji Jundu imekuja kufuatia Mbunge wa Singida Mashariki, ambaye ni Msemaji wa Kambi Rasmi ya Upinzani Bungeni na Waziri Kivuli wa Wizara ya Katiba na Sheria, Lissu kutoa ushahidi mbele ya Kamati ya Haki, Maadili na Madaraka ya Bunge, kuthibitisha alichokisema bungeni Julai 13, mwaka huu kuhusu uteuzi wa majaji na sifa zao.

Jaji Jundu alisema hayo jana, alipokuwa akihojiwa na waandishi wa habari ofisini kwake, kuhusu tuhuma zilizotolewa kwake, kuwa wadhifa wake aliupata kinyemela.

“Nawatoa hofu wananchi, aliyekuwa kitini wakati nateuliwa ni Jaji Augustino Ramadhani, ambaye anaheshimika sana, amesifiwa na Mbunge wa Singida Mashariki, Tundu Lissu (CHADEMA), atawezaje kupitisha mkataba wa aina hiyo.

“Hoja kama hizi, zinapotolewa bungeni, hatuna namna ya kujitetea, tumenyamaza kimya kwa sababu habari za bungeni tutamjibu nani, wataendelea kuchafua majina yetu, lakini wenye akili watajua.

“Hatutaki majibizano yasiyo na faida, sijui yalizungumzwa hayo kwa kumlenga Rais au majaji, Bunge halina ubavu wa kujadili mahakama wala majaji kwa majina, kwa sababu hatuna nafasi ya kujitetea,” alisema Jaji Jundu.

Alisema hiyo, ni dalili mbaya inayoonyesha kuna watu fulani kama wakifanikiwa kutawala nchi hii, watawakandamiza wengine bila kuwapa nafasi ya kujitetea.

Alisema jaji anapostaafu, Rais akimuona anafaa kwa manufaa ya taifa, basi humuomba kushika wadhifa mwingine.

“Rais ana watu wake na wanasheria wanaohusika katika uteuzi, haiingii akilini watu wote hao wanyamazie makosa,” alisema.

Alisema kama upo mkataba wake aliopata kinyemela, yupo tayari kuona unachapishwa kwenye magazeti.

Alisema anatuhumiwa kuwa na ubia na Jaji, Kassimu Nyangarika jambo ambalo halina ukweli wowote.

Hivi karibuni Mbunge wa Singida Mashariki ambaye ni Msemaji wa Kambi Rasmi ya Upinzani Bungeni na Waziri Kivuli wa Wizara ya Katiba na Sheria, Lissu alitoa ushahidi mbele ya Kamati ya Haki, Maadili na Madaraka ya Bunge, kuthibitisha alichokisema bungeni Julai 13, mwaka huu kuhusu uteuzi wa majaji na sifa zao.

Akizungumzia ajira ya Jaji Jundu, alisema iko katika kundi la watu wasiokuwa majaji kwa mujibu wa Katiba.

Alisema Julai 29, 2009, Jaji Jundu wakati huo akiwa Jaji Mfawidhi wa Kanda ya Iringa, alitoa taarifa ya kustaafu kwa mujibu wa sheria.

Hata hivyo, mara baada ya kutoa taarifa hiyo, Jaji Jundu si tu alipewa mkataba wa ujaji kwa miaka mitatu, bali pia alipandishwa cheo na kuwa Jaji Kiongozi.

Alisema inasemekana sasa, Jaji Kiongozi Jundu ameongezewa mkataba mwingine tena wa miaka miwili, ili aendelee kushika wadhifa huo, hadi Julai 29, 2012.

Kabla ya kujibu tuhuma hizo, Jaji Jundu alimwapisha John Kayoza kuwa Naibu Msajili wa Mahakama Kuu. Kayoza kabla ya uteuzi huo, alikuwa Msajili wa Mahakama ya Rufaa.

“Dhamira ya kufanya uteuzi wa wasajili ni kuwapa muda wa kutosha kushughulikia mambo ya mahakama tofauti na zamani, ambapo wasajili walikuwa wakifanya kazi za utawala na mahakama,” alisema.

Alisema Serikali iliahidi kutenga Sh bilioni 20, kwa ajili ya mahakama lakini kiasi kilichowekwa ni Sh bilioni 14.5 kwa mazingira hayo kuweka asilimia ni ngumu.


[h=4]Toa Maoni yako kwa habari hii[/h]

[h=3][/h]
010812.jpg
 
Back
Top Bottom