Jaji kiongozi Fakh Jundu amjibu Lissu kuhusu tuhuma zilizotolewa dhidi ya Mahakama Bungeni | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Jaji kiongozi Fakh Jundu amjibu Lissu kuhusu tuhuma zilizotolewa dhidi ya Mahakama Bungeni

Discussion in 'Jukwaa la Sheria (The Law Forum)' started by Mikael P Aweda, Aug 31, 2012.

 1. Mikael P Aweda

  Mikael P Aweda JF Gold Member

  #1
  Aug 31, 2012
  Joined: Dec 17, 2010
  Messages: 2,934
  Likes Received: 33
  Trophy Points: 0
  Wakuu,
  Jaji kiongozi wa mahakama ya Tanzania Fakh Jundu amejibu tuhuma zilizotolewa na msemaji wa wizara ya Sheria na katiba tundu Lissu, kuwa si kweli.

  Ninamnukuu,
  Akizungumza baada ya kumuapisha Naibu Msajili wa Mahakama hiyo, John Kahyoza, kushika wadhifa huo jana, Jaji Jundu alisema yuko katika nafasi hiyo kwa mujibu wa sheria.

  Alisema Rais ana mamlaka ya kuwaongezea muda majaji baada ya wao wenyewe kukubali.

  "Taarifa iliyotolewa bungeni kuhusu majaji, imenisikitisha sana. Kwa sababu hatuna nafasi ya kwenda kujitetea. Na kuhusu mimi kuendelea kuwa kwenye kiti hiki kwa mkataba bandia ni suala la uzushi, ambalo halina ukweli," alisema Jaji Jundu na kuongeza:

  "Vyombo vya habari vilivyoandika taarifa hiyo, waanike huo mkataba niliosaini kuendelea kuwa na wadhifa huu."

  My take; Jaji hakujibu hoja za tundu Lissu hata mmoja, kweli Lissu ni Kiboko.
  Source Nipashe.  Habari kamili. Hii hapa.
  Jaji Mkuu: Nimekasirishwa


  Jaji Kiongozi, Fakihi Jundu, amesema amesikitishwa na kitendo cha majaji wa Mahakama Kuu ya Tanzania kutuhumiwa bungeni, kwa kuwa hawana nafasi ya kwenda kwenye chombo hicho kujitetea.

  Miongoni mwa tuhuma zinazodaiwa kutolewa bungeni na Msemaji wa Kambi Rasmi ya Upinzani Bungeni wa Wizara ya Katiba na Sheria, Tundu Lissu, dhidi ya majaji hao, ni pamoja na iliyomhusu yeye mwenyewe (Jaji Jundu) ya kuendelea kuwa kwenye kiti hicho kwa kutumia mkataba bandia.

  Lissu ambaye ni Mbunge wa Singida Mashariki (Chadema) na Mnadhimu Mkuu wa Kambi hiyo, alitoa tuhuma hizo wakati akiwasilisha maoni ya kambi hiyo kuhusu hotuba ya makadirio ya mapato na matumizi ya Wizara ya Katiba na Sheria iliyowasilishwa na Waziri wa wizara hiyo, Mathias Chikawe.

  Akizungumza baada ya kumuapisha Naibu Msajili wa Mahakama hiyo, John Kahyoza, kushika wadhifa huo jana, Jaji Jundu alisema yuko katika nafasi hiyo kwa mujibu wa sheria.

  Alisema Rais ana mamlaka ya kuwaongezea muda majaji baada ya wao wenyewe kukubali.

  "Taarifa iliyotolewa bungeni kuhusu majaji, imenisikitisha sana. Kwa sababu hatuna nafasi ya kwenda kujitetea. Na kuhusu mimi kuendelea kuwa kwenye kiti hiki kwa mkataba bandia ni suala la uzushi, ambalo halina ukweli," alisema Jaji Jundu na kuongeza:

  "Vyombo vya habari vilivyoandika taarifa hiyo, waanike huo mkataba niliosaini kuendelea kuwa na wadhifa huu."

  Hata hivyo, alisema Mahakama ya Tanzania haiwezi kufanya mabishano ambayo hayana msingi kwa kuwa yote yaliyozungumzwa yamesikilizwa upande mmoja.

  Tuhuma hizo zinazodaiwa kutolewa na Lissu dhidi ya majaji wanane wa Mahakama Kuu, mmoja wao akiwa ni Jaji wa Mahakama ya Rufaa ya Tanzania pamoja na Jaji Jundu.

  Baadhi ya majaji wanatuhumiwa kuteuliwa wakiwa wamekaribia muda wao wa kustaafu kwingineko katika utumishi wa umma na wanapewa ‘zawadi' ya ujaji ili kuwawezesha kupata mafao ya majaji wastaafu, ambayo yameboreshwa sana katika miaka ya karibuni.

  Wengine wanatuhumiwa kuteuliwa huku wakiwa wagonjwa mahututi, ambapo inadaiwa kuwa hawakuwahi kuandika hukumu hata moja kabla ya mauti kuwafika.

  Majaji wengine wanatuhumiwa kwa kutoandika hukumu na hivyo kuwa wacheleweshaji wakubwa wa kesi katika Mahakama Kuu na wengine kwa kupewa mkataba mpya baada ya kustaafu kama Jaji wa mahakama hiyo.

  Majaji wengine wanatuhumiwa kwa "kushinikiza au kushawishi kushughulikia au kuamua kwa upendeleo mashauri yaliyowahusu jamaa au rafiki zao na kuwaandalia sababu za rufaa baadhi ya washitakiwa waliotiwa hatiani na mahakama za mahakimu.

  Julai 13, 2012 Kambi Rasmi ya Upinzani Bungeni iliwasilisha maoni yake kuhusu Mpango na Makadirio ya Matumizi ya Wizara ya Katiba na Sheria kwa mwaka wa fedha 2012/2013. Pamoja na mambo mengine, yalihusu utaratibu wa uteuzi wa majaji wa Mahakama ya Tanzania.

  Maoni ya Kambi yalizua mjadala mkubwa ndani na nje ya Bunge huku wachangiaji wengi wakimtuhumu Msemaji wa Kambi kwa "kuidhalilisha" Mahakama na "kuwadhalilisha majaji" (Gosbert Blandes-Karagwe CCM); "kuwavunjia heshima majaji" (Naibu Spika Job Ndugai); kuwatukana na kuwadhalilisha majaji (Murtaza Mangungu-Kilwa Kaskazini); "kuwa-offend, kuwadhalilisha na kuwanyanyasa majaji" (Assumpter Mshama-Nkenge CCM); "kufedhehesha Mahakama na majaji" (Mwanasheria Mkuu wa Serikali Frederick Werema).

  Aidha, Msemaji wa Kambi ya Upinzani alishambuliwa kwa kudaiwa kuwa mfitini na asiye na akili timamu (Muhammad Chomboh- Magomeni CCM)); na "kujiamini kwamba yeye anajua zaidi kuliko watu wengine wote" (Mangungu).

  Kwa upande wake, Waziri Chikawe alilihakikishia Bunge kwamba "... haijatokea hata siku moja katika nchi hii Rais akamteua Jaji wa Mahakama Kuu bila kuzingatia mapendekezo yaliyopelekwa kwake na Tume ya Uajiri wa Mahakama. Zaidi ya hayo labda Mheshimiwa Lissu anamjua Jaji angalau mmoja na anaweza akamtaja aseme Jaji huyu ametolewa tu mitaani na Mheshimiwa Rais, yupi hakuna… hawa majaji wote walioteuliwa wamepitia mchakato huu wa kikao kizito sana cha watu ambao ndiyo wenye sheria ya nchi hii."

  Baadaye Msemaji wa Kambi alitakiwa kufuta kauli yake kuhusu uteuzi wa majaji usiofuata utaratibu uliowekwa na Katiba.

  Lissu alikataa kufuta kauli hiyo na Mwenyekiti wa kikao alielekeza Msemaji wa Kambi apelekwe kwenye Kamati ya Haki, Maadili na Madaraka ya Bunge kwa hatua zaidi.

  Alichukua uamuzi huo ili masuala hayo yapatiwe ufafanuzi ili wananchi wapate picha kamili na ya kweli kuhusu jambo hilo.

  Hata hivyo taarifa zilizovuja kutoka kwenye kamati hiyo zilieleza kile alichowasilisha Lissu kuwa ni kufafanua tuhuma moja baada ya nyingine na kuwataja majaji hao kwa majina na walivyoteuliwa au kushindwa kuwajibika kwa mujibu wa viapo vya kazi yao.

  Katika maelezo yake kwa Kamati ya Haki, Maadili na Madaraka ya Bunge, Lissu alisema, "Nitajitahidi kwa kadri inavyowezekana kutoa ushahidi unaothibitisha kwamba siyo tu kwamba utaratibu wa kikatiba katika uteuzi wa majaji umekiukwa mara nyingi, bali pia majaji wengi walioteuliwa kwa utaratibu wa nje ya Katiba wamekuwa hawana ‘uwezo, ujuzi na kwa kila hali hawakufaa kukabidhiwa madaraka ya Jaji wa Mahakama Kuu."

  Ripoti ya kamati hiyo hajawekwa hadharani, ingawa kuna hisia kwamba utetezi wa Lissu siyo tu umefungua mambo mapya bali umewafanya waliokuwa wanamkejeli na kupuuza kuanza kuwaza mara mbili juu ya misimamo yao ya awali.
  CHANZO: NIPASHE
   
 2. mizambwa

  mizambwa JF-Expert Member

  #2
  Aug 31, 2012
  Joined: Oct 8, 2008
  Messages: 4,409
  Likes Received: 569
  Trophy Points: 280
  Huyu Jaji hakupaswa kusimama na kuwateetea majaji wenzie.

  Mh. Lissu aliwataja kwa majina, sasa kwa nini wale awtuhumiwa wasijitokeze kujibu hoja kwa ushahidi kama wanaona wameonewa????

  Huyu Jaji Kiongozi ni nani hata awajibie wenzie ambao nao wana midomo na akili????

  Kama kawaida yetu kuteteana katika uozo!!!!!!

  HJOja ni moja tu "Madaraka ya Rais yapunguzwe kwani anatoa fadhira kwa marafiki zake, kuna vijana wengi tu wana maliza vyuo na wanahitaji ajira, hawa waliostaafu hakuna haja ya kuendelea kuajiriwa tena wapewe nafasi vijana damu changa walete mabadiliko katika chombo hiki cha kisheria.  MIZAMBWA
  INANIUMA SANA!!!
   
 3. B

  Bangoo JF-Expert Member

  #3
  Aug 31, 2012
  Joined: Nov 3, 2011
  Messages: 5,594
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 135
  Kashikwa pabaya huyo!
  Yani anatetea uozo!
   
 4. G

  Gagnija JF-Expert Member

  #4
  Aug 31, 2012
  Joined: Apr 28, 2006
  Messages: 6,317
  Likes Received: 618
  Trophy Points: 280
  Atueleze pia kama rais anaweza kuteua mtu asiye na shahada ya sheria kuwa jaji.
   
 5. Lyimo

  Lyimo JF-Expert Member

  #5
  Aug 31, 2012
  Joined: Mar 7, 2006
  Messages: 3,828
  Likes Received: 33
  Trophy Points: 145
  Hapa Ndiyo mahakama inapojidharaulisha. Ni bora wangejibu madai yore yaliyotolewa kwa hoja, ama wangekaa kimya kumwachia udhaifu huo Mh.Rais kama alivyotuhumiwa.
   
 6. Nzenzu

  Nzenzu JF-Expert Member

  #6
  Aug 31, 2012
  Joined: Aug 10, 2011
  Messages: 859
  Likes Received: 2
  Trophy Points: 0
  Huyu nae ni mmoja ya wenye kashifa!
   
 7. OKW BOBAN SUNZU

  OKW BOBAN SUNZU JF-Expert Member

  #7
  Aug 31, 2012
  Joined: Aug 24, 2011
  Messages: 22,815
  Likes Received: 17,935
  Trophy Points: 280
  Basi tukawa na usalama mmoja pande za G&G Hotel Mwanza tukibadilishana uzoefu kuhusu mambo ya corruption and fraud, jamaa akakazia kuwa TUNDU LISSU kwa hili kaivua nguo nchi......na hakuna wa kuweza kumjibu.......akawachambua pia baadhi ya majaji wa Lissu ambao hata yeye amewahi kushuhudia ''undezi'' wao.....Chapa ilale CHADEMA
   
 8. M

  Mkwe21 JF-Expert Member

  #8
  Aug 31, 2012
  Joined: Apr 11, 2011
  Messages: 1,859
  Likes Received: 500
  Trophy Points: 280
  Hadi Aibu!! Sijui kama Huyu jaji anaweza Kuandika Report ya Kisheria!! Naye anajibu Kisiasa Hivi?? Tanzania Kazi Tunayo!! Bora angekaa Kimya!!
   
 9. Mpaka Kieleweke

  Mpaka Kieleweke JF-Expert Member

  #9
  Aug 31, 2012
  Joined: Feb 27, 2007
  Messages: 4,137
  Likes Received: 68
  Trophy Points: 145
  Kuhusu Jundu Lissu alisema hivi;

  JAJI KIONGOZI FAKIH JUNDU


  Jaji Kiongozi Fakih Jundu aliteuliwa kuwa Jaji wa Mahakama Kuu na Rais Mkapamwaka 2003. Julai 29, 2009, Jaji Jundu wakati huo akiwa Jaji Mfawidhi wa Kandaya Iringa, alitoa taarifa ya kustaafu kwa mujibu wa sheria. Hata hivyo, marabaada ya kutoa taarifa hiyo, Jaji Jundu siyo tu alipewa mkataba wa ujaji kwamiaka mitatu, bali pia alipandishwa cheo na kufanywa Jaji Kiongozi.


  Kama hiyo haitoshi, inasemekana sasa kwamba Jaji Kiongozi Jundu ameongezewamkataba mwingine tena wa miaka miwili kuendelea kuwa Jaji Kiongozi kuanziaJulai 29, 2012! Huu ni ukiukaji wa Katiba. Kwanza, kwa mujibu wa Taarifa yaKikundi Kazi, "... umri wa kustaafu wa Jaji Kiongozi ni miaka sitini.... Hivyo,iwapo Rais atamuongezea Jaji Kiongozi muda wa kufanya kazi, hatamuongezea kamaJaji Kiongozi."  Kwa maana nyingine, kama ilikuwa makosa kikatiba kumpa Jaji Jundu mkataba waajira kama Jaji wa kawaida, ilikuwa makosa makubwa zaidi kikatiba kumpandishacheo na kumfanya Jaji Kiongozi wakati alikwishafikisha umri wa kustaafu wa JajiKiongozi! Pili, kwa utamaduni uliozoeleka Tanzania, majaji wamekuwawanaongezewa kipindi kimoja cha miaka miwili ili wamalizie kesi walizokuwa nazohadi muda wao wa kustaafu unawadia. Kwa msimamo wa kikatiba ulioelezwa na Jajiwa Rufaa Luanda, Jaji Mkuu Ramadhani na Kikundi Kazi, siyo sahihi kwa JajiKiongozi Jundu kustaafu na kupewa mkataba wa kuendelea na wadhifa huokupindukia muda wake wa kustaafu kwa mujibu wa Katiba!  Nyongeza hii ya pili ya mkataba wa Jaji Kiongozi Jundu imewafanya watuwanaojiita ‘Watumishi wa Mhimili wa Mahakama' kumwandikia Msajili wa Mahakamaya Rufani ya Tanzania kulalamikia jambo hilo. Kwa mujibu wa barua yao, ambayopia ilinakiliwa kwa Mwanasheria Mkuu na Jaji Mkuu, watu hao wamesema yafuatayokuhusu Jaji Kiongozi Jundu: "Sisi watumishi wa Mahakama tunafahamu udhaifumkubwa kiutendaji alionao Jaji Kiongozi wetu wa sasa. Kimsingi hamudu madarakahaya. Ipo mifano mingi ya udhaifu wa Jaji Jundu. Mfano alimhamisha hakimukutoka kituo chake cha kazi kama adhabu kwa vile hakimu huyo alitoa maamuziambayo yeye hakuyafurahiya kwenye ile kesi maarufu ya kibaragashia. Ni busaraza Jaji Mkuu, Mohamed Chande Othman, ndizo zilizomsaidia hakimu huyo."

  sasa hapo kajibu kitu gani?
   
 10. Manyanza

  Manyanza JF-Expert Member

  #10
  Aug 31, 2012
  Joined: Nov 4, 2010
  Messages: 4,446
  Likes Received: 21
  Trophy Points: 135
  Sasa huyu Jaji Jundu kaongea nini? Bora angenyamaza yaani Tundu Lissu kaivua nguo serikali na yeye huyu jaji kaja kuropoka tu bora angenyamaza na hii yote ni kutokana na udhaifu wa raisi na serikali yake yeye anatoa uraji kwa washikaji zake bila kuzingatia kanuni na taratibu za ajira, hivi ni wangapi wenye taaluma zao wanapigika kitaa halafu huyu raisi anatoa favour kwa vishoka kama jaji Jundu....

  Big up Tundu Lissu hakuna anayeweza kupimana ubavu na wewe, maana Mwanasheria mkuu,Waziri wa Sheria na Katiba na wabunge wa CCM pamoja na wake zao CUF wameangukia pua kanyaga mwendo kamanda Lissu
   
 11. Henge

  Henge JF-Expert Member

  #11
  Aug 31, 2012
  Joined: May 14, 2009
  Messages: 6,767
  Likes Received: 78
  Trophy Points: 145
  kwani hii ilitokea mkuuu???
   
 12. M

  Moitalel Member

  #12
  Aug 31, 2012
  Joined: May 8, 2010
  Messages: 88
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Tetetete-Serikale ya Kikwete ndiyo hiyo---------Ero lete hiyo kisusion bana! nishuhudie hili gemu.
   
 13. P

  Precise Pangolin JF-Expert Member

  #13
  Aug 31, 2012
  Joined: Jan 4, 2012
  Messages: 12,202
  Likes Received: 1,978
  Trophy Points: 280
  Huko kenya kuna Majaji walitolewa mkuku na Tume Fulani hapa kwetu ikifanywa Kama Kenya tutabakia na Majaji sita
   
 14. bushman

  bushman JF-Expert Member

  #14
  Aug 31, 2012
  Joined: Nov 1, 2010
  Messages: 2,312
  Likes Received: 67
  Trophy Points: 145
  Hii nchi jk inaitumbukiza chooni tunamwangalia na kumchekea!!!!!!!!!!!!!
   
 15. lukindo

  lukindo JF-Expert Member

  #15
  Aug 31, 2012
  Joined: Mar 20, 2010
  Messages: 7,892
  Likes Received: 6,086
  Trophy Points: 280
  hata sisi wakiwepo sita wenye uwezo ni bora mara mia kuliko kuwa na majaji mia aliowasema Lissu. Better kufikiri juu ya quality na sio quantity!
   
 16. Kongosho

  Kongosho JF-Expert Member

  #16
  Aug 31, 2012
  Joined: Mar 21, 2011
  Messages: 36,126
  Likes Received: 306
  Trophy Points: 160
  Mmmh, hivi ni wajibu wa jaji kutetea majaji???

  Nilitegemea aliyeambiwa anaboronga kuchangua ndio atoe tamko.
   
 17. tembeleh2

  tembeleh2 JF-Expert Member

  #17
  Aug 31, 2012
  Joined: Jul 27, 2010
  Messages: 768
  Likes Received: 3
  Trophy Points: 35
  Hakujibu hoja hata moja ya Tundu Lissu. Nami naungana na wadau wengine wa maendeleo kwa kuuliza " KWA NINI AONGEZEWE MKATABA WAKATI WATU WENGINE WA KUFANYA KAZI HIYO WAPO?" au huyu jaji kiongozi ni SO SPECIAL kiasi kwamba hatakiwi kustaafu kwa sababu anafanya kazi ambayo wengine hawawezi kuifanya?
   
 18. Mikael P Aweda

  Mikael P Aweda JF Gold Member

  #18
  Aug 31, 2012
  Joined: Dec 17, 2010
  Messages: 2,934
  Likes Received: 33
  Trophy Points: 0
  Majaji makosa yao ni madogo, kukubali Kuteuliwa. Mwenye kujibu hoja ya msingi ni mteuaji - JK
   
 19. Mikael P Aweda

  Mikael P Aweda JF Gold Member

  #19
  Aug 31, 2012
  Joined: Dec 17, 2010
  Messages: 2,934
  Likes Received: 33
  Trophy Points: 0
  Lyimo,
  Zile hoja za Lissu kiukweli ni kwamba hazijibiki hata iweje. Watamchongea cheti cha degree ya Sheria Mbarouk aliyeko darasani na kuiback date? Akiambiwa walete walimu wako na classmate si ataumbuka?
   
 20. Mikael P Aweda

  Mikael P Aweda JF Gold Member

  #20
  Aug 31, 2012
  Joined: Dec 17, 2010
  Messages: 2,934
  Likes Received: 33
  Trophy Points: 0
  Henge,
  Jaji Mborouk, mmoja kati ya majaji 3 wanaosikiliza Rufaa ya Lema hana degree ya sheria. Je, kama yeye yuko pale kimizengwe atamtendea haki Lema? Si anajipendekeza kwa mteuaji wake anayegombana na Lema?

   
Loading...