Mzee Mwanakijiji
Platinum Member
- Mar 10, 2006
- 33,474
- 39,987
Naanza kumchunuku Jaji Kiongozi.. nimemfuatilia tangu alipoteuliwa na kwa namna fulani nimegundua kuwa haumi umi maneno na anasema kila anchomaanisha. Safari amenigusa kwenye jambo hili jingine la watuhumiwa kukaa rumande wakati "upelelezi unaendelea". Mara nyingi tumekuwa tukisikia haya pale watu wanakamatwa na kwa haraka wanafikishwa mahakamani halafu waendesha mashtaka wanadai kuwa mtuhumiwa asiachiliwe kwa sababu upelelezi unaendelea. Siyo hapo tu wakati mwingine mtu anaenda mahakamani kufuatilia kesi yake miaka nenda na kila ikitajwa wenye akili wetu wanatoa hoja iahirishwe kwa sababu upelelezi bado unaendelea.
Pendekezo langu ni kuwa wakati umefika kuwa mtu akifikishwa mahakamani lazima iwe ni pale ambapo upelelezi umefikia mahali pa kukamilika ili kesi kuanza. Na zaidi ya yote kesi isiahirishwe zaidi ya mwaka kwa kusubiri "upelelezi". Mahakama lazima ianze kupima ushahidi uliopo kwenye discovery na kutoa agizo kama kesi iendelee kuliko mtindo huu wa kuwaacha prosecutors kuahirisha kesi kwa muda mrefu. Na ninaamini huu ndio msimamo wa Jaji Kiongozi.
IPPMedia
[FONT=ArialMT, sans-serif]Jaji Kiongozi wa Mahakama Kuu nchini, Fakhi Jundu ameonyesha kutoa huruma kwa watuhumiwa wanaosota muda mrefu wakiwa magezani, ambapo amewataka Mahakimu kuanza utaratibu wa kuwaachia huru washtakiwa waliokaa magerezani muda mrefu endapo upelelezi wa kesi zao unasuasua.[/FONT]
[FONT=ArialMT, sans-serif]
[/FONT]
[FONT=ArialMT, sans-serif]Akiongea wakati akitoa tathimini ya ziara aliyoifanya ya kutembelea Mahakama za Mwanzo za Kanda ya Dar es Salaam, Jaji Jundu alisema wakati umefika sasa kwa mahakimu wa Mahakama za ngazi zote kutumia busara kwa kuangalia uwezekano wa kuzifuta kesi zote zinzooneka mwenendo wake sio nzuri ili kupunguza mrundikano ndani ya magereza.[/FONT]
[FONT=ArialMT, sans-serif]
[/FONT]
[FONT=ArialMT, sans-serif]Alisema, kuna watu wengi wanaendelea kukaa magerezani zaidi ya miaka mitano, ambapo ukichunguza kwa makini utabaini wanashindwa kuhukumiwa kutokana na waendesha Mashtaka kutomaliza upelelezi wa kesi zao.[/FONT]
[FONT=ArialMT, sans-serif]
[/FONT]
[FONT=ArialMT, sans-serif]"Nimetembelea ndani ya magereza nimegundua watu wengi wanaendelea kukaa magerezani kutokana na upelelezi wa kesi zao kutokamilika, huu sio utaratibu wa kutenda haki, huyu mtu atakaa gerezani kwa miaka mingapi ili upelelezi ukamilike?" alihoji Jaji Jundu.[/FONT]
[FONT=ArialMT, sans-serif]
[/FONT]
[FONT=ArialMT, sans-serif]"Kwa maana hiyo Mahakimu wanatakiwa kutokubaliana na utaratibu huu, waanze kutumia busara kwa kuwaachia huru washtakiwa hawa ili wakikamilisha upelelezi wao wawakamate tena ili wajibu kesi zao," alisema.[/FONT]
[FONT=ArialMT, sans-serif]
[/FONT]
[FONT=ArialMT, sans-serif]Akifafanua Jaji Kiongozi alisema, Mahakamu wana uwezo wa kutumia kifungu cha 225 cha makosa ya jinai, ambapo kinaeleza mtuhumiwa anaweza kuachiwa huru kama kosa lake halikuwa na ushahidi wa kutosha lakini anaweza kukamatwa tena kwa kosa hilo hilo endapo ushahidi utapatikana.[/FONT]
[FONT=ArialMT, sans-serif]
[/FONT]
[FONT=ArialMT, sans-serif]Sambamba na hilo, alisema amewaagiza Mahakimu wa ngazi za Wilaya na Mahakimu wakazi wa Mkoa kutembelea magereza mbalimbali kwa ajili ya kwenda kuzungumza na wafungwa wote ambao wameonekana kufungwa kimakosa au kupewa adhabu kubwa kulingana na kosa alilofanya.[/FONT]
[FONT=ArialMT, sans-serif]
[/FONT]
[FONT=ArialMT, sans-serif]Alisema amechukua hatua hiyo baada ya kumkuta mwanamke mmoja katika gereza la Bukoba akiwa amefungwa kutokana na kosa la kutolipa pesa alizokopeshwa, lakini kutokana na sababu zisizoeleweka alifunguliwa kesi ya jinai na kufungwa miaka mitano na kibaya zaidi wakati huo alikuwa na hali ya ujauzito.[/FONT]
[FONT=ArialMT, sans-serif][/FONT]
[FONT=ArialMT, sans-serif]"Nashukuru yule mama kajifungua akiwa ndani ya gereza, lakini hakutakiwa kufungwa kifungo kama kile kwa kuwa hakutakiwa kushtakiwa kwa kosa la jinai, alitakiwa kuwa na kesi ya madai ingawa hakimu na mwendesha mashtaka kwa namna wanavyoelewa wao walifanya hivyo," alisema jaji Jundu.[/FONT]
[FONT=ArialMT, sans-serif]
[/FONT]
[FONT=ArialMT, sans-serif]Katika ziara yake aliyoifanya katika Wilaya za Bagamoyo, Mkuranga na Kibaha, Jaji Jundu aliweza kushuhudia Mahakama za Kimanzichana na Kibaha zikiwa katika hali mbaya na kuwaomba Halmashauri za Wilaya wakishirikiana na wananchi kusaidia kujenga upya Mahakama ili huduma ziweze kutolewa katika hali bora.[/FONT]