Kiranga
Platinum Member
- Jan 29, 2009
- 71,274
- 105,471
Kwani haiwezekani kwamba kukawa na ushahidi wenye utata fulani, utata unaotakiwa kutatuliwa kwa kesi kusikilizwa, na hilo likasababisha mshtakiwa awe na kesi ya kujibu, hata kama ni kwa kujisafisha, na jaji kusema kuna kesi ya kujibu?Uko sawa. Lakini Jaji hawezi kutoa ruling kwamba mtuhumiwa ana kesi ya kujibu kama hajawa convinced na ushahidi uliotolewa na upande wa mashtaka kwamba mtuhumiwa ana hatia ya makosa mahsusi (specific offenses).
Inawezekana pia akawa hana hatia. Ndio maana, kufikia hatua hiyo, LAZIMA upande wa utetezi upewe nafasi kujitetea kwa ushahidi na vielelezo kupinga ruling hiyo ili kuthibitisha kuwa mtuhumiwa hana hatia.
Kwa DPP, hiyo ni point of no return - in a credible juridical process.
Kwani kuwa na kesi ya kujibu hakuwezekani kuletwa na technicality ambayo haina uhusiano wowote na mtu kuwa au kutokuwa na hatia?