Jaji Ihema wa tume ya Maadili ang'olewe! - Wafanyakazi

Mzee Mwanakijiji

Platinum Member
Mar 10, 2006
33,474
39,987
"ka nzi" kanakozunguka kwenye ofisi mbalimbali za serikali kamerudi na uchafu mwingine. Uchafu huu unadaiwa kuwa uko kwenye Tume ya Maadili ya Viongozi ambayo ndiyo chombo ambacho Watanzania wanatarajia kiwe cha kwanza kwa usafi. Wafanyakazi wanasema wamechoka, na wanataka mkuu wao ang'olewe na wameandika barua kadhaa kuanzia Ikulu na Ofisi ya Waziri Mkuu. Zifuatazo ni barua zao mbili ambazo KLHN imefanikiwa kuzipata kutoka kwa "ka nzi" ketu. Je ni kweli au ni uzushi? amua mwenyewe.
 

Attachments

  • hojadhidiyaihema.pdf
    17.9 KB · Views: 379
  • kutakaihemaaondoke.pdf
    13.3 KB · Views: 244
Last edited by a moderator:
Kwa wale wanaomfahamu Jaji Ihema, wanamuelezea kuwa ni mtu wa namna gani? Je picha inayochorwa na madai haya dhidi yake ina ukweli wowote ule?
 
Mkjj, msanii JK aliunda tume kuchunguza tuhuma dhidi ya ufisadi uliofanywa na Richmond/Dowans. Moja ya recommendations zao ni kuondolewa Hosea pale TAKUKURU, lakini hadi hii leo bado anapeta tu!!! Sijui kuna umuhimu gani wa kuunda tume zinazotumia mabilioni ya fedha ili kufanya kazi waliyotumwa na mheshimiwa, halafu recommendations zao wanazotoa hazifanyiwi kazi yoyote na mheshimiwa!!!! Pamoja na Wafanyakazi kutaka huyu fisadi aondolewe hapo haraka iwezekanavyo, tusishangae kumuona anaendelea kupeta tu maana nchi yetu kwa sasa ni kama haina uongozi wowote ule
 
Mwanakijiji haka ka-inzi katawasumbua sana. Ha ha ha aaaaaaaaaaaa...............kengine kapo hapa JF LOL.

Dawa yake waache UFISADI
 
Mkuu Mwanakijiji,

Heshima Mbele,

Mie nahisi vyeo vote vya kuteuliwa na Rais huwa vina matatizo na huwa siyo Rahisi kwa mwenye Nchi kumng'oa mtu bila mashauriano kati ya vyombo vya usalama na mwenye nafasi hiyo.

Mie nadhani Wananchi wawe wanachagua kila kiongozi wanayemtaka akae sehemu flani na akishindwa wanamng'oa.
 
hahahahah Gembe.. does that include the President... usikose makala yangu ya kesho.
 
hahahahah Gembe.. does that include the President... usikose makala yangu ya kesho.
Yes,as long as he needs votes from Wananchi...I will read it kama Gazeti litakuwa kwenye mtandao..hope ni TZDaima?or on the other part i love to read?
 
both kesho we are taking a notch higher... ila ungelipata la mtaani ungependa zaidi kwani lina kakatuni kazuri (nimeambiwa). In the tradition of "Ndege ya Lowassa" and "Kasungura ka Lowassa". But b'cause Lowassa is not there so, we'll go for something more exciting.

Nikirudi kwenye mada though, kama hawa watumishi wa tume ya maadili wanaona mambo hayaendi vizuri na hawasikilizwi na uendeshaji ni wa kiubabaishaji je kweli wanaweza kuangalia maadili ya viongozi wetu kweli? Kama walikuwa na muda wa kukaa chini kuandika vitu hivyo, ina maana huyo mtu hakuwa na muda wa kuandika ripoti ya maadili juu ya kiongozi fulani.

Sasa tunaweza kuwasaidia vipi?
 
Kwa wale wanaomfahamu Jaji Ihema, wanamuelezea kuwa ni mtu wa namna gani? Je picha inayochorwa na madai haya dhidi yake ina ukweli wowote ule?
Kwa mujibu wa tarifa za kimahakama mahakama toka kwa wadau wa judiciary jaji Ihema hata kuteuliwa kwake na mkapa was very questionable kwani katika judiciary alikuwa na tuhuma nyingi tu za rushwa,kila mtu aliishia kunung'unika tu,hatushangai leo kuwa hao jamaa hawamtaki.
 
Yes,as long as he needs votes from Wananchi...I will read it kama Gazeti litakuwa kwenye mtandao..hope ni TZDaima?or on the other part i love to read?

Jk kavotiwa na wengi je anapendwa kweli?? je anafanya kazi ya wananchi sawasawa??? tanzania dem,okrasia ya kura bado sana tuu
 
sasa mtu aliyezungukwa na tuhuma za rushwa ndiyo anapewa kusimamia maadili?

Aaaah, Mkjiji Kwa Bongo hii ni kama kunywa maji vile, kwani humuoni Hossea anavopeta kwa raha zake japo alitueleza RICHMONDI safiiiii! Na yeye mwenyewe ni mwanatume ya kuchunguza wezi wa wa EPA?? Hapo inabakia vile vile nani amfunge paka Kengele period!


Ni mwendo mdundo ( JK 2005)
 
Hayo ni sawa na maajabu ya Chenge kuwa Mwenyekitiw a Kamati ya Maadili ya CCM!

Hey MN,

kwa mujibu wa Peter Kisumo hilo halina shida kabisa katika Uongozi wa Tanzania, as long huyo mwenye cheo anatetea chama chake (CCM) na kumsaidia JK! Sasa tujiulize JK anasaidiwa katika lipi?
 
well.. kwani maadili ni nini hasa? maana naona ni kitu kinachozungumzwa sana lakini hatujakipa maana yake hasa labda ndio sababu watu kama kina Chenge au Ihema ndio wanapewa nafasi hizo. Halafu huyu jaji anadaiwa kupendelea Wasukuma.
 
Huyu mpuuzi kwanini anawatesa wafanyakazi? Inabidi barua zao zisipojibiwa basi wafanyakazi hao wagome maanke hiyo ilikua njia mojawapo ya diplomasia iliyoshindikana.Nimekuja kugundua kwamba hapo Tanzania watu hawawezi kusikia malalamiko na kuyafanyia kazi unless tutumie nguvu.

Jaribuni kutumia hii option ili kumwondoa huyu dikteta.Pia mwanakijiji jaribu kumtafuta huyu fisadi uhojiane nae ili ajue kuna watu wana uchungu na madudu yake anayofanya.that's very reckless governance bwana.Hah!
 
well.. kwani maadili ni nini hasa? maana naona ni kitu kinachozungumzwa sana lakini hatujakipa maana yake hasa labda ndio sababu watu kama kina Chenge au Ihema ndio wanapewa nafasi hizo. Halafu huyu jaji anadaiwa kupendelea Wasukuma.

Ala!! kumbe ni mkabila pia.......
 
Back
Top Bottom