Jaji Ihema wa tume ya Maadili ang'olewe! - Wafanyakazi

Mzee Mwanakijiji

Platinum Member
Mar 10, 2006
33,178
2,000
Nyani.. siyo madai yangu ni ya hao jamaa; lakini ni vigumu kuamini kwa msukuma kuwa mkabila. Nadhani hapo wanaweza kuwa wamekosea kwani katika Tanzania ukabila unadaiwa kuwa ni domain ya watu wa eneo fulani la nchi yetu. koh koh koh...
 

WomanOfSubstance

JF-Expert Member
May 30, 2008
5,462
0
Nyani.. siyo madai yangu ni ya hao jamaa; lakini ni vigumu kuamini kwa msukuma kuwa mkabila. Nadhani hapo wanaweza kuwa wamekosea kwani katika Tanzania ukabila unadaiwa kuwa ni domain ya watu wa eneo fulani la nchi yetu. koh koh koh...


Bonge la innuendo Mkuu!
I like that... hahahhhhaaaaa
 

kaiyurankuba

Member
May 16, 2008
55
0
This is an institutional issue. Tume ya maadili imeundwa ili ishindwe kufanya kazi yake na siyo ifanikiwe. Ndiyo maana issue za bajeti, financial controls, administrative procedures vinapuuzwa. uongozi wa sasa wa tanzania ndio unanufaika na tume ya maadili inayoongozwa kama kilabu cha pombe za kienyeji (mpika gogo ndio huyo huyo muonjaji, muuzaji na dj pia!!). na hii siyo taasisi pekee ambayo ina matatizo ya aina hii.

tume inayoendeshwa namna hii, haiwezi hata siku moja ikasimamia utekelezaji wa maadili ya uongozi ama kuchukua hatua zinazostahili kwa wakati unaostahili kwa viongozi wanaokiuka maadili kwani tume yenyewe imeundwa isifuate maadili! yote hii ni kwa faida ya mafisadi.
 

Gustanza_The

Senior Member
Aug 6, 2008
126
0
Mie nahisi vyeo vote vya kuteuliwa na Rais huwa vina matatizo na huwa siyo Rahisi kwa mwenye Nchi kumng'oa mtu bila mashauriano kati ya vyombo vya usalama na mwenye nafasi hiyo. Mie nadhani Wananchi wawe wanachagua kila kiongozi wanayemtaka akae sehemu flani na akishindwa wanamng'oa.

Nyogeza: Nahisi solution hapa ni kuwa na Serikali za Majimbo. Kama tungekuwa na serikali za majimbo, basi ingekuwa rahisi sana kuwakaba mashati/dhibiti hao wanaoleta upuuzi wa kiutendaji.

Tatizo ni kwamba, serikali kuu imekuwa kubwa mno. Uwajibikaji ni zero. Na ukibahatika ukapewa nafasi kama Jaji Stephen Ihema alivyobahatika, then kinachofuata ni kurudisha fadhila kwa hao waliokuweka kwenye hiyo nafasi.

Point ni kwamba, Jaji Ihema, hana uchungu kwa wakazi wa Tarime (kwasababu hatoki huko) wanaochafuliwa mazingira na kunyang'anywa maeneo yao ili kuipisha Barrick Gold Corp iibe maliasili zetu, wala hana uchungu hata kidogo na wakazi wa Kahama ambao nao pia wako mbioni ku-face the same fate.

Ila kama tungekuwa na Serikali za majimbo kisha kuzipatia power Local Governments, basi ungesikia moto unavyowaka (huko Tarime, Barrick wangeshang'oa nanga siku nyingi!).
 

Nemesis

JF-Expert Member
Feb 13, 2008
5,013
2,000
Nyani.. siyo madai yangu ni ya hao jamaa; lakini ni vigumu kuamini kwa msukuma kuwa mkabila. Nadhani hapo wanaweza kuwa wamekosea kwani katika Tanzania ukabila unadaiwa kuwa ni domain ya watu wa eneo fulani la nchi yetu. koh koh koh...

Mzee Mwanakijiji umesema kweli, kabila kubwa Tanzania ni wasukuma lakini hawana/hatuna tabia za ukabila kabisa. Ila bado kwa mtu mmoja binafsi inaweza kutokea yaani ikawa ni tabia yake tu kama unavyoweza kubahatika kumpata mnyakyusa mnyimi (asiye mkarimu).
 

Mwita Maranya

JF-Expert Member
Jul 1, 2008
10,565
2,000
Mzee Mwanakijiji umesema kweli, kabila kubwa Tanzania ni wasukuma lakini hawana/hatuna tabia za ukabila kabisa. Ila bado kwa mtu mmoja binafsi inaweza kutokea yaani ikawa ni tabia yake tu kama unavyoweza kubahatika kumpata mnyakyusa mnyimi (asiye mkarimu).

Imeshaelezwa hapa kuwa Jaji Ihema alikuwa na tuhuma nyingi tangu akiwa mahakama kuu, tuhuma za rushwa na tabia nyingine ambazo ni kinyume na maadili ya taaluma na utumishi wake kama mtoa haki.Kwahiyo huyu mtu ana matatizo yake binafsi wala haiwezi kulinganishwa na ukabila uliowahi kuzungumzwa hapa, ukabila unaofanywa kwa makusudi kabisa kwa kiwango kikubwa.Kwahiyo MMKJJ wala usilazimishe kikohozi, kwakuwa hutaki kukubaliana na ukabila unaotajwa dhidi ya watu fulani ambao wewe ni mtetezi wao.
Kwakuwa wafanyakazi wametuonyesha namna Ihema anavyowaburuza na kuendesha taasisi hiyo kidikteta, ni vizuri tujikite kuujadili huo udikteta wake badala ya kutaka kuhamisha mada kwenda kwenye ukabila ambao katika barua za wafanyakazi hawajautaja.
 

Mzee Mwanakijiji

Platinum Member
Mar 10, 2006
33,178
2,000
Ungesoma hizo barua usingefikia hiyo hatima; na mimi na ukabila ni vitu viwili tofauti. Mtu akiudai tu ninashtuka. Soma tena hizo barua halafu uje tena ujaribu.
 

WomanOfSubstance

JF-Expert Member
May 30, 2008
5,462
0
Mzee Mwanakijiji umesema kweli, kabila kubwa Tanzania ni wasukuma lakini hawana/hatuna tabia za ukabila kabisa. Ila bado kwa mtu mmoja binafsi inaweza kutokea yaani ikawa ni tabia yake tu kama unavyoweza kubahatika kumpata mnyakyusa mnyimi (asiye mkarimu).

Kwani ukabila ni nini na unaanzaje? unasababishwa na nini?
How can you claim kuwa hamna ukabila... it is for others to judge and not you.
Huyu hapa msukuma mwenzio sasa...anatuhumiwa kwa ukabila!
 

WomanOfSubstance

JF-Expert Member
May 30, 2008
5,462
0
Imeshaelezwa hapa kuwa Jaji Ihema alikuwa na tuhuma nyingi tangu akiwa mahakama kuu, tuhuma za rushwa na tabia nyingine ambazo ni kinyume na maadili ya taaluma na utumishi wake kama mtoa haki.Kwahiyo huyu mtu ana matatizo yake binafsi wala haiwezi kulinganishwa na ukabila uliowahi kuzungumzwa hapa, ukabila unaofanywa kwa makusudi kabisa kwa kiwango kikubwa.Kwahiyo MMKJJ wala usilazimishe kikohozi, kwakuwa hutaki kukubaliana na ukabila unaotajwa dhidi ya watu fulani ambao wewe ni mtetezi wao.
Kwakuwa wafanyakazi wametuonyesha namna Ihema anavyowaburuza na kuendesha taasisi hiyo kidikteta, ni vizuri tujikite kuujadili huo udikteta wake badala ya kutaka kuhamisha mada kwenda kwenye ukabila ambao katika barua za wafanyakazi hawajautaja.

Mkuu!
Mwanzo wa ngoma ni lele.... tusubiri kusikia zaidi
 

kisiju

New Member
Aug 7, 2008
1
0
nimewasikiliza wana forum wenzangu, mimi nimevutiwa na namna wengi wenu weye kumjua huyu jaji ihema, kama mmoja wenu alivyosema jaji ihema akiwa mahakama kuu alikosa maadili kabisa,alipokea rushwa na kupendelea kesi za wasukuma, na aligombana mara kwa mara na jaji mkuu mstaafu barnabas samata hadi kufikia samata kutishia kujiuzulu endapo jaji ihema angeongezewa mkataba wa kuendelea kuwa jaji mahakama kuu, ndo muone ni kiongozi gani waliye naye tume ya maadii

na suala la kuteuliwa kwake kuwa kamishna wa maadili mwaka 2005, liligubikwa na utata mno, maana utumishi hawakumshortlist kwenye majina matatu yanayotakiwa kupelekwa kwa rais kwa ajili ya uteuzi, na hata waziri muhusika wa wakati huo wilson masilingi alirukwa katika suala hili, na mtu aliyempigia debe jaji ihema kuwa kamishna wa maadili ni ndugu ANDREW CHENGE, ni msukuma wa bariadi shinyanga, na jaji ihema ni msukuma wa kahama shinyanga, mara ikatangazwa kuwa jaji mstaafu stephen Ihema ameteuliwa na rais mkapa kuwa kamishna wa maadili, habari hii iliwastua hata utumishi wenyewe waliopendekeza majina matatu ambapo jina la ihema halikuwepo, hata majaji wenzake walishangazwa sana kwa ihema kuteuliwa kwani walimju kwa kuosa maadili

Baada ya kuanza kazi katika tume hiyo akakuta muundo wake unampa madaraka makubwa mno, na kwa kuwa anajiona anajua mambo yote kuliko mtu yeyote hapa duniani
na akakuta wafanyakazi ambo ni waoga mno, wasioweza kumpinga kwa lolote lile, ni mbabe kupindukia, hasikilizi ushauri wa yeyote, anatumia magari ya serikali kuhudumia mashamba yake huko mkuranga na tegeta, anafuja fedha za tume kwa maslahi yake na hataki watu wahoji lolote
lakini kwa kuwa kuna damu mpya imeingia ndani ya tume hii,ndo maana umma unaanza kujua kinachoendelea , lakini kwa kuwa wana dhamira ya dhati, ni lazima jaji ihema atango'ka hata kwa winchi, mkataba wake unaisha mwaka 2010, lakini kwa sababu uoza umezidi katika tume hii, ni lazima atangolewa kabla ya 2010 ili asizidi kuichafua serikali na habari zake zinajulikana ikulu kitambo

katika uongozi wake hamna chochote kilichofanyika kuhusiana na uchunguzi wa maadili ya viongozi, anafanya usanii tu na kula fedha za serikali

habari ndo hiyo
 

Kungurumweupe

JF-Expert Member
Jun 17, 2008
317
0
Mzee Mwanakijiji umesema kweli, kabila kubwa Tanzania ni wasukuma lakini hawana/hatuna tabia za ukabila kabisa. Ila bado kwa mtu mmoja binafsi inaweza kutokea yaani ikawa ni tabia yake tu kama unavyoweza kubahatika kumpata mnyakyusa mnyimi (asiye mkarimu).


Mkuu nziku,

Nakubaliana na wewe kuwa ninyi wasukuma ni wengi hapo tz yaani mko zaidi ya 30% ya watz wote. Lakini sikubaliani na wewe unaposema ninyi hamna ukabila kabisa!

Ni kweli wasukuma tunawafahamu kwa ukarimu na upole wenu, lakini hiyo haimanishi kuwa hamuna ukabila hata chembe! Labda kama ulikusudia kusema kuwa ukabila wenu si mkubwa na haunuki kama ule wa wenzenu wachaga. Hapo nitakuelewa!

Hoja hapa ni kwamba huyu mkulu wa tume ya maadili hajui na hawezi kusimamia maadili ya viongozi na watumishi wa umma wa tz. Huenda aliwekwa pale kwa malengo maalumu ya kuwalinda viongozi mafisadi akina mkaapo na wenzake. Hivo inabidi aachie ngazi ili awekwe mwingine ambaye hatimaye atasaidia kufichua maovu ya viongozi wasio waadilifu hasa wale waliotoa taarifa za uongo juu ya mali zao kabla na baada ya uongozi wao katika taasisi za umma.
 

Mzee Mwanakijiji

Platinum Member
Mar 10, 2006
33,178
2,000
Unaona jinsi sumu ya ukabila inavyokula.... ukishauona mahali fulani lazima uuone kwingine na mkimalizana mnatafuta kitu kingine cha kubagua n.k Ni sumu mbaya sana. Kama Ihema alifanya kitu cha upendeleo tusihusishe na Kabila zima au kudemonize jamii nzima ya watu kwa kitendo cha mtu mmoja.
 

Mavanza

Member
Jun 12, 2008
38
0
Mkjj, msanii JK aliunda tume kuchunguza tuhuma dhidi ya ufisadi uliofanywa na Richmond/Dowans. Moja ya recommendations zao ni kuondolewa Hosea pale TAKUKURU, lakini hadi hii leo bado anapeta tu!!! Sijui kuna umuhimu gani wa kuunda tume zinazotumia mabilioni ya fedha ili kufanya kazi waliyotumwa na mheshimiwa, halafu recommendations zao wanazotoa hazifanyiwi kazi yoyote na mheshimiwa!!!! Pamoja na Wafanyakazi kutaka huyu fisadi aondolewe hapo haraka iwezekanavyo, tusishangae kumuona anaendelea kupeta tu maana nchi yetu kwa sasa ni kama haina uongozi wowote ule

Babu kukumbusha tu ni kuwa msanii JK hakuunda tume ya Richmond isipokuwa ilikuwa kamati teule ya bunge. Nafikiri hii inaweka uzito zaidi. Azimio la Bunge ni kuwa Hosea na Mwanyika waachie ngazi, lakini bado wapo tu. Hiki kiburi dhidi ya chombo kinachowakilisha wananchi wanakitoa wapi? Kama wanadharau bunge ujue tu wana mtu juu anayewapa hicho kiburi na si mwingine isipokuwa JK. Serikali ya uswahiba sijui itatufikisha wapi!!!!!!!
 

Fidel80

JF-Expert Member
May 3, 2008
21,954
2,000
Hivi hawa mafisadi tutawalea mpaka lini?
Kwa taarifa yenu JK ndiye anaye walea hawa mafisadi na si mwingine,kama uchafu wanaofanya anaujua A-Z kwa nini asiwashughulikie?
Ndipo tunakuja kupata jibu kuwa mafisadi wana UBIA na urais wa JK.Full stop hapa dawa ni kumng'oa huyu baba yao JK tubadilishe au tufumue kabisa uongozi wote.
 

Fidel80

JF-Expert Member
May 3, 2008
21,954
2,000
katika uongozi wake hamna chochote kilichofanyika kuhusiana na uchunguzi wa maadili ya viongozi, anafanya usanii tu na kula fedha za serikali

Hawa tume ya maadili wanajisifia kwa kulinda maadili ya mafisadi tu mbona hakuna hata kiongozi mmoja walio muwajibisha?Fedha za walipa kodi zitakuja watokea puani.
 

Mwita Maranya

JF-Expert Member
Jul 1, 2008
10,565
2,000
Ungesoma hizo barua usingefikia hiyo hatima; na mimi na ukabila ni vitu viwili tofauti. Mtu akiudai tu ninashtuka. Soma tena hizo barua halafu uje tena ujaribu.

MMKJJ,
Nimesoma tena na tena hizo barua mbili, nilichokiona ni hiki hapa, nanukuu:

"Amewagawa watumishi katika matabaka mawili, lakwanza ni wale wanaomsujudia, wasiompinga ambao yeye anawapendawakiwemo wa kabila lake(wasukuma) na la pili ni lile asilolipenda......." mwisho wa kunukuu.

na ukisoma zaidi hizo barua unagundua kuwa Ihema na tuhuma nyingine kubwa ya matumizi mabaya ya fedha za idara, mathalani kujilipa fedha nyingi kwa ajili ya vikao na kujichotea sh.milioni 3 kila mwaka kwa ajili ya likizo n.k

kwahiyo mtazamo wangu ni kwamba, Ihema anawapendelea hata wasiokuwa wasukuma ilimuradi hawampingi na au wanamsujudia!
 

BAK

JF-Expert Member
Feb 11, 2007
114,195
2,000
Uteuzi wake Tume ya Maadili wahojiwa

na Mwandishi Wetu
Tanzania Daima~Sauti ya Watu

WAKATI Rais Kikwete akiishambulia Tume ya Maadili ya Viongozi wa Umma katika hotuba yake bungeni wiki iliyopita, yameibuliwa madai ya wafanyakazi wa tume hiyo, yanaoonyesha udhaifu wa utekelezaji wa kazi na ukiukwaji mkubwa wa maadili ndani ya tume.

Wafanyakazi wa tume hiyo wanadai kuwa utendaji wa chombo hicho umekuwa wa mashaka kutokana na uamuzi wenye utata uliofanywa na Rais mstaafu wa Awamu ya Tatu, Benjamin Mkapa, kumteua Jaji mstaafu Stephen Ihema, ambaye rekodi ya utendaji kazi wake si ya kuridhisha, kuwa Kamishna wa Maadili wa tume hiyo.

Katika barua ya wafanyakazi hao waliyomwandikia Katibu Mkuu Kiongozi, Philemon Luhanjo, Julai 10 mwaka huu, na gazeti hili kupata nakala yake, wafanyakazi hao wanaeleza kuwa uamuzi wa Mkapa kumteua Jaji mstaafu Ihema kushika wadhifa huo, uliwashangaza wanasheria wengi, akiwemo aliyekuwa Jaji Mkuu wa Tanzania, Barnabas Samatta.

Wanadai kuwa Mkapa alimteua Jaji mstaafu Ihema kuwa bosi wa tume hiyo huku akijua kuwa aliyekuwa Jaji Mkuu, Samatta, alitishia kujiuzulu wadhifa wake iwapo Ihema angeongezewa muda wa utumishi katika Mahakama Kuu ya Tanzania kwa sababu ya kukiuka maadili ya kazi.

“…Chombo hiki kimekosa uongozi bora, tunamaanisha viongozi wakuu wa idara hii, kwa maana ya Kamishna wa Maadili na makatibu wawili wanaoshughulika na viongozi wa utumishi wa umma na viongozi wa siasa, Kamishna wa Maadili ndiye mkuu wa idara hii na pia ndiye Ofisa Maduhuli ( Accounting Officer).

“Jaji mstaafu Ihema aliteuliwa Oktoba 2005 na Rais mstaafu Benjamin Mkapa kuwa Kamishna wa Maadili, hatujui ni vigezo gani vilitumika kwa kuwa hata majaji wenzake na wanasheria wengine walishangazwa sana na uteuzi wake kwa namna walivyomjua kwa kukosa uadilifu….. na kiburi dhidi ya Jaji Mkuu Samatta, ambaye alishawahi kumuonya dhidi ya tabia yake ya kutoamua kesi kwa muda unaostahili.

“Na alipoomba kuongezewa mkataba Mahakama Kuu baada ya kustaafu ujaji, Jaji Mkuu mstaafu Samatta, alitishia kujiuzulu iwapo angepewa mkataba wa kuendelea na kazi ya ujaji, hii yote inaonyesha ni aina gani ya kiongozi tuliyenaye hapa Sekretarieti ya Maadili,” inasomeka sehemu ya barua hiyo.

Wafanyakazi hao wanamtuhumu Jaji Ihema kwa kukiuka taratibu za fedha kwa kuhodhi madaraka ya kupanga bajeti ya chombo na kutumia fedha anavyotaka, jambo ambalo limeondoa morali ya kazi ya watumishi walio chini yake.

Wanaeleza zaidi katika kile kinachoonyesha kuwa mkakati wake wa kujijengea wigo wa kutoingiliwa na mtu yeyote katika maamuzi yake, alimteua mmoja wa watumishi wa tume hiyo (jina tunalo), kuwa mhasibu mkuu, lakini wafanyakazi hao wanadai kuwa mteule huyo hana sifa za kushika wadhifa huo.

“Watumishi tumekuwa tukiambiwa ofisi haina fedha, lakini inapotokea safari inayomhusu Ihema au mhasibu mkuu, fedha zinapatikana mara moja,” inaeleza zaidi barua hiyo.

Wafanyakazi hao katika barua yao, pia wanamtuhumu bosi wao huyo kwa kushirikiana na mhasibu mkuu kukandamiza haki za wafanyakazi, ikiwa ni pamoja na kuwanyima posho za safari na kuwapunja stahili zao nyingine na kwa kutumia mwanya walionao wa kutoruhusu mtu yeyote kujua mpangilio wa bajeti ya ofisi hiyo.

Wanadai kuwa wawili hao wamefanikiwa kuandaa taarifa ya matumizi ya tume isiyo ya kweli na kuiwasilisha kwa Mkaguzi na Mdhibiti Mkuu wa Serikali, aliyetoa hati safi wakati fedha nyingi zinafujwa.

Walipendekeza serikali kuepuka kuteua watu waliostaafu utumishi wa umma kuongoza idara nyeti za umma kwa sababu mara nyingi wateule hao hujali zaidi masilahi yao kuliko kuutumikia umma.

Katika mapendekezo mengine, walimtaka Katibu Mkuu Kiongozi, Philemon Luhanjo, kumuamuru Ihema afuate maelekezo ya Wizara ya Fedha ya kugawanya bajeti kwa mujibu wa vitengo vilivyoidhinishwa, na wakuu wa idara husika wasimamie wenyewe mafungu yao bila kushinikizwa naye.

Aidha, walipendekeza kuwa, kiundwe cheo cha Mkurugenzi Mkuu wa Sekretarieti, mwenye taaluma ya uongozi atakayekuwa Ofisa Maduhuli, ili kuinusuru tume na ubadhirifu unaofanyika sasa.

Pia walipendekeza kuwa katika mchakato wa kurekebisha sheria, kuwepo muundo wa utumishi maalumu kwa watumishi wa sekretarieti, kwa vile mbali na kazi ya kutunza daftari la mali na madeni ya viongozi wa umma, wana dhima nzito ya kuchunguza uvunjifu wa maadili kwa viongozi tangu ngazi ya rais hadi wakurugenzi.

Jitihada za Tanzania Daima Jumapili kumpata Jaji Ihema kuzungumzia madai hayo ya wafanyakazi, kwa muda wa wiki mbili hazikuweza kufanikiwa, ambapo kila mara katibu muhtasi wake alidai kuwa bosi wake ana kazi nyingi, licha ya ahadi kadhaa zilizotolewa na katibu wake huyo kuwa apewe muda wa kujiandaa kuzungumzia madai hayo.

Naye Katibu Mkuu Kiongozi hakupatikana alipofuatwa ofisini kwake katikati ya wiki hii.
 

Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Top Bottom